Hakuna Utendewaji Maalum katika Kanisa
Liu Xin Mji wa Liaocheng, Mkoa wa Shandong
Baada ya kumfuata Mungu kwa miaka hii, nilihisi kuwa nilikuwa nimevumilia mateso na kulipa gharama fulani, kwa hiyo nilianza kuyategemea mapato yangu ya zamani na kuringia ukubwa wangu. Niliwaza: Nimeondoka nyumbani kwa miaka mingi na familia yangu haijaisikia kutoka kwangu kwa muda mrefu. Katika hali hii, kanisa hakika litanitunza.
Hata nisipofanya kazi yangu vizuri hawatanituma nyumbani. Si zaidi ya hayo wataniondoa tu na kunielekeza kufanya kazi nyingine. Kutokana na kufikiri kama huko, sikuwa na mzigo wowote kamwe katika kazi yangu. Nilipuuza kila kitu, na hata nikaiona kazi ya injili kama mzigo, daima nikiishi katikamatatizo na visingizio. Hata kama nilihisi moyo wangu kama umeshutumiwa na dhamira yangu kulaumiwa kwa sababu nilimwia Mungu mengi zaidi kupitia kwa tabia yangu ya uzembe, na kwamba ningeondoshwa siku moja, bado tu nilitangatanga pamoja na fikira ya kutumaini kupata bahati zaidi, nikipoteza wakati wa siku zangu kwa kuzembea katika kanisa.
Mungu ni mwenye haki na mtakatifu. Hatimaye, baada ya kuvuruga kazi yangu kabisa kupitia kwa shughuli zangu za muda mrefu za uzembe, nilifukuzwa na kutumwa nyumbani ili kutafakari kujihusu. Wakati huo, nilitiwa bumbuazi: Je, wangewezaje kukosa kunionyesha nadhari kidogo zaidi? Baada ya kufanya kazi kwa miaka mingi sana, sasa ninalazimika kwenda nyumbani, hivyo tu. Lakini ninawezaje kukabiliana na familia yangu nikirudi nyumbani sasa? Nitakuwa na matumaini gani wakati ujao? ... Moyo wangu ulikuwa na machafuko mno na nikajaa suitafahamu na lawama kumwelekezea Mungu. Nilianguka katika giza, nikipambana katika maumivu.
Katikati ya mateso ya kuzidi kiasi, nilikuja mbele ya Mungu na kumwita Yeye: Ee Mungu, siku zote nilifikiri kwamba baada ya kufanya kazi mbali na nyumbani kwa miaka yote hii na kuvumilia mateso fulani, kanisa halingenitendea hivi. Sasa ninaishi katika giza, moyo wangu umejaa suitafahamu na lawama kukuelekea Wewe. Tafadhali nihurumie tena ili nipate kupokea nuru Yako na mwongozo katika giza. ... Baada ya kuomba mara kwa mara jinsi hii mara kadhaa, neno la Mungu lilinipa nuru. Siku moja, Niliona maneno haya ya Mungu: “Mimi Sitakuwa na hisia ya huruma kwa wale ambao wanateseka kwa miaka mingi na kufanya kazi kwa bidii bila matokeo yoyote. Hata sivyo, Mimi Huwachukulia wale ambao hawajatosheleza madai Yangu kwa adhabu, sio zawadi, sembuse huruma. Labda mnawaza kwamba kwa kuwa mfuasi kwa miaka mingi unaweka bidii katikabila kujali hali yoyote, hivyo kwa namna yoyote unaweza kupata bakuli la mchele katika nyumba ya Mungu kwa kuwa mtendaji huduma. Ningesema wengi wenu mnafikiri hivi kwa sababu mmekuwa siku zote hadi sasa mkifuatilia kanuni ya jinsi ya kujinufaisha na jambo fulani bila kuwa na manufaa kwa wengine. Hivyo Mimi nawaambia sasa katika uzito wote: Sijali jinsi kazi yako ya bidii ni ya kutunukiwa, jinsi sifa zako ni za kuvutia, jinsi unanifuata Mimi kwa karibu, jinsi una umashuhuri, au jinsi umeendeleza mwelekeo wako; mradi hujafanya kile Ninachodai, kamwe hutaweza kushinda sifa Zangu. … kwa sababu Siwezi kuwaleta maadui Wangu na watu waliojawa na maovu kwa mfano wa Shetani katikaufalme Wangu, katika kipindi kijacho” (“Dhambi Zitampeleka Mwanadamu Jahanamu” katikaNeno Laonekana katika Mwili). Kila neno la Mungu lilifichua uadhama Wake na ghadhabu, likinichoma moja kwa moja katika sehemu yangu ya udhaifu mkuu kama upanga wenye sehemu mbili za makali, na kuangamiza kabisa ndoto yangu ya "kuweza angalau kupata riziki katika kanisa bila kujali lolote kwa sababu ya kazi niliyoifanya, hata kama si yenye kustahili." Kwa wakati huu, sikuwa na budi ila kutafakari kujihusu: Ingawa niliondoka nyumbani na nimekuwa nikitimiza wajibu wangu nje kwa miaka hii michache iliyopita, nikionekana kwa nje kuwa nimelipa gharama kiasi na kuteseka kidogo, sikuhisi huzuni ya Mungu hata kidogo, na kamwe sikuwahi kufikiria jinsi ya kutimiza wajibu wangu ipasavyo ili kumridhisha Mungu. Badala yake, nilitenda kwa uzembe katika kushughulika na kazi yangu. Hasa katika kipindi hiki, sikuwa na mzigo wowote kamwe katika kazi yangu ya injili na hata sikuchukua sehemu ya haki ya injili ya kanisa, bila kujali kama niliikamilisha au la na bila kuhisi kama nilimwia Mungu chochote. Hata niliichukulia kazi ya injili kama mzigo, nikifikiri kuwa kama watu wapya zaidi ni lazima waje na siwezi kupata mtu yeyote wa kuwanyunyizia hata itakuwa ya udhia zaidi. Kwa hiyo, sikuonyesha shauku yoyote katika kazi ya injili na niliisababishia kupitia hasara kubwa. Kwa kuwa sikuzingatia kazi ya kuwanyunyizia watu wapya, ilisababisha waumini wengine wapya kuondoka kwa sababu hawakuwa na yeyote wa kuwanyunyizia. Kanisa lilinipangia kupata familia wenyeji na kushughulikia baadhi ya mambo mengine ya kawaida, lakini bado nilikuwa nikiishi katika matatizo na visingizio, nikikataa kushirikiana na Mungu. Zaidi ya hayo, niliridhika na hali yangu ya wakati huo na sikutafuta maendeleo, kuwa nimeharibika tabia kwa kiasi fulani na kupoteza pakubwa kazi ya Roho Mtakatifu, na kusababisha vipengele mbalimbali vya kazi ya kanisa kuanguka katika machafuko. ... Nilifikiri kuhusu tabia yangu: Je, hili lilikuwa linatimiza wajibu wangu vipi? Lilikuwa ni kufanya uovu tu! Lakini kwa kweli nilihisi kuwa, hata kama kazi yangu haingekuwa yenye kustahili, nilikuwa angalau nimefanya kazi ngumu, na kwamba bila kujali nini, ni lazima angalau ningeweza kujikimu kimaisha katika kanisa. Kanisa lilipopanga nirudi nyumbani ili kutafakari kujihusu, hata nilihisi kwamba nilikuwa nimekosewa. Hata nilijiona kama mchangiaji wa kanisa, bila aibu nikifanya madai kwa Mungu na kuringia ukubwa wangu. Kwa kweli nilikuwa muhali mno, nimepungukiwa mno katika maarifa ya kawaida! Tabia hii yangu ilikuwa ya kuchukiza mno na ya karaha kwa Mungu! Kanisa ni tofauti kwa jamii na ulimwengu kwa kuwa tabia ya haki ya Mungu haina huruma kwa mtu yeyote. Haijalishi ni kiasi kipi umestahili, ni kuteseka kiasi gani umestahimili, au ni kwa muda gani umemfuata Yeye. Ukiikosea tabia ya Mungu, yote yatakayokushukia ni ghadhabu na uadhama wa Mungu. Je, kimelea kama mimi ambaye hakufanya kazi yake halisi na aliishi tu kwa kulitegemea kanisaangewezaje kuwa jambo la pekee mbele ya Mungu mwenye haki? Ni hapo tu nilipogundua kwamba kufukuzwa kwangu na kunifanya nitafakari kujihusu ilikuwa kabisa ni haki ya hukumu ya Mungu kwangu. Ilikuwa pia ni upendo mkubwa mno na wokovu ambao Mungu angeweza kumpa mtoto huyu Wake mwasi. Vinginevyo, bado ningekuwa nimeshikilia mtazamo usio sahihi wa "kuweza angalau kupata riziki katika kanisa bila kujali lolote kwa sababu ya kazi niliyoifanya, hata kama si yenye kustahili," kama nimelala katika ndoto nzuri niliyojisokotea mwenyewe, na hatimaye kuangamia katika mawazo yangu mwenyewe.
Ee Mungu! Asante! Wewe usifiwe! Hata kama njia yako ya kuokoa hailingani na dhana zangu, sasa ninaelewa nia Zako na kuona utunzaji na mawazo Yako. Niko tayari kukubali kuadibu Kwako na hukumu, na kwa njia hiyo nitafakari kujihusu na kujijua mwenyewe, kujua tabia Yako ya haki, na zaidi ya hayo kuwa tayari kutubu na kuanza upya ili kuwa mtu mpya!
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni