Sura ya 16 | Kanisa la Mwenyezi Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Kuna mengi Mimi natamani kumwambia mwanadamu, mambo mengi sana ambayo lazima Nimwambie. Lakini uwezo wa mwanadamu wa kukubali una upungufu mwingi: Hana uwezo wa kuyaelewa kabisa maneno Yangu kulingana na kile Ninachokitoa, na anaelewa kipengele kimoja tu lakini haelewi vingine. Lakini Simmalizi mwanadamu kwa ajili ya ukosefu wa nguvu wake, wala Siudhiki na udhaifu wake.
Naifanya tu kazi Yangu, na kuongea kama Nimekuwa Nikifanya daima, hata kama mwanadamu haelewi matakwa Yangu; siku itakapokuja, watu watanijua Mimi ndani kabisa ya nyoyo zao, na watakuja kunikumbuka Mimi kwenye mawazo yao. Nitakapoondoka duniani ndipo haswa Nitakapopanda arshi kwenye moyo wa binadamu, ndivyo kusema, itakuwa wakati watu wote watakuja kunijua Mimi. Hivyo pia, itakuwa wakati wana Wangu na watu watatawala dunia. Wale ambao wanijua Mimi bila shaka watakuwa nguzo za ufalme Wangu, na wao peke yao watastahiki kutawala na kuwa na nguvu kwenye ufalme Wangu. Wote ambao wanijua Mimi wamemilikiwa na nafsi Yangu, na wana uwezo kuishi kwa kunidhihirisha miongoni mwa watu wote. Sijali mwanadamu ananijua Mimi kwa kiwango gani: Hakuna yeyote anayeweza kuzuia kazi Yangu kwa njia yoyote, na mwanadamu hawezi kunipa Mimi usaidizi wowote wala kunifanyia Mimi lolote. Mwanadamu anaweza tu kufuata mwongozo Wangu kwenye mwangaza Wangu, na kutafuta matakwa Yangu kwenye mwangaza huu. Leo, watu wamehitimu, na wanaamini wanaweza kutembea kwa maringo mbele Yangu, na kucheka na kufanya mzaha na Mimi bila kizuizi hata kidogo, na kunihutubia Mimi kama wenzao. Bado mwanadamu hanijui Mimi, bado anaamini kuwa kiasili sisi ni kama tuko sawa, kuwa sisi sote ni wa nyama na damu, na sote tunaishi kwenye dunia ya binadamu. Heshima kuu yake Kwangu ni kidogo sana; ananiheshimu Mimi anapokuwa mbele Yangu, lakini hawezi kunihudumia Mimi mbele ya Roho. Ni kama, kwa mwanadamu, Roho hayupo kabisa. Kwa hivyo, hakuna mwanadamu ashawahi kumjua Roho; katika kupata mwili Kwangu, watu huona tu mwili wa nyama na damu, na hawamtambui Roho wa Mungu. Matakwa Yangu yanaweza kupatikana kwa njia kama hii? Watu ni mabingwa wa kunihadaa Mimi; wanaonekana kama ambao wamepewa mafunzo maalum na Shetani ili kunihadaa Mimi. Lakini Shetani bado hanibabaishi Mimi. Bado Nitatumia hekima Yangu kuwashinda wanadamu wote na kumshinda ambaye anawapotosha wanadamu wote, ili ufalme Wangu uanzishwe duniani.
Miongoni mwa binadamu, kuna wale ambao wamejaribu kujua ukubwa wa nyota, au upana wa mbingu. Lakini utafiti wao haujawahi kuweza kuzaa matunda, na hawana hiari ila tu kuinamisha vichwa vyao kwa masikitiko na kukubali kushindwa kwao. Nikiwaangalia watu wote na kuchunguza mienendo ya mwanadamu katika kushindwa kwake, Sioni yeyote yule ambaye ameamini kuhusu Mimi kabisa, hakuna ambaye ananitii Mimi na kujisalimisha Kwangu. Matarajio ya wanadamu ni kaidi kwa kiasi gani! Wakati uso wote wa undani ulikuwa na kiza, miongoni mwa wanadamu Nilianza kuonja uchungu wa dunia. Roho Yangu husafiri kote duniani na kuangalia ndani ya nyoyo za watu wote, licha ya hayo, pia, Mimi hushinda mwanadamu katika nyama ya kuwa mwili Kwangu. Mwanadamu huwa hanioni Mimi, kwa kuwa yeye ni kipofu; mwanadamu hanijui Mimi, kwani amekuwa hana hisia; mwanadamu hunipinga Mimi, kwa kuwa amekuwa si mtiifu; mwanadamu huja kusujudu mbele Yangu, kwa kuwa ameshindwa na Mimi; mwanadamu huja kunipenda Mimi, kwa kuwa Nastahili kiasili kupata upendo wa mwanadamu; mwanadamu huishi kulingana na Mimi na kunidhihirisha Mimi, kwa sababu nguvu Zangu na hekima Yangu humfanya autafute moyo Wangu. Nina nafasi katika moyo wa mwanadamu, lakini kamwe Sijawahi kupokea upendo wa mwanadamu Kwangu katika roho yake. Kwa kweli, kuna mambo katika roho ya mwanadamu anayoyapenda kuliko yote mengine, lakini Mimi si mojawapo wa mambo hayo, na kwa hivyo upendo wa mwanadamu ni kama kiputo cha sabuni: Upepo unapovuma, hukipasua na kimeenda, kisiwahi kuonekana tena. Mtazamo Wangu kuhusu mwanadamu ni wa daima na haujawahi kubadilika. Kuna yeyote kati ya wanadamu, ambaye angeweza kufanya vivyo hivyo? Machoni mwa mwanadamu, Mimi sigusiki wala Mimi sionekani na ni kama hewa, na kwa sababu hii, idadi kubwa ya watu hutafuta tu katika anga isiyokuwa na mipaka, au juu ya bahari ambayo si tulivu, au juu ya ziwa tulivu, au miongoni mwa barua na mafundisho tupu. Hakuna mtu hata mmoja anayejua kiini cha binadamu, kwa kiasi cha chini zaidi wala mmoja anayeweza kusema chochote kuhusu fumbo lililo ndani Yangu, na kwa hivyo huwa Siulizi mwanadamu afikie viwango vya juu zaidi ambavyo yeye hudhani Nahitaji kutoka kwake.
Ndani ya maneno Yangu, milima hupinduliwa, maji hutiririka kinyumenyume, mwanadamu huwa mtiifu, na maziwa huanza kutiririka bila kusita. Ingawa bahari isiyo tulivu hulipuka kwa hasira kuelekea mbinguni, ndani ya maneno Yangu bahari za aina hii hutulia kama uso wa ziwa. Kwa kupunga mkono Wangu kidogo tu, upepo mkali kabisa hutokomea na kutoka Kwangu mara moja, na ulimwengu wa mwanadamu hurejesha utulivu wake mara moja. Lakini Ninapoamua kutoa ghadhabu Yangu, milima hupasuliwa vipande mbalimbali mara moja, ardhi huanza kutetemeka mara moja, maji hukauka mara moja, na mwanadamu huzingirwa na maafa mara moja. Kwa ajili ya ghadhabu Yangu, huwa Mimi sisikilizi vilio vya mwanadamu, huwa sitoi msaada ili kujibu vilio vyake, kwani hasira Yangu inapanda. Ninapokuwa miongoni mwa mbingu, kamwe nyota hazijawahi kutishiwa na kuwepo Kwangu. Bali, huwa zinaweka nyoyo zao kunifanyia kazi Mimi, kwa hivyo, Mimi huzipa mwangaza zaidi na kuzifanya zing’are zaidi, ili zipate utukufu zaidi kwa ajili Yangu. Kila mbingu inapong’aa zaidi, ndivyo dunia chini yake inazidi kuwa na giza; watu wengi hulalamika kuwa mipango Yangu huwa hayafai, wengi wameniacha kuunda ufalme wao wenyewe, ambao wanautumia kunisaliti, na kubadili hali ya giza. Ila nani ameweza kutimiza hili kwa azma yao? Na nani amefaulu katika azimio lake? Nani anaweza kubadili yale ambayo yamepangwa na mkono Wangu? Wakati majira ya machipuko yanaenea kwenye ardhi, Mimi hupeleka mwangaza kwa siri na kimya ulimwenguni, ili, duniani, wanadamu wawe na hisia ya usafi kwenye hewa. Hata hivyo, wakati huo huwa Ninafunika macho ya mwanadamu, ili awe anaona tu ukungu ukiwa umefunika ardhi, na watu na vitu vyote havibainiki. Watu kupumua tu kwa masikitiko. Mbona mwangaza uling’aa kwa muda mdogo tu? Kwa nini Mungu humpa binadamu ukungu na utusitusi tu? Huku kukiwa na kukata tamaa miongoni mwa watu, ukungu hupotea mara moja, lakini wanapoona dalili ya mwangaza, Mimi huachilia mkaragazo wa mvua juu yao, na viini vyao vya masikio vinavunjwa kwa ajili ya mvua ya ngurumo na radi wanapolala. Wanaposhikwa na hofu, hawana wakati wa kupata pahali pa kujificha, na hugubikwa na mvua kubwa. Hapohapo, yote yaliyo chini ya mbingu hufagiliwa katika ghadhabu Yangu ya kuchukizwa. Watu hawalalamiki tena kuhusu mwanzo wa mvua kubwa, na ndani yao wote, heshima kuu huzaliwa. Kwa sababu ya uvamizi huu wa ghafla wa mvua, idadi kubwa ya watu wanazama ndani ya maji yanayonyesha kutoka mbinguni, na kuwa maiti ndani ya maji. Naangalia dunia nzima na kuona kuwa wengi wanaamka, kuwa wengi wanatubu, kuwa wengi wanatafuta chanzo cha maji katika mashua ndogo, kuwa wengi wananisujudu Mimi na kuomba msamaha Wangu, kuwa wengi wameona mwangaza, kuwa wengi wameona uso Wangu, kuwa wengi wana ujasiri wa kuishi, na kuwa ulimwengu mzima umebadilishwa. Kufuatia mkaragazo huu mkubwa wa mvua, vitu vyote vimerudi kama vile Ninavyoyafikiria katika akili Yangu, na haviasi tena. Kabla ya muda mrefu, ardhi yote imejaa sauti za vicheko, na kila mahali duniani kuna mazingira ya sifa, na hakuna popote ambapo hakuna utukufu Wangu. Hekima Yangu iko kote duniani, na katika ulimwengu mzima. Miongoni mwa vitu vyote, kuna matunda ya hekima Yangu, miongoni mwa watu wote, kumejaa sanaa bora zaidi za hekima Yangu; kila kitu ni kama mambo yote katika ufalme Wangu, na watu wote wanakaa kwa mapumziko chini ya mbingu Zangu kama kondoo kwenye uwanja wa malisho Wangu. Nasonga juu ya wanadamu wote na Natazama kila mahali. Hakuna kinachokaa kizee wakati wowote, na hakuna mtu yuko alivyokuwa. Ninapumzika katika enzi, Naegemea juu ya ulimwengu mzima, na Nimeridhika kikamilifu, kwani kila kitu kimerejesha utakatifu wake, na Ninaweza kukaa kwa amani ndani ya Zayuni tena, na watu duniani wanaweza kuishi maisha tulivu na ya kuridhisha chini ya mwongozo Wangu. Watu wote wanasimamia kila kitu mkononi Mwangu, watu wote wamerejesha akili yao ya awali na mwonekano wao wa kiasili; hawafunikwi tena na vumbi, lakini, ndani ya ufalme Wangu, ni wasafi kama lulu, kila mmoja akiwa na uso kama wa mtakatifu ndani ya moyo wa binadamu, kwani ufalme Wangu umekuwa imara miongoni mwa binadamu.
Machi 14, 1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni