Sura ya 18 | Maneno ya Mungu
Mwenyezi Mungu alisema:" Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, wanadamu wamepata tena utakatifu waliokuwa nao wakati mmoja. Oh, ya kwamba dunia potovu ya zamani mwishowe imeanguka na kutumbukia ndani ya maji ya taka na, kuzama chini ya maji, na kuyeyuka na kuwa tope! Ah, ya kwamba binadamu wote Niliouumba hatimaye umerudiwa na uhai tena katika mwanga, kupata msingi wa kuwepo, na kuacha kupambana katika tope! Ah, Mambo mengi ya uumbaji Ninayoyashikilia mikononi Mwangu!
Wanawezaje, kukosa kufanywa upya, kupitia maneno Yangu? Wanawezaje, katika mwanga, kukosa kuendeleza kazi zao? Dunia si kimya na nyamavu tena, mbingu si ya ukiwa na yenye huzuni tena. Mbingu na nchi, bila kutenganishwa na utupu tena, zimeungana kama kitu kimoja, kamwe kutotenganishwa tena. Wakati huu wa shangwe, wakati huu wa nderemo, haki Yangu na utakatifu Wangu umeenea kila mahali katika ulimwengu, na binadamu wote wanavisifu bila kikomo. Miji yote ya mbingu inacheka kwa furaha, na falme zote za nchi zinacheza kwa shangwe. Ni nani wakati huu ambaye haonyeshi furaha? Na ni nani wakati huu ambaye halii? Nchi katika hali yake ya asili ni miliki ya mbingu, na mbingu imeungana na nchi. Mwanadamu ni ugwe unaounganisha mbingu na nchi, na kwa sababu ya utakatifu wake, kwa ajili yake kufanywa upya, mbingu haijafichwa tena kutoka kwa nchi, na nchi haiko kimya tena kwa mbingu. Nyuso za binadamu zimezingirwa na tabasamu za shukurani, na nyoyo zao zinadondokwa na utamu usiokuwa na kifani. Mwanadamu hagombani na mwanadamu, wala binadamu kupigana wenyewe kwa wenyewe. Kunao wale ambao, katika mwanga Wangu, hawaishi kwa furaha na wenzao? Kunao wale ambao, katika siku Yangu, hufedhehesha jina Langu? Binadamu wote huelekeza macho yao ya heshima Kwangu, na wao hunililia kwa siri katika nyoyo zao. Nimechunguza kila kitendo cha binadamu: Miongoni mwa wanadamu waliotakaswa, hakuna yeyote aliye mkaidi Kwangu, hakuna anayenielekezea hukumu. Binadamu wote umejawa na tabia Yangu. Kila mtu anakuja kunijua, ananijongelea, na ananiabudu. Msimamo wangu ni mmoja katika roho ya mwanadamu, Nimetukuzwa kwa kiwango cha juu zaidi kwa macho ya mwanadamu, na hububujika katika damu ya mishipa yake. Nderemo za furaha katika nyoyo za wanadamu huenea kila sehemu ya uso wa nchi, hewa ni ya kuchangamsha na bichi, ukungu mzito hauitandai ardhi tena, na mwangaza wa jua huvutia.
Sasa, ona ufalme Wangu, ambamo Mimi ni mfalme juu ya vyote, na Ninamotawala juu ya vyote. Tangu mwanzo wa uumbaji hadi sasa, wana wangu, wakiongozwa na Mimi, wameyapitia matatizo mengi sana ya maisha, dhuluma nyingi sana kutoka kwa ulimwengu, mema na mabaya mengi ya ulimwengu, lakini sasa huishi katika nuru Yangu. Je, ni nani ambaye halii kwa ajili ya dhuluma za jana? Je, ni nani ambaye hatokwi na machozi juu ya dhiki za kuifikia leo? Na tena, kuna wowote ambao hawaichukui fursa hii kujitolea kwa dhati kwa ajili Yangu? Je, kuna wowote ambao hawachukui fursa hii kueleza kwa dhati uchu unaochipuka mioyoni mwao? Je, kuna wowote ambao, wakati huu, hawaongei juu ya yale waliyoyapitia? Wakati huu, binadamu wote wanaziweka wakfu sehemu zao zilizo bora zaidi kwa ajili Yangu. Ni wangapi wanateseka na majuto kwa upumbavu wa giza wa jana, ni wangapi wanajichukia kwa sababu ya malengo ya jana. Binadamu wote wamepata kujijua, wote wameona matendo ya Shetani na maajabu Yangu, na ndani ya nyoyo zao, wametengeneza mahali kwa ajili Yangu. Sitakumbana tena na chuki na kukataliwa miongoni mwa wanadamu, kwani kazi Yangu kubwa imekwisha tekelezwa, na haizuiliwi tena. Leo, miongoni mwa wana Wangu, kunao wowote ambao hawajatafakari kwa niaba yao wenyewe? Kunao wowote ambao hawana sababu ya ziada ya masumbuko kwa ajili ya njia ambazo kwazo kazi Yangu ilifanywa? Kunao wowote ambao wamejitolea kwa kweli kwa ajili Yangu? Uchafu ulio ndani ya mioyo yenu umepungua? Ama umeongezeka? Iwapo sehemu chafu katika nyoyo zenu hazijakuwa nyingi ama chache, watu kama hawa Nitawatupa nje bila shaka. Wale Ninaowataka ni watakatifu wanaofuata moyo Wangu, sio nafsi chafu zinazoniasi. Hata kama Siulizi mengi kutoka kwa binadamu, ulimwengu wa ndani wa nyoyo za watu una changamano kiasi kwamba binadamu hauwezi kuafikiana na mapenzi Yangu bila kusita ama mara moja kutosheleza mahitaji Yangu. Wengi wa wanadamu wanaweka jitihada kisiri kwa matumaini ya kuweza kupata laurusi ya kuvishwa taji hatimaye. Idadi kubwa ya wanadamu wanajitahidi kwa nguvu zao zote, bila kuzembea hata kidogo, wakihofia kutekwa nyara na Shetani tena. Hawathubutu tena kuwa na manung’uniko juu Yangu, lakini daima huonyesha utiifu wao Kwangu. Nimesikia maneno yaliyozungumzwa kutoka kwa moyo na watu wengi, visa vilivyosimuliwa na watu wengi sana juu ya matukio machungu ya mateso; Nimeona wengi sana, katika dhiki kubwa sana, wakinipa utiifu wao bila kukosa, na kuona wengi sana, walipopitia kwenye shida, wakipambana kutafuta suluhisho. Katika hali hizi, hawajawahi kulalamika; hata wakati, wakishindwa kupata mwanga, walijipata kuwa wenye huzuni kidogo, hawajawahi kulalamika hata mara moja. Lakini pia Nimesikia watu wengi sana wakitoa mawazo yao bila woga kwa maapizo kutoka kwa vina vya nyoyo zao, wakiilaani Mbingu na kuishutumu nchi, na Nimeona, vilevile, watu wengi sana wakijiruhusu kukata tamaa katikati ya dhiki yao, wakijitupa mbali kama taka kwa jaa, halafu kufunikwa kwa uchafu na masizi. Nimesikia watu wengi sana wakigombana baina yao, kwa sababu mabadiliko katika cheo, pamoja na mabadiliko ya “uso” yanayoandamana nayo, yamesababisha mabadiliko katika uhusiano wao na binadamu wenzao, hivi kwamba marafiki wanaacha kuwa marafiki na kuwa maadui, huku wakishambuliana kwa midomo. Wengi wa watu hutumia maneno Yangu kama risasi kutoka kwa bombomu, wakiwafyatulia wengine kwa ghafla, hadi ulimwengu wa waume umejawa kila mahali na makelele yanayoharibu kimya kitulivu. Kwa bahati nzuri, sasa ni leo ; ama sivyo ni nani anayejua ni wangapi wangekuwa wamekufa kupitia kwa mfululizo usio na huruma wa moto huu wa bombomu.
Kufuatia maneno yanayotoka Kwangu, na kwenda sambamba na hali za binadamu wote, ufalme Wangu, hatua kwa hatua, hushuka duniani. Mwanadamu hahodhi tena fikira zenye wasiwasi, ama “kuzingatia” mambo ya watu wengine, au “kutafakari” kwa niaba yao. Na kwa hivyo, migogoro yenye ubishi haipo tena, na, kufuatia maneno yanayotoka Kwangu, baadhi ya “silaha” za enzi ya kisasa zimeondolewa pia. Binadamu hupata amani na binadamu, moyo wa binadamu hunururisha roho ya uwiano tena, hakuna yeyote mwenye mwelekeo wa kujikinga dhidi ya mashambulizi ya siri. Binadamu wote wamerudia hali yao ya kawaida na kuanza maisha mapya. Wakiishi katika mazingira mapya, idadi kubwa ya watu huangalia kandokando yao, wakihisi kana kwamba wameingia katika ulimwengu mpya kabisa, na kwa sababu ya hili wanashindwa kubadilika mara moja katika mazingira yao ya sasa ama kushika njia nyofu. Na kwa hivyo linakuwa ni jambo la “roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu” kwa kadiri binadamu unavyohusika. Ingawa Mimi, kama mtu, sijaonja machungu ya mashaka Mwenyewe, Nayajua yote ya kujulikana kuhusu upungufu wa mwanadamu. Ninayaelewa kwa undani mahitaji ya mtu, na uelewa Wangu wa udhaifu wake ni mtimilifu. Kwa sababu hii, Simfanyii mzaha binadamu kwa dosari zake; Mimi husimamia tu, kulingana na matendo yake dhalimu, kipimo mwafaka cha “elimu”, bora zaidi ili kumwezesha kila mtu kushika njia nyofu, ili kwamba binadamu uache kuwa mayatima wanaozurura na kuwa watoto wachanga wenye nyumba. Hata hivyo, matendo Yangu yanaelekezwa na kanuni. Kama wanadamu hawataki kufurahia upeo wa furaha iliyo ndani Yangu, Ninaweza tu kukubaliana na uchu wao na kuwatupa kuzimu. Katika hatua hii, hakuna anayestahili kuyahodhi malalamiko moyoni mwake tena, ila wote wanapaswa kuona haki Yangu katika mipango ambayo Nimeifanya. Siulazimishi binadamu kunipenda Mimi, wala Sitampiga mwanadamu yeyote kwa kunipenda Mimi. Ndani Yangu ni uhuru kamili, ufunguliwaji kamili. Ingawa majaliwa ya mtu yamo mikononi Mwangu, Nimempa binadamu hiari ambayo haitegemei uongozi Wangu. Kwa njia hii, wanadamu hawatabuni njia za kuingia katika matatizo kwa sababu ya amri Zangu za kiutawala, bali, kwa kutegemea ukarimu Wangu, watajipatia ufunguliwaji. Na kwa hivyo watu wengi, bila kufungiwa katika kizuizi Kwangu, huenda kutafuta njia yao wenyewe ya kutoka, katika tendo la kupata ufunguliwaji.
Daima Mimi huushughulikia binadamu kwa mkono mkarimu, bila kusababisha matatizo yasiyoweza kutatulika, bila kuweka mtu yeyote katika shida; je, si hivi ndivyo? Ingawa watu idadi kubwa hawanipendi, bila kukasirishwa na mtazamo wa aina hii, Nimewapa wanadamu uhuru, kuwaruhusu hiari kiasi kwamba nimewaacha kuogelea pote katika bahari chungu. Kwa kuwa mtu ni chombo na hastahili kudhaminiwa: Ingawa yeye huona baraka Ninayoibeba mkononi Mwangu, hana shauku ya kuifurahia, ila angefurahia kuchomoa mjeledi kutoka kwa mkono wa Shetani matokeo yake yakiwa ni kujihukumu mwenyewe kumung’unywa na Shetani kama “chakula”. Bila shaka, kuna wengine ambao wameiona nuru Yangu kwa macho yao, na kwa hivyo, hata kama wao wanaishi katika ukungu wa wakati huu, hawajapoteza imani katika mwanga kwa ajili ya ukungu huu wenye giza, lakini wameendelea kupapasa na kutafuta kupitia kwa ukungu—ijapokuwa katika njia ilichozagazwa vikwazo. Mwanadamu anaponiasi, Mimi humwelekezea hasira Zangu zenye ghadhabu, na kwa hivyo mwanadamu anaweza kuangamia kwa ajili ya kutotii kwake. Anaponitii, Mimi hubaki nimejificha kutoka kwake, kwa njia hii nikiamsha pendo katika kina cha moyo wake, pendo ambalo halinuii kulaghai ila kunipa raha. Ni mara ngapi, katika uchunguzi wa mwanadamu kunipata, Nimefunga macho Yangu na kukaa kimya, kwa kusudi la kuvuta imani yake ya kweli? Lakini wakati Nimekosa kuongea, imani ya mwanadamu hubadilika ghafula, na hivyo kile Ninachokiona tu ni “mali” ghushi, kwa sababu mwanadamu hajawahi kunipenda kwa dhati. Ni wakati tu Ninapojidhihirisha Mwenyewe ndiyo kwamba binadamu wote hufanya onyesho kubwa la “imani”; lakini wakati Nimejificha katika pahali Pangu pa siri, wanakua dhaifu na kudhoofika moyo, kama kwamba wanahofia kunikosea, au hata kwa sababu baadhi yao hawawezi kuuona uso Wangu, wananishughulikia kikamilifu na kutokana na hilo wanakata kauli kuwa kwa kweli Mimi Siishi. Je, ni watu wangapi hubaki katika hali hii, ni watu wangapi wana fikira za aina hii, lakini ni kwamba wanadamu wote ni wazuri kwa kuficha yale ya aibu ndani yao. Kwa sababu ya hili, hawako radhi kutangaza dosari zao wenyewe, na hukubaliana na ukweli wa maneno Yangu tu ilhali wakitafuta bila haya majificho ya kuzikinga staha zao binafsi.
Machi 17, 1992

kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni