Sura ya 54. Watu Ambao Daima Wana Mahitaji kwa Mungu Ndio wa Mwisho Kuwa Tayari Kusikia Hoja
Mwenyezi Mungu alisema, Kama utajielewa, ni lazima uielewe hali yako ya kweli; jambo muhimu zaidi katika kuielewa hali yako mwenyewe ni kuwa na ufahamu juu ya fikira zako na mawazo yako. Katika kila kipindi cha muda, fikira za watu zimekuwa zikidhibitiwa na jambo moja kubwa; ikiwa unaweza kuzielewa fikira zako, unaweza kukielewa kitu kilicho nyuma yazo.
Hakuna mtu anayeweza kuzidhibiti fikira na mawazo yake. Je, fikira na mawazo haya hutoka wapi? Je, ni nini kiini cha matilaba haya? Je, fikira hizi na mawazo haya huzalishwaje? Je, zinadhibitiwa na nini? Asili za fikira na mawazo haya ni nini? Baada ya tabia yako kubadilika, fikira na mawazo yako, tamaa ambazo moyo wako unatafuta na maoni yako kwa ukimbizaji, ambazo zimefanyizwa kutokana na sehemu ambazo zimebadilika zitakuwa tofauti. Hizo fikira na mawazo zinazotokana na vitu ambavyo hujabadilisha, vitu ambavyo wewe huvielewi kwa dhahiri, na vitu ambavyo hujabadilisha na uzoefu wa ukweli ni vichafu, vyenye taka na visivyovutia. Watu siku hizi ambao wamepitia kazi ya Mungu kwa miaka kadhaa wana hisia na ufahamu kiasi wa mambo haya. Watu ambao wamepitia kazi ya Mungu kwa kipindi cha muda mfupi bado hawaelewi mambo haya; bado hayako dhahiri. Bado hawajui udhaifu wao uliko na ni sehemu gani ambazo ni rahisi kwao kuanguka! Hamjui kwa sasa nyinyi ni mtu wa aina gani, na watu wengine wanaweza kuona kwa kiasi fulani nyinyi ni aina gani ya watu, ambapo hamuwezi kuhisi. Hamuwezi kwa dhahiri kutofautisha fikira zenu za kawaida au nia, na hamuelewi kwa dhahiri ni nini asili ya mambo haya. Jinsi unavyokielewa kipengele kwa kina, ndivyo utakavyozidi kubadilika katika kipengele hicho; kisha mambo unayoyafanya yatakuwa kwa mujibu wa ukweli, utakuwa na uwezo wa kuyatimiza mahitaji ya Mungu, na utakuwa karibu na mapenzi ya Mungu. Ni kwa kutafuta kwa njia hii tu ndipo utaweza kupata matokeo. Watu wengi wanaamini katika Mungu, lakini wao hawazingatii kubadilisha tabia ya maisha yao; badala yake, wao huzingatia mtazamo wa Mungu kwao na ikiwa wanayo nafasi katika moyo wa Mungu. Wao daima hukisia wao ni aina gani ya mtu katika macho ya Mungu na kama wana hadhi katika moyo wa Mungu au la. Watu wengi wako namna hii, na wakimwona Mungu, watakuwa wakiangalia daima kuona kama Mungu anazungumza kwa furaha au kwa hasira kwao. Pia kunao baadhi ya watu ambao siku zote huwauliza wengine: "Je, Mungu Ametaja matatizo yangu? Mtazamo wa Mungu kwangu ni upi? Je, Yeye hunijali? "Kuna watu ambao ni wa kustaajabisha hata zaidi ambao huonekana kugundua matatizo mapya: "Aa, Mungu ameniangalia vibaya, sijui ni kipi nilichokifanya vibaya" Watu huyapa mambo haya uangalifu maalum. Baadhi ya watu husema: "Tunaamini katika Mungu ambaye alichukua mwili; ikiwa Yeye hatatujali, si tumekwisha?" Maana ya msingi ya hili ni: Tunaamini kwa nini kama hatuna hadhi katika moyo wa Mungu? Basi hatutaamini! Si huu ni muhali? Je, unajua ni kwa nini watu wanapaswa kumwamini Mungu? Watu ni siku zote hutafuta nafasi katika moyo wa Mungu kukaa na kamwe hawatafakari kama Mungu ana nafasi ndani ya mioyo yao au la ama jinsi wao humtendea Mungu. Watu ni wenye kiburi na majivuno sana! Hapa ndipo watu huwa muhali zaidi. Hata kuna baadhi ya watu ambao hukosa mantiki kiasi kwamba wanapomsikia Mungu akiuliza juu ya watu wengine, bila kuuliza juu yao au kuyataja majina yao, ama wakati Mungu anawajali watu wengine na hawajali wao, au Anawafikiria watu wengine lakini Hawafikirii wao, hawaridhiki nao husema: "Siwezi kuamini tena; aina hii ya Mungu ni dhalimu na si wa haki au hayuko tayari kusikia hoja." Wao huanza kulalamika, ambalo ndilo suala na mantiki ya watu; wao ni wazimu. Wao mara nyingi husema: Mimi nitaitii mipango ya Mungu, kuitii mipangilio ya Mungu. Bila kujali jinsi gani Mungu hunitendea, sitawahi kulalamika kamwe; Mungu anaweza kunishughulikia, Anipogoe na kunihukumu. Lakini mambo yanapowajia kwa kweli, hawawezi kufaulu. Je, watu huwaza kwa njia hii? Watu hasa hujiheshimu, na wao hufikiri kuwa ni muhimu kwa namna ya pekee. Usijali kupogoa na kushughulika, ikiwa mtazamo mmoja hauonekani sawa, halafu wanahisi kuwa hakuna tumaini. "Nimekwisha! Sitaamini tena! Mungu haniangalii, sina matumaini." Ama ni sauti ambayo ni kali kiasi inaiyochoma mioyo yao na wanapoteza matumaini na kukatishwa tamaa tena, "Mungu alisema nami wakati huu na toni ya sauti ambayo haikuwa nzuri! Kuna maneno ndani ya maneno hayo, kuna miiba ndani ya maneno hayo, na maneno hayo yanabeba maana zingine. Nahisi kama hakuna umuhimu kwa imani yangu katika Mungu, Mungu haniangalii, kwa hiyo ni vigumu kwangu kumwamini tena. "Katika siku za nyuma baadhi ya watu wamefikiri: "Unaona jinsi ambavyo wengine wamekuwa yakini sana kuhusu Mungu na jinsi wanavyomuona kuwa muhimu sana. Kama mtazamo mmoja kutoka kwa Mungu haukuwa wa kawaida, wao wangechunguza kile Mungu alichomaanisha na hili. Wao ni waaminifu kwa Mungu kwa njia isiyo ya kawaida na humuona Yeye akiwa wa maana ya kipekee; Hii kwa kweli ni kumchukua Mungu aliye duniani kama Mungu aliye mbinguni. Wao huona mtazamo kutoka kwa Mungu kama muhimu kwa njia isiyo ya kawaida. "Je, ni hivyo? Baadhi ya watu wamechanganyikiwa sana; hawaoni chochote kwa dhahiri. Kimo cha watu ni kidogo sana, kwa kweli ni maonyesho ya kutahayarisha. Mantiki ya watu ina dosari sana, na wana mahitaji mengi mno kwa Mungu, ambayo ni mengi kupita kiasi; hawana mantiki. Watu daima wamekuwa wakimtaka Mungu kufanya mambo kwa njia hii na kwa njia ile. Wameshindwa kabisa kumtii Mungu au kumwabudu. Badala yake, wao huja na maombi yao yasiyo na busara kulingana na matamanio yao wenyewe; wao humwomba Mungu awe na uvumilivu mwingi, asiwe na hasira juu ya chochote, daima kuwaangalia kwa tabasamu kwenye uso Wake, na Yeye anapowaona, lazima awaruzuku na kuwasiliana nao. Bila kujali wakati, Mungu lazima azungumze daima, daima Aizuie hasira Yake, na kuonyesha maneno mazuri kwao. Watu wana mahitaji mengi mno na husumbuka na mambo mengi sana. Mnapaswa kutafakari juu ya mambo haya. Je, si mantiki ya binadamu ina dosari sana? Siyo tu kwamba wameshindwa kuitii kabisa mipango na mipangilio ya Mungu au kukubali kila kitu kutoka kwa Mungu, lakini kinyume chake wao hulazimisha mahitaji mengine ya ziada kwa Mungu. Watu wanawezaje kuwa waaminifu kwa Mungu ikiwa wana mahitaji ya aina hii? Wanawezaje kuitii mipango ya Mungu? Ikiwa watu wana aina hizi za mahitaji, basi wanawezaje kumpenda Mungu? Watu wote wana mahitaji ya jinsi Mungu anastahili kuwapenda, kuwavumilia, kuwaangalia na kuwalinda, na kuwatunza, lakini hawana mahitaji ya wao wenyewe ya jinsi ya kumpenda Mungu, jinsi ya kumfikiria Mungu, jinsi ya kumwangalia Mungu, jinsi ya kumridhisha Mungu, jinsi ya kuwa na Mungu mioyoni mwao, na jinsi ya kumwabudu Mungu. Je, vitu hivi vimo katika mioyo ya watu? Hivi ni vitu ambavyo watu wanapaswa kufanya, hivyo kwa nini watu hawasongi mbele kwa bidii katika vitu hivi? Watu wengine wana shauku kwa muda, lakini si ya kudumu; wakikumbana na kipingamizi kidogo, kinaweza kuwasababisha wakose tumaini na kulalamika. Watu wana shida nyingi zaidi na kuna watu wachache sana ambao huutafuta ukweli na hutaka kumpenda na kumridhisha Mungu. Watu hasa ni muhali na hawasimami kwa usahihi katika nafasi zao. Aidha, wao hujiona kuwa muhimu kwa namna ya pekee. Baadhi ya watu husema: "Mungu hutuona kama mboni ya jicho Lake, Yeye hakusita kumruhusu Mwana Wake wa pekee kusulubiwa ili kuwakomboa wanadamu; sisi ni wa thamani sana, Mungu alilipa gharama kubwa kuturejesha; sote tuna nafasi katika moyo wa Mungu, moyo Wake ni mkubwa sana. Watoto Wake wengi na watu wanayo nafasi moyoni Mwake, na sisi sio watu sahili. " Watu hujiheshimu sana na kujiona kuwa wakubwa sana. Kwa kweli, awali kulikuwa na baadhi ya viongozi wa jinsi hii ambao, baada ya wao kupandishwa vyeo na kuwa na hadhi, waliwaza: "Mungu hunipendelea na ameniruhusu kuwa kiongozi. Nitashughulika kwa bidii na kufanya kazi kwa ajili ya Mungu na Mungu amenijali ." Walikuwa wameridhika vya kushangaza, na kwa sababu hiyo, kwa muda mfupi, tabia zao halisi zilibainika walipofanya mambo mabaya kiasi. Walirudishwa nyumbani, na waliinamisha vichwa vyao kwa aibu na kusema, "Aa, Mungu ameniondoa, Mimi nimekwisha, heri niharakishe na kurudi nyumbani." Kama maonyesho yao mabaya yalifichuliwa na kushughulikiwa, walikuwa hasi hata zaidi, na hawangeamini tena. Hatimaye, walitafakari: "Mimi niko karibu na nani katika dunia hii? Mbali na mama na baba yangu, hakuna mtu aliye karibu nami. Hakuna Anachofanya Mungu kinachokaribia matarajio yangu, Hana moyo wa kupendana au hisia. Inasemekana kuwa Mungu huyahisi maono ya watu, hivyo kwa nini nimeondolewa baada ya kufanya kosa dogo jinsi hii? "Matokeo yake, wakawa wamevunjika moyo na hawakutaka kuamini. Watu huwa hawahitaji mengi kutoka kwao wenyewe, lakini huhitaji mengi kutoka kwa wengine. Wanapaswa kuwa na subira na uvumilivu kwao, wawatunze, wawaruzuku, wawatabasamie, wawe na maridhia kwao, na wajitoe kwao. Wanapaswa kuwatunza kwa njia nyingi, na hawawezi kuwa wakali kwao, kuwachochea, au kufanya chochote ambacho hawangetaka. Mantiki ya mtu ina upungufu sana! Watu hawako wazi juu ya wanakopaswa kusimama, wanachopaswa kufanya, kile wanachopaswa kukamilisha, ni maoni gani wanayopaswa kuwa nayo, ni nafasi gani wanapaswa kusimamia ili kumhudumia Mungu, na ni mahali gani wanafaa kuwa ili kujiweka ndani. Watu wenye nafasi ndogo hujipenda sana, na watu wasiokuwa na nafasi pia hujipenda kweli. Watu huwa hawajielewi kamwe. Kama mnaweza kuendelea na imani yenu, kutolalamika kamwe, na kutimiza wajibu wako kama kawaida bila kujali ni nini kinachosemwa kwako, jinsi unavyotendewa kwa ukali kwa ukali na jinsi unavyopuuzwa, basi utakuwa mtu mwenye kukomaa na wenye uzoefu, Na kwa kweli utakuwa na hadhi fulani na mantiki ya kawaida. Hutahitaji vitu vya Mungu, hutakuwa na tamaa za ubadhirifu, na hutaomba vitu vya watu wengine au vya Mungu kwa msingi wa vitu unavyovipenda. Hii inaonyesha kuwa unamiliki mfano wa mtu kwa kiwango fulani. Kwa sasa mna mahitaji mengi mno na ni mengi kupita kiasi. Nia zako nyingi zinathibitisha kwamba wewe hujasimama katika nafasi ya sawa, nafasi yako iko juu mno, na umejiona kama mheshimiwa kuzidi kiasi kana kwamba wewe huko chini zaidi ya Mungu. Kwa hiyo wewe ni mgumu wa kushughulikiwa, na hii ni asili ya Shetani hasa. Ikiwa kuna hali kama hizo zilizopo ndani yako, hakika utakuwa hasi mara nyingi, utakuwa wa kawaida kwa nadra, maendeleo yako yatapungua. Watu wengine wana matatizo machache na hawawazi sana hivyo, kwa hivyo huingia ndani haraka. Wao ni sahili na hivyo hawapitii matatizo mengi sana; lakini wewe huwaza sana, mawazo yako na hisia zako ni nzito na wewe hulenga vitu vingi sana na una mahitaji mengi sana kwa Mungu. Hivyo wewe hupitia shida zaidi na una vikwazo zaidi. Mtu wa aina hii ana shida kuingia ndani. Watu wengine watatafuta kwa namna moja bila kujali jinsi wengine wanavyowatendea; hawaathiriki kamwe. Nyoyo zao zimefunguka wazi, hivyo hawatapitia matatizo mengi; wataingia ndani kwa kawaida na hawatakuwa na vikwazo vingi. Wewe husumbukia mambo mengi sana; leo unawaza suala hili na kesho unawaza lile. Mtu fulani anaweza kukutupia jicho vibaya, akuangalie kwa dharau au kukupuuza, au Mungu huenda akasema neno ambalo linakuchochea, likakusumbua, linakuumiza, linaloumiza kujistahi kwako, huuchoma moyo wako, au unaweza kutotendewa heshima wakati unakula chakula, au kitu kizuri kinapewa mtu mwingine badala yako. Unawaza sana, moyo wako ni changamano sana, wewe huna busara kabisa, msimamo wako ni wa chini zaidi, uadilifu wako ni wa chini sana, na wewe ni msumbufu zaidi na ni mgumu wa kushughulikiwa. Una dosari nyingi sana; Je, ni ukweli kiasi gani unapaswa kuelewa na utahitaji muda gani wa kusafishwa ili ubadilike? Umefungashwa katika vitu vingi mno, mawazo yako ni changamano na mazito visivyo kawaida. Mtu wa aina hii lazima akabiliwe na shida nyingi na kumwaga machozi zaidi. Si rahisi kupatana na kushirikiana na mtu wa aina hii. Nyinyi mara nyingi hupashana mambo haya na baadhi ya watu husema: "Mimi niliteleza katika jambo fulani, na nilielewa baada ya kupitia matatizo kadhaa" Watu wengi wana aina hii ya uzoefu. Inaweza kuwa imechukua miaka kadhaa kufikia ufahamu huu; ufahamu na mabadiliko haya vinaweza kuwa vimekuja baada ya maumivu makali na uchungu wa kupita kiasi wa kusafishwa. Ni la kusikitisha mno! Jinsi uchafu ulivyo mwingi katika imani ya watu! Imani yao kwa Mungu ni ngumu sana kwao! Hata leo, kila mtu ana uchafu mwingi ndani. Kiasi cha mahitaji uliyo nayo kwa Mungu ni kiasi cha uchafu ulio nao ndani. Uchafu huu unathibitisha kuwa kuna tatizo na mantiki ya watu. Uchafu huo pia ni mfichuo wa asili za watu. Unapaswa kuwa na uwezo wa kutofautisha ni maombi yapi watu waliyo nayo kwa Mungu yanayofaa na yale ambayo hayafai. Ni lazima uwe wazi juu ya ni wapi watu wanapaswa kusimama na ni sababu zipi wanazopaswa kuwa nazo. Watu wengine wako hivi, na mioyo yao daima hushika vitu hivi: ni akina nani Mungu ni mwema kwao au sio mwema kwao, au ni akina nani ambao Hapendezwi nao. Wakigundua kwamba Yeye hafurahishwi nao, au wakisikia maneno yoyote juu yao, basi hawataachilia, na haijalishi jinsi unavyolieleza jambo kwao, haitakuwa na maana yoyote, na hawataweza kugeuka kwa muda mrefu. Watafikia uamuzi bila kutafakari kujihusu na wataelewa kirai kimoja kuamua mitazamo ya Mungu kuwahusu. Bila kujali unachosema ili kuwaeleza jinsi wanavyopaswa kutafuta kwa kawaida au jinsi wanavyopaswa kuitembea njia iliyo mbele, hawatahisi kwamba kinachosemwa ni juu yao; watahisi kuwa ni kuwadanganya. Inaweza kuonekana kuwa watu hawaelewi tabia ya haki ya Mungu hata kidogo; hawaelewi hasa kwamba kuna mchakato wa kubadilisha na mtazamo wa Mungu kwa watu utabadilika. Ikiwa mtazamo wako kwa Mungu haubadiliki, basi mtazamo Wake kwako unaweza kubadilika? Ukibadilika, basi Mungu Atabadilisha jinsi anavyokutendea. Usipobadilika, basi Yeye Hatabadilika. Kuna watu ambao bado hawaelewi wazi mambo ambayo Mungu hudharau na mambo ambayo Yeye hupenda, wala huwa hawaelewi hisia Zake za ridhaa, hasira, huzuni, na furaha. "Mungu ni mwenyezi na mwenye busara; Yeye ni mwenye hekima sana, kiasi kwamba watu hawaelewi kwa dhahiri." Watu wanahisi kuwa hawawezi kuelewa vizuri. Hili ndilo jambo gumu kwa watu. Watu huwa hawakumbuki ushauri wenye ari na wenye nia nzuri unaosemwa kwao; kama neno la ukali linasemwa kwao, au maneno ya kupogoa, kushughulika, na hukumu yanasemwa kwao, huichoma mioyo yao. Basi kwa nini watu huwa hawachukui ushauri bayana bila utani? Kwa nini wao hukosa raha na kuwa hasi, na kwa nini hawawezi kuamka tena baada ya kusikia maneno fulani ya hukumu na kupogoa na kushughulika? Mwishowe, huenda wakageuka baada ya kutafakari kwa muda mrefu; Na wao watarudi kwa hali halisi tu kwa msaada wa kirai cha maneno ya kufariji. Bila maneno haya ya faraja, hawataamka. Watu wanapoanza kupata uzoefu, wanakuwa na kutokuelewa kwingi na kuelewa mambo visivyo; watu siku zote hufikiri kwamba wao wako sahihi, na wao hawawezi kuwasikiliza watu wengine bila kujali wanawasemesha nini. Baada ya kupata uzoefu kwa miaka mitatu hadi mitano, wao huanza kuelewa na kuona kwa dhahiri, na watahisi kuwa wamekuwa wagumu wa kushughulikiwa kana kwamba hatimaye wamekua wakomavu. Watu wenye uzoefu mwingi humuelewa Mungu na wana visa vichache vya kuelewa mambo visivyo. Hawalalamiki tena na wao huanza kuamini katika Mungu kama kawaida. Kwa kulinganisha na kimo chao katika siku za nyuma, wao hujihisi kukua zaidi sasa. Katika siku za nyuma, walikuwa kama watoto wachanga, daima wenye hasira na hasi, wakijitenga kutoka kwa Mungu, mara nyingi wakiwa na malalamiko kwa ndani na kuwa na shaka. Sasa kuna maendeleo na hali zao ziko imara zaidi kuliko hapo awali. Haya ndiyo matokeo ya kuuelewa ukweli na athari ambazo ukweli unazo kwa watu. Hiyo ni kusema, almradi watu wanavyouelewa ukweli, wanaweza kutatua matatizo kiasi chochote; mradi watu wanaweza kuukubali kweli, wanaweza kutatua shida yoyote. Kwanza kabisa linahusiana na uzoefu na wakati wa watu, na inachukua mchakato. Kwa kuwatumia kufanya kazi sasa haimaanishi kwamba mna kimo kikubwa; wewe mna sifa nzuri zaidi kiasi tu kuliko watu wa wastani, mnatafuta zaidi kidogo kuliko wao na kuwa na thamani kidogo ya kuendeleza zaidi kuliko wao; lakini hiyo haimaanishi kwamba unaweza kumtii Mungu na kuweza kuikubali mipango ya Mungu, na haimaanishi kuwa umeyaacha matarajio na matumaini yako ya baadaye. Watu bado hawafikirii hivi; nyinyi nyote mna mielekeo hasi na mna hali fulani katika kazi yenu. Inaonekana kwamba mnajaribu kuyafidia makosa yako, hujafurahi na huko radhi kufanya kazi hiyo, na hujafikia kiwango ambacho bila kujali jinsi Mungu anavyonitendea, nitalifungia macho na kufanya kazi tu, nitafanya kazi tu kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu na kulingana na mahitaji ya Mungu. Je, mnaweza kufikia hili? Watu hawawazi hivi! Kila mtu anataka kuchunguza: Ni aina gani ya mtazamo ambao Mungu anao kwangu? Je, kweli Yeye anitumia au Yeye anatumia huduma yangu? Kila mtu ana nia ya kuchunguza; je, wewe unadhubutu kusema kwamba huna nia yoyote ya aina hiyo? Kila mtu anayo nia, lakini hakuna mtu anayetaka kulisema. Ukweli kwamba huthubutu kusema inaonyesha kwamba wewe unadhibitiwa na kitu: Hakuna haja ya kuzungumza, hii ni asili yangu na haiwezi kubadilika. Hata hivyo, juu ya kile ninachoweza au nisichoweza kufanya, bora nina ufahamu, nimemaliza. Mradi sifanyi mambo mabaya basi mimi niko sawa. Mahitaji yangu si ya juu vile. Wewe hujiwekea kiwango cha chini zaidi na mwishowe, hupigi hatua yoyote. Unapofanya kazi, wewe hufanya kazi bila uangalifu, na hatimaye, baada ya kuwasiliana nanyi mara chache, mnaelewa kidogo na mna ufahamu kidogo. Kutumiwa au kutotumiwa na mitazamo ya Mungu kukuelekea wewe si vitu muhimu. La muhimu ni kuhusu bidii yako ya nafsi, kama unaweza kubadilika au la; na njia unayoichagua. Hivi ndivyo vitu vya umuhimu zaidi. Haina faida wakati mtazamo wa Mungu kwako ni mzuri lakini hubadiliki. Wakati mtazamo Wake kwako ni mzuri, lakini jambo fulani likujie nawe uanguke, haina maana. Je, la muhimu bado halihusiani na njia unayoichukua? Katika siku za nyuma, maneno ya laana na kukirihi na kuchukia yamesemwa kwako, lakini leo umebadilika, kwa hivyo mwelekeo wa Mungu kwako pia umebadilika hatimaye. Watu daima huhisi hofu na kukosa usalama. Hii inathibitisha kwamba bado hawayaelewi mapenzi ya Mungu. Sasa vile jambo hili li wazi, je, jambo la aina hii bado linaweza kutokea baadaye wakati jambo fulani linakujia? Je, mna ufahamu kiasi wa asili zilizo ndani ya watu na kila kipengele cha mantiki ya kibinadamu? Je, mna kidokezo? Katika siku za nyuma, watu wengine wamefukuzwa kwa kufanya mambo kadhaa mabaya na kanisa limewakataa. Wanatangatanga kwa miaka kadhaa, na kisha wanarudi. Ni vizuri kwamba hawajatoroka kabisa; kwa kuwa hawajatoroka kabisa, wana fursa na tumaini la kuokolewa. Kama wangetoroka na hawakuamini, na wakawa kama makafiri, basi wangekwisha kabisa. Kama wanaweza kugeuka, basi wana tumaini. Hii ni nadra na ya thamani. Bila kujali jinsi Mungu huwafinyanga watu na bila kujali jinsi Mungu huwatendea watu, huwachukia watu, au huwakirihi watu, kama utakuja wakati ambapo watu wanaweza kugeuka, basi Mimi nitapata faraja maalum; hii ina maana kwamba watu bado wana wingi wa Mungu ndani ya mioyo yao, hajapoteza mantiki ya kibinadamu kabisa, hawajapoteza ubinadamu kabisa, bado wana nia ya kumwamini Mungu, na wanatarajia kumkubali na kurudi kwa Mungu. Bila kujali ni nani anayekimbia, wakirudi, na familia hiibado iko katika mioyo yao, Mimi nitakuwa mwepesi wa upendo kidogo na kuhisi faraja; hata hivyo, wale ambao hawarudi kamwe ni wa kudharaulika. Ikiwa wanaweza kurudi na kuanza kuamini katika Mungu kwa kweli, moyo Wangu utajazwa hasa na furaha. Waliweza kurejea, na yaelekea wao hawajanisahau Mimi na wamerejea. Wana moyo na akili kweli. Wakati huo tutakapokutana, Mimi nitaguswa; ulipoenda, kwa hakika ulikuwa hasi na hali yako haikuwa nzuri, lakini sasa umerudi, ambayo inathibitisha kwamba bado una imani kwa Mungu. Hata hivyo, bado haijulikani ikiwa una uwezo wa kuzidi kusonga mbele, kwani watu hubadilika haraka sana. Katika Enzi ya Neema, Yesu alikuwa na huruma na neema kwa watu. Kama kondoo mmoja angepotea miongoni mwa mia moja, angewaacha tisini na tisa na kumtafuta yule mmoja. Fungu hili halielezi tendo la kimitambo, siyo kanuni, lakini linaonyesha nia ya Mungu kwa wanadamu, lengo la dharura la Mungu la kumwokoa binadamu, na mapenzi ya kina ya Mungu kwa wanadamu. Si njia ya kutenda, lakini ni tabia Yake na akili Yake. Kwa hiyo, watu wengine huondoka kwa mwaka mmoja au nusu mwaka, au wana udhaifu mwingi na kuelewa kwing visivyoi. Baadaye, ikiwa wataamka kwa ukweli na wanaweza kuwa na ufahamu na kugeuka na kurudi kwenye njia sahihi, hasa Mimi nitafarijiwa na kupendezwa na hili. Kuwa na uwezo wa kusimama katika dunia ya sasa na enzi ya raha za kimwili na uovu, kuwa na uwezo wa kumkubali Mungu, na kuwa na uwezo wa kurudi kwa njia sahihi na kurudi ni mambo ambayo kwa kweli huleta faraja na ni ya kusisimua. Ukiwalea watoto, bila kujali kama ni watoto, ungesikiaje kama wangekosa kukukubali na wakimbie? Si moyo wako daima ungekataa kufa moyo juu yao na si daima ungefikiri: Mwanangu atarudi lini? Ningependa kumwona. Nimekuwa naye kama mtoto wangu daima; nimemlea na kumpenda. Daima umekuwa ukifikiri kwa njia hii na umetamani siku hiyo ije. Kila mtu ana hali hii. Watu siku hizi wana kimo kidogo, lakini siku moja wataelewa, isipokuwa wasiwe na nia yoyote ya kuamini na hawamtambui Yeye kama Mungu. Kwa mujibu wa kimo cha watu siku hizi, mbali na kushughulikiwa kuhusu matatizo makubwa, wanahitaji pia kusimamiwa mara kwa mara na kuangaliwa kidogo, na hawawezi kabisa kuachwa peke yao; itakuwa vizuri wakati hamtahitaji kuwa na wasiwasi kamwe. Kimo chenu kikiwa vile kilivyo, hamstahili kusimamiwa na kudhibitiwa na watu wengine daima. Kama wengine ni lazima bado wawaangalie na kuwasimamia ili mfanye kazi, basi ni vigumu kuhalalisha na inathibitisha kuwa mmepungukiwa sana na kimo chenu ni kidogo mno. Bila ukweli na mkiwa na kimo kidogo, hamuwezi kumfariji au kumtosheleza Mungu. Mnahitaji kuwa na matilaba na uamuzi kiasi ili Mimi nisiwe na wasiwasi.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni