Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Unampenda Mungu kiasi gani hasa leo? Na unajua kiasi gani hasa kuhusu yote ambayo Mungu amefanya ndani yako? Haya ni mambo unayopaswa kujifunza. Mungu anapowasili duniani, yote ambayo Amefanya ndani ya mwanadamu na kumkubalia mwanadamu kuona ni ili mwanadamu atampenda na kumjua Yeye kweli. Kwamba mwanadamu anaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu na ameweza kufikia umbali huu ni, kuhusiana na jambo moja, kwa sababu ya upendo wa Mungu, na kuhusiana na jambo lingine,
ni kwa sababu ya wokovu wa Mungu; zaidi ya hayo, ni kwa sababu ya kazi ya hukumu na kuadibu ambayo Mungu ametekeleza ndani ya mwanadamu. Kama hamna hukumu, kuadibu, na majaribio ya Mungu, na kama Mungu hajawafanya mteseke, basi, kusema ukweli, ninyi hamumpendi Mungu kweli. Kadri kazi ya Mungu ilivyo kuu zaidi ndani ya mwanadamu, na kadri mateso ya mwanadamu yalivyo makuu zaidi, ndivyo inavyoweza kuonyesha zaidi hasa vile kazi ya Mungu ilivyo ya maana, na ndivyo moyo wa mwanadamu unavyoweza kumpenda Mungu kweli zaidi. Unajifunzaje jinsi ya kumpenda Mungu? Bila mateso makali na usafishaji, bila majaribio ya kuumiza—na kama, zaidi ya hayo, yote ambayo Mungu alimpa mwanadamu ingekuwa neema, upendo, na rehema—je, ungeweza kufikia upendo wa kweli kwa Mungu? Kwa upande mmoja, wakati wa majaribio ya Mungu mwanadamu huja kujua kasoro zake, na huona kwamba yeye ni mdogo, wa kudharauliwa, na duni, kwamba hana chochote, na si kitu; kwa upande mwingine, wakati wa majaribio Yake Mungu humuumbia mwanadamu mazingira tofauti yanayomfanya mwanadamu aweze zaidi kupitia kupendeza kwa Mungu. Ingawa maumivu ni makubwa, na wakati mwingine yasiyoshindika—na hata hufikia kiwango cha huzuni ya kuseta—baada ya kuyapitia, mwanadamu huona vile kazi ya Mungu ndani yake ni ya kupendeza, na ni juu ya msingi huu tu ndiyo ndani ya mwanadamu huzaliwa upendo wa kweli kwa Mungu. Leo mwanadamu huona kwamba na neema, upendo na rehema ya Mungu pekee, hana uwezo wa kujijua mwenyewe kweli, sembuse kuweza kujua kiini cha mwanadamu. Ni kupitia tu usafishaji na hukumu ya Mungu, ni wakati tu wa usafishaji kama huo ndiyo unaweza kujua kasoro zako, na kujua kwamba huna chochote. Hivyo, upendo wa mwanadamu kwa Mungu umejengwa juu ya msingi wa usafishaji na hukumu ya Mungu. Kama wewe hufurahia tu neema ya Mungu, na maisha ya familia yenye amani au baraka yakinifu, basi hujampata Mungu, na imani yako kwa Mungu haijafaulu. Mungu tayari ametekeleza hatua moja ya kazi ya neema katika mwili, na tayari amempa mwanadamu baraka yakinifu—lakini mwanadamu hawezi kufanywa mkamilifu na neema, upendo, na rehema pekee. Katika uzoefu wa mwanadamu yeye hukabiliwa na baadhi ya upendo wa Mungu, na huuona upendo na rehema ya Mungu, lakini baada ya kupitia kwa kipindi fulani cha wakati, yeye huona kwamba neema ya Mungu na upendo na rehema Yake hayawezi kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na hayana uwezo wa kufichua kile ambacho ni potovu ndani ya mwanadamu, wala hayawezi kumwondolea mwanadamu tabia yake potovu, au kufanya kuwa kamilifu upendo na imani yake. Kazi ya Mungu ya neema ilikuwa kazi ya kipindi kimoja, na mwanadamu hawezi kutegemea kufurahia neema ya Mungu ili kumjua Mungu.
Ni kupitia nini ndiyo ukamilishaji wa Mungu kwa mwanadamu hutimizwa? Kupitia tabia Yake yenye haki. Tabia ya Mungu hasa huwa na haki, ghadhabu, uadhama, hukumu, na laana, na ukamilishaji Wake wa mwanadamu hasa ni kupitia hukumu. Watu wengine hawaelewi, na huuliza ni kwa nini Mungu anaweza tu kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu kupitia hukumu na laana. Wao husema kwamba kama Mungu angemlaani mwanadamu, si mwanadamu angekufa? Kama Mungu angemhukumu mwanadamu, si mwanadamu angelaaniwa? Basi anawezaje hata hivyo kufanywa mkamilifu? Hayo ndiyo maneno ya watu wasioijua kazi ya Mungu. Kile ambacho Mungu hulaani ni uasi wa mwanadamu, na kile Anachohukumu ni dhambi za mwanadamu. Ingawa Yeye hunena kwa ukali, na bila kiwango cha hisi hata kidogo, Yeye hufichua yote yaliyo ndani ya mwanadamu, na kupitia maneno haya makali Yeye hufichua kile kilicho muhimu ndani ya mwanadamu, lakini kupitia hukumu kama hiyo, Yeye humpa mwanadamu ufahamu mkubwa wa kiini cha mwili, na hivyo mwanadamu hujitiisha chini ya utii mbele za Mungu. Mwili wa mwanadamu ni wa dhambi, na wa Shetani, ni wa kutotii, na chombo cha kuadibu kwa Mungu—na kwa hiyo, ili kumruhusu mwanadamu kujijua, maneno ya hukumu ya Mungu lazima yamfike na lazima kila aina ya usafishaji itumike; ni wakati huo tu ndiyo kazi ya Mungu inaweza kuwa ya kufaa.
Kutokana na maneno yaliyonenwa na Mungu inaweza kuonekana kwamba tayari Ameulaani mwili wa mwanadamu. Je, haya maneno, basi, ni maneno ya laana? Maneno yaliyonenwa na Mungu hufichua tabia halisi ya mwanadamu, na kupitia ufichuzi kama huo unahukumiwa, na unapoona kwamba huwezi kuyaridhisha mapenzi ya Mungu, ndani unahisi huzuni na majuto, unahisi kwamba unapaswa kumshukuru Mungu sana, na usiyetosha kwa ajili mapenzi ya Mungu. Kuna nyakati ambapo Roho wa Mungu hukufundisha nidhamu kutoka ndani, na nidhamu hii hutoka kwa hukumu ya Mungu; kuna nyakati ambapo Mungu hukushutumu na kuuficha uso Wake kutoka kwako, wakati ambapo hakusikilizi, na Hafanyi kazi ndani yako, akikuadibu bila sauti ili kukusafisha. Kazi ya Mungu ndani ya mwanadamu ni hasa ili kuweka wazi tabia Yake yenye haki. Ni ushuhuda gani ambao mwanadamu hatimaye huwa nao kwa Mungu? Yeye hushuhudia kwamba Mungu ni Mungu mwenye haki, kwamba tabia yake ni haki, ghadhabu, kuadibu, na hukumu; mwanadamu hushuhudia kwa tabia yenye haki ya Mungu. Mungu hutumia hukumu Yake kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, Amekuwa Akimpenda mwanadamu, na kumwokoa mwanadamu—lakini ni kiasi gani kiko ndani ya upendo Wake? Kuna hukumu, uadhama, ghadhabu, na laana. Ingawa Mungu alimlaani mwanadamu katika wakati uliopita, Hakumtupa mwanadamu kabisa ndani ya shimo la kuzimu, lakini Alitumia njia hiyo kuisafisha imani ya mwanadamu; Hakumuua mwanadamu, lakini alitenda ili kumfanya mwanadamu awe mkamilifu. Kiini cha mwili ni kile ambacho ni cha Shetani—Mungu alikisema sahihi kabisa—lakini ukweli unaotekelezwa na Mungu haukamilishwi kufuatana na maneno Yake. Yeye hukulaani ili uweze kumpenda, na ili uweze kujua kiini cha mwili; Yeye hukuadibu ili uweze kuamshwa, kukuruhusu wewe ujue kasoro zilizo ndani yako, na kujua kutostahili kabisa kwa mwanadamu. Hivyo, laana za Mungu, hukumu Yake, na uadhama na ghadhabu Yake—yote ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu awe mkamilifu. Yote ambayo Mungu anafanya leo, na tabia yenye haki ambayo Yeye huifanya kuwa wazi ndani yenu—yote ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na huo ndio upendo wa Mungu.
Katika dhana za mwanadamu za kitamaduni, upendo wa Mungu ni neema Yake, fadhili, na huruma kwa udhaifu wa mwanadamu. Ingawa mambo haya pia ni upendo wa Mungu, yanaegemea upande mmoja sana, na si njia za msingi ambazo kwazo Mungu humfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Wakati ambapo watu wengine wameanza tu kumwamini Mungu, ni kwa sababu ya ugonjwa. Ugonjwa huu ni neema ya Mungu kwako; bila huo, hungemwamini Mungu, na kama hungemwamini Mungu basi hungefika umbali huu—na hivyo hata neema hii ni upendo wa Mungu. Katika wakati wa kumwamini Yesu, watu walifanya mengi ambayo hayakupendwa na Mungu kwa sababu hawakuelewa ukweli, lakini Mungu ana upendo na rehema, na Amemleta mwanadamu umbali huu, na ingawa mwanadamu haelewi chochote, bado Mungu humruhusu mwanadamu amfuate Yeye, na, zaidi ya hayo, Amemwongoza mwanadamu mpaka leo. Je, huu si upendo wa Mungu? Kile ambacho kinadhihirishwa katika tabia ya Mungu ni upendo wa Mungu—hili ni sahihi bila shaka. Wakati ambapo ujenzi wa kanisa ulifikia kilele chake, Mungu alifanya hatua ya kazi ya watendaji-huduma na akamtupa mwanadamu katika shimo la kuzimu. Maneno ya wakati wa watendaji-huduma yote yalikuwa laana: laana za mwili wako, laana za tabia yako potovu ya kishetani, na laana za mambo yanayokuhusu ambayo hayatimizi mapenzi ya Mungu. Kazi iliyofanywa na Mungu katika hatua hiyo ilidhihirishwa kama uadhama, karibukaribu sana baadaye Mungu alitekeleza hatua ya kazi ya kuadibu, na kisha kukaja majaribio ya kifo. Katika kazi kama hiyo, mwanadamu aliona ghadhabu, uadhama, hukumu, na kuadibu kwa Mungu, lakini aliona pia neema ya Mungu, na upendo na rehema Yake; yote aliyofanya Mungu, na yote yaliyodhihirishwa kama tabia Yake, ulikuwa upendo wa mwanadamu, na yote ambayo Mungu alifanya yaliweza kutimiza mahitaji ya mwanadamu. Aliyafanya ili kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na kutoa kwa kadri ya kimo cha mwanadamu. Kama Mungu hangefanya hili, mwanadamu hangekuwa na uwezo wa kuja mbele za Mungu, na hangekuwa na njia ya kuujua uso wa kweli wa Mungu. Tangu wakati ambapo mwanadamu alianza kwa mara ya kwanza kumwamini Mungu mpaka leo, Mungu amemkimu mwanadamu polepole kwa mujibu wa kimo chake, ili kwamba, ndani, mwanadamu amekuja kumjua Yeye polepole. Ni kwa kuweza kufika leo tu ndiyo mwanadamu ametambua hasa vile hukumu ya Mungu ni ya ajabu. Hatua ya kazi ya watendaji-huduma ilikuwa tokeo la kwanza la kazi ya laana tangu wakati wa uumbaji mpaka leo. Mwanadamu alilaaniwa kwenda katika shimo la kuzimu. Kama Mungu hangefanya hivyo, leo mwanadamu hangekuwa na ufahamu wa kweli wa Mungu; ni kupitia tu laana ya Mungu ndiyo mwanadamu hukutana kwa urasimu na tabia ya Mungu. Matukio hayo yalimwonyesha mwanadamu kwamba uaminifu wake haukukubalika, kwamba kimo chake kilikuwa kidogo sana, kwamba hakuwa na uwezo wa kuridhisha mapenzi ya Mungu, na kwamba madai yake ya kumridhisha Mungu wakati wote yalikuwa maneno matupu tu. Ingawa katika hatua ya kazi ya watendaji-huduma Mungu alimlaani mwanadamu, ikitazamwa kutoka leo hatua hiyo ya kazi ilikuwa ya ajabu: Ilileta mgeuzo mkubwa kwa mwanadamu, na kusababisha mabadiliko makuu katika tabia yake ya maisha. Kabla ya wakati wa watendaji-huduma, mwanadamu hakuelewa chochote kuhusu ukimbizaji wa maisha, ni nini maana ya kumwamini Mungu, au hekima ya kazi ya Mungu, wala hakufahamu kwamba kazi ya Mungu inaweza kumjaribu mwanadamu. Tangu wakati wa watendaji-huduma mpaka leo, mwanadamu huona vile kazi ya Mungu ni ya ajabu, haiwezi kueleweka kwa mwanadamu, na akitumia akili yake hawezi kufikiria jinsi Mungu hufanya kazi, na pia huona vile kimo chake ni kidogo na kwamba kiasi kikubwa chake ni cha kutotii. Mungu alipomlaani mwanadamu, ilikuwa ili Atimize athari, na Hakumuua mwanadamu. Ingawa Alimlaani mwanadamu, Alifanya hivyo kupitia maneno, na laana Zake hazikumwangukia mwanadamu kwa kweli, kwani kile ambacho Mungu alilaani kilikuwa kutotii kwa mwanadamu, na kwa hiyo maneno ya laana Zake pia yalikuwa kwa ajili ya kumfanya mwanadamu awe mkamilifu. Kama Mungu atamhukumu mwanadamu au kumlaani, yote mawili humfanya mwanadamu kuwa mkamilifu: Yote mawili ni kwa ajili ya kukifanya kamili kile ambacho ni kichafu ndani ya mwanadamu. Kupitia njia hii mwanadamu alisafishwa, na kile ambacho kilikuwa kinakosekana ndani ya mwanadamu kilifanywa kamilifu kupitia maneno na kazi Yake. Kila hatua ya kazi ya Mungu—kama ni maneno makali, au hukumu, au kuadibu—humfanya mwanadamu kuwa mkamilifu, na inafaa kwa uhalisi. Kotekote katika enzi zote Mungu hajawahi kufanya kazi kama hii; leo, Yeye hufanya kazi ndani yenu ili muweze kufahamu hekima Yake. Ingawa mmepitia maumivu fulani ndani yenu, mioyo yenu inajisikia thabiti, na kwa amani; ni baraka yenu kuweza kufurahia hatua hii ya kazi ya Mungu. Haijalishi kile mnachoweza kupata katika siku za baadaye, yote mnayoona kuhusu kazi ya Mungu ndani yenu leo ni upendo. Kama mwanadamu hapitii hukumu na kuadibu kwa Mungu, matendo yake na ari daima yatakuwa nje, na tabia yake daima itaendelea kutobadilika. Je, hii inahesabika kama kupatwa na Mungu? Leo, ingawa bado kuna mengi ndani ya mwanadamu ambayo ni yenye kiburi na yenye majivuno, tabia ya mwanadamu ni imara zaidi kuliko awali. Mungu kukushughulikia wewe ni ili kukuokoa, na ingawa unaweza kuhisi maumivu kidogo wakati huo, siku itafika ambapo kutatokea mabadiliko katika tabia yako. Wakati huo, utakumbuka ya nyuma na kuona vile kazi ya Mungu ni ya hekima, na huo utakuwa wakati ambao utaweza kufahamu kwa kweli mapenzi ya Mungu. Leo, kuna watu wengine ambao husema kwamba wanafahamu mapenzi ya Mungu—lakini hiyo si ya kweli kamwe, wao wanazungumza upuuzi, kwa sababu wakati huu bado hawajafahamu kama mapenzi ya Mungu ni kumwokoa mwanadamu au kumlaani mwanadamu. Labda huwezi kuliona kwa dhahiri sasa, lakini siku itafika ambapo utaona kwamba siku ya kutukuzwa kwa Mungu imefika, na uone jinsi ni ya maana kumpenda Mungu, ili utakuja kuyajua maisha ya binadamu, na mwili wako utaishi katika ulimwengu wa kumpenda Mungu, kwamba roho yako itawekwa huru, maisha yako yatajaa furaha, na kwamba daima utakuwa karibu na Mungu, na utamtegemea Mungu daima. Wakati huo, utajua kweli jinsi kazi ya Mungu ni ya thamani leo.
Leo, watu wengi sana hawana ufahamu huo. Wao huamini kwamba mateso hayana thamani, wao hukanwa na ulimwengu, maisha yao ya nyumbani yamesumbuliwa, wao si wapendwa wa Mungu, na matazamio yao ni matupu. Kuteseka kwa watu wengine hufikia kiwango fulani, na fikira zao hugeukia kifo. Huu si upendo wa kweli kwa Mungu; watu kama hao ni waoga, hawana ustahamilivu, wao ni wadhaifu na wasio na nguvu! Mungu ana hamu ya mwanadamu kumpenda Yeye, lakini kadri mwanadamu anavyompenda Yeye, ndivyo kuteseka kwa mwanadamu huwa kwingi zaidi, na kadri mwanadamu anavyompenda Yeye, ndivyo majaribio ya mwanadamu huwa makubwa zaidi. Ikiwa unampenda Yeye, basi kila aina ya mateso yatakufika—na ikiwa humpendi, basi labda kila kitu kitaendelea kwa urahisi kwako, na kila kitu kinachokuzunguka kitakuwa kitulivu kwako. Unapompenda Mungu, utahisi kwamba mengi kandokando yako hayawezi kushindikana, na kwa sababu kimo chako ni kidogo sana utasafishwa; aidha, huwezi kumridhisha Mungu, na daima utahisi kwamba mapenzi ya Mungu ni ya juu sana, kwamba hayawezi kufikiwa na mwanadamu. Kwa sababu ya haya yote utasafishwa—kwa sababu kuna udhaifu mwingi ndani yako, na mengi yasiyoweza kuridhisha mapenzi ya Mungu, utasafishwa ndani. Lakini lazima muone kwa dhahiri kwamba utakaso hutimizwa tu kupitia usafishaji. Hivyo, katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana. Unapojaribiwa, unapaswa kusema: “Moyo wangu ni wa Mungu, ndivyo Mungu hukubariki zaidi, na ndivyo nguvu za upendo wako kwa Mungu huwa kuu zaidi; kwa hiyo, vilevile, utakuwa na imani na azimio, na utahisi kwamba hakuna kilicho na thamani zaidi au cha maana kuliko kutumia maisha ukimpenda Mungu. Inaweza kusemwa kwamba mwanadamu anatakiwa tu kumpenda Mungu ili kuishi bila huzuni. Ingawa kuna nyakati ambazo mwili wako ni dhaifu na unazongwa na matatizo mengi ya kweli, katika nyakati hizi utamtegemea Mungu kweli, na ndani ya roho yako utafarijiwa, na utahisi hakika, na kwamba una kitu cha kutegemea. Kwa njia hii, utaweza kushinda hali nyingi, na kwa hiyo hutalalamika kuhusu Mungu kwa sababu ya uchungu unaopitia; utataka kuimba, kucheza, na kuomba, kukusanyika na kuwasiliana kwa karibu, kumfikiria Mungu, na utahisi kwamba watu wote, mambo, na vitu vilivyo kandokando yako ambavyo vimepangwa na Mungu vinafaa. Kama humpendi Mungu, yote ambayo unategemea yatakuwa yenye kero kwako, hakuna kitakachokuwa cha kufurahisha machoni mwako; ndani ya roho yako hutakuwa huru bali wa kudhulumiwa, moyo wako daima utalalamika kuhusu Mungu, na daima utahisi kwamba unapitia mateso mengi sana, na kwamba ni udhalimu sana. Kama hufuatilii kwa ajili ya furaha, bali ili umridhishe Mungu na kutoshtakiwa na Shetani, basi ukimbizaji kama huo utakupa nguvu nyingi za kumpenda Mungu. Mwanadamu anaweza kutekeleza yote yanayonenwa na Mungu, na yote ayafanyayo yanaweza kumridhisha Mungu—hii ndiyo maana ya kuwa na hakika. Kufuatilia ridhaa ya Mungu ni kuutumia upendo wa Mungu kutia maneno Yake katika vitendo; pasipo kutia maanani wakati—hata kama wengine hawana nguvu—ndani yako bado kuna moyo unaompenda Mungu, ambao unamtamani Mungu sana, na humkosa Mungu. Hiki ni kimo halisi. Jinsi ambavyo kimo chako ni kikubwa hasa hutegemea jinsi upendo wako kwa Mungu ulivyo mkuu, kama unaweza kusimama imara wakati unajaribiwa, kama wewe ni mdhaifu hali fulani inapokujia, na kama unaweza kusimama imara wakati ambapo ndugu zako wanakukataa; majilio ya ukweli yataonyesha hasa upendo wako kwa Mungu ukoje. Inaweza kuonekana kutoka kwa kazi nyingi ya Mungu kwamba Mungu kweli anampenda mwanadamu, ni hasa tu macho ya roho ya mwanadamu bado hayajafunguliwa kabisa, na hawezi kufahamu kazi nyingi ya Mungu, na mapenzi ya Mungu, na vitu vingi ambavyo ni vya kupendeza kuhusu Mungu; mwanadamu ana upendo kidogo sana wa kweli kwa Mungu. Umemwamini Mungu kotokote katika wakati huu wote, na leo Mungu amezuia njia zote za kutoroka. Kusema kwa kweli, huna chaguo lingine ila kuifuata njia sahihi, njia sahihi ambayo umeelekezwa kwayo kwa hukumu kali na wokovu mkubwa kabisa wa Mungu. Ni baada tu ya kupitia taabu na usafishaji ndiyo mwanadamu hujua kwamba Mungu ni wa kupendeza. Baada ya kupitia mpaka leo, inaweza kusemwa kwamba mwanadamu amekuja kujua sehemu ya kupendeza kwa Mungu—lakini hili bado halitoshi, kwa sababu mwanadamu amepungukiwa sana. Lazima apate uzoefu zaidi wa kazi ya Mungu ya ajabu, na zaidi ya usafishaji wote wa mateso uliowekwa na Mungu. Ni wakati huo tu ndiyo tabia ya maisha ya mwanadamu itaweza kubadilishwa.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni