Kanisa la Mwenyezi Mungu | 49. Uso halisi wa Mtu Anayedaiwa Kuwa Mtu Mzuri
Kemu Jiji la Zhumadian, Mkoa wa Henan
Katika mawazo yangu mwenyewe, daima nimejifikiria kuwa na ubinadamu mzuri. Nimefikiria hivi kwa sababu, majirani zangu mara nyingi walinisifu mbele ya wazazi wangu kwa kuwa mwenye busara na wa kuijali familia yetu; wakisema kuwa mimi nilikuwa kipenzi cha wazazi wangu. Baada ya kuolewa, wakwe zangu walinishukuru mbele ya majirani kwa kuwa wema na mtoto wao. Katika kitengo changu, kiongozi wangu alinisifu kwa kuwa mwaminifu na mwenye ustadi. Na tangu nikubali hatua hii ya kazi ya Mungu, nimekuwa mtii kwa chochote kanisa huniomba kufanya. Huwa sipingani kamwe na kiongozi hata nikikemewa na kiongozi huyu kwa kutofanya kazi nzuri, na mara nyingi mimi huwasaidia ndugu wa kiume na wa kike walio na mahitaji.
Kwa hivyo, ninaamini kuwa mimi ni wa maana, mwenye huruma, na mtu mwema mwenye ubinadamu. Sijawahi kujifikiria mwenyewe kwa njia ya maneno ambamo Mungu hufichua kuwa mwanadamu hana ubinadamu au kwamba mtu ana ubinadamu dhaifu. Wakati wa kuwasiliana maneno ya Mungu na ndugu wa kiume na wa kike, ingawa najua nahitaji kuwa na ufahamu wa asili yangu mwenyewe, bado mimi hudumisha mtazamo wangu mwenyewe, nikifikiria moyoni mwangu: Hata kama mimi si mtu wa ubinadamu mzuri, bado nina ubinadamu bora kiasi ukilinganisha na wengine. Aidha, bila kujali neno la Mungu linavyosema au kile ndugu wa kiume na wa kike wanavyosema, siko tayari kujitenga na wazo la kuwa mtu wa ubinadamu mzuri.
Siku moja, nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, kifungu kimoja kilivuta nadhari yangu. Mungu anasema, “Watu wengine ni wazuri kiasili; wana uwezo wa kutenda ukweli. Ubinadamu wa watu wengine ni mnyonge, hivyo ni vigumu kwao kutenda ukweli…. Je, mnaweza kusema kuwa yule ambaye hatendi ukweli amewahi kuutafuta ukweli? Hajautafuta kabisa! Fikira zake binafsi hutokea: 'Njia hii ni nzuri, ni kwa faida yangu.' Mwishowe, bado anatenda kulingana na mawazo yake binafsi. Hatafuti ukweli kwa sababu kuna kitu kisicho sawa na moyo wake, moyo wake hauko sawa. Hatafuti, hachunguzi, wala haombi mbele za Mungu; anatenda tu kwa ukaidi kulingana na matakwa yake. Mtu wa aina hii hana upendo wa ukweli kabisa. … Wale wasio na upendo kwa ukweli hawatautafuta katika wakati huo, wala hawatajichunguza baadaye. Kamwe hawachunguzi kama tendo lilitekelezwa kwa sawa ama kwa makosa hatimaye, hivyo wanakiuka kanuni kila wakati, wanakiuka ukweli. … Mtu aliye na moyo anaweza kufanya makosa mara moja tu anapofuata utendaji, mara mbili kwa kiwango cha juu zaidi—mara moja ama mbili, sio mara tatu ama nne, hii ni akili ya kawaida. Kama anaweza kutenda makosa hayo sawa mara tatu ama nne, hii inathibitisha kuwa hana upendo wa ukweli, wala hautafuti ukweli. Mtu wa aina hii kwa waziwazi sio mtu mwenye utu” (“Kutatua Asili na Kutenda Ukweli” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Baada ya kusoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu, nilikuwa na ufunuo wa ghafla. Inavyoelekea, ubinadamu mzuri au mbaya unahusiana kwa karibu na utekelezaji wa ukweli. Mtu wa ubinadamu mzuri atatafuta ukweli na kutenda ukweli katika kila kitu, na kujichunguza mwenyewe baadaye. Nimemejiona daima kuwa na ubinadamu mzuri, hivyo mimi ni mtu ambaye hutafuta na kutenda ukweli katika kila kitu? Nikifikiria nyuma, sikuomba au kutafuta ukweli kuhusu vitu vingi vilivyonikabili. Sikujichunguza au kujifahamu baadaye. Ingawa nilikuwa nimeonyesha tabia yangu potovu, sikutatua masuala yangu kwa kutafuta ukweli, lakini niliendelea kufanya kosa hilo hilo tena na tena. Wakati mwingine hata kama nilielewa kipengele kimoja cha ukweli, sikuonekana kutaka kukitenda. Nakumbuka mifano mingi ya jambo hili kwa dhahiri. Wakati mmoja, nakumbuka nikihisi hisi ya utengano na mtu niliyeshirikishwa naye. Nilikuwa na ufahamivu kuwa lingeathiri moja kwa moja matokeo yatakikanayo ya kazi ikiwa tatizo halikutatuliwa, lakini kwa sababu ya kiburi na majivuno yangu, nilikataa kuacha ubinafsi wangu na kuwa na mawasiliano ya wazi naye. Badala yake, nilistahimili jambo chungu lakini lisiloepukika na kuendelea kufanya kazi, na kusababisha kazi isiyofanikiwa sana. Wakati mwingine nilipoona ndugu wa kiume na wa kike wakifichua kipengele fulani cha hali yao potovu, sikujaribu kuwasiliana nao katika ukweli ili kuwasaidia kujijua, lakini badala yake niliwahukumu bila wao kujua. Sikutubu au kujaribu kubadilisha njia zangu hata baada ya kushughulikiwa mara chache, lakini badala yake niliendelea katika njia zangu za zamani. Sikujitahidi kupata matokeo mazuri mno katika kufanya kazi yangu, lakini daima nilikuwa mvivu na mjanja, nikishughulika na mambo kihobelahobela, daima nikimdanganya Mungu ili kudumisha nafasi yangu mwenyewe, bahati na hadhi. Sikuyapa umuhimu au kuwa na hisia ya hatia. Sikutafuta au kuchunguza mambo yalipotokea kazini mwangu, lakini nilifanya tu kama nilivyotaka. Hata kama ilileta hasara kubwa kwa kanisa, sikuhisi kama nilikuwa na deni kwa Mungu, wala sikuaibishwa na matendo yangu maovu. Hata kama Mungu alinikumbusha kupitia maneno Yake na kufichua upotovu wangu kwa njia ya kunishughulikia na kunipogoa, niliendelea kumpuuza Yeye, na kufanya makosa yale yale zaidi ya mara tatu au nne. Si vitendo hivi vinathibitisha kwamba nina ukosefu wa ubinadamu na mimi si mpenzi wa ukweli machoni pa Mungu? Bila kujali, sijajaribu kujijua kwa msingi wa asili yangu, lakini naendelea kuvaa laurusi ya "ubinadamu mzuri" juu ya kichwa changu. Nimekuwa mtovu wa haya jinsi gani!
Hivi sasa, moyo wangu umejaa hatia, na wakati huo huo umejaa shukrani kwa Mungu. Siwezi kujizuia kujimwaga mbele ya Mungu, "Mungu, asante kwa nuru Yako, kuniruhusu nijue kuwa mimi si mtu mwenye ubinadamu mzuri, kunisaidia kuelewa kuwa mtu mwenye ubinadamu wa kweli ni yule anayependa ukweli, ni mtu ambaye humsikiliza Mungu na kumtii Mungu, ni mtu ambaye yuko tayari kutenda ukweli na kufuatilia upendo wa Mungu. Mimi pia natambua ufahamu wangu juu yangu hautegemezwi kwa ukweli wa maneno ya Mungu, lakini umetegemezwa fikra zangu na dhana zangu, na vilevile maoni yangu ya kidunia. Ni upumbavu kabisa. Mungu, tangu sasa kuendelea, sitaki kujipima kulingana na mtazamo wa Shetani au mawazo yangu mwenyewe. Ninataka kujijua kwa msingi wa maneno Yako, na kufanya kila linalowezekana kufuatilia ukweli, ili hivi punde niweze kuwa mtu aliye na ukweli na ubinadamu ili kuufariji moyo Wako."
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni