Kama mamia ya mamilioni ya wafuasi wengine wa Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo - na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri shahiri kwamba sisi pia tunajiamini kutembelea njia ya kutii mapenzi ya Baba aliye mbinguni.
Tunatamani kurudi kwake Bwana Yesu, ujaji tukufu wa Bwana Yesu, kwa mwisho wa maisha yetu hapa duniani, kwa kuonekana kwa ufalme, na kwa kila kitu kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo: Bwana anafika, na analeta maafa, na kuwazawadia walio wema na kuwaadhibu walio waovu, na anawachukua wale wote wanaomfuata na kukaribisha kurudi Kwake angani kumlaki. Kila wakati tunawaza kuhusu haya, hatuna budi ila kujawa na hisia. Tunashukuru kwa kuwa tulizaliwa nyakati za mwisho na tuna bahati ya kutosha ya kushuhudia kuja kwake Bwana. Ingawa tumepitia mateso, yote ni kwa ajili ya malipo ya “utukufu wa milele unaozidi kuwa mwingi sana”; hii ni baraka iliyoje! Hamu hii yote na neema inayopewa na Bwana mara kwa mara hutufanya kuingia kwenye maombi, na hutuleta pamoja kila mara. Labda mwaka ujao, labda kesho, au labda hata mapema wakati mwanadamu hatarajii, Bwana atarejea ghafla, na atatokea kati ya kundi la watu ambao wamekuwa wakimsubiri kwa umakinifu. Sote tunashindana kati yetu, hakuna anayetaka kubaki nyuma, ili kuwa kundi la kwanza la kutazama kuonekana kwa Bwana, na kuwa mmoja ya wale watakaochukuliwa kwenda mbinguni. Tumetoa kila kitu, bila kujali gharama, kwa ajili ya kuwadia kwa siku hii. Baadhi yetu wameacha kazi zao, wengine wameachana na familia zao, wengine kukana ndoa zao, na baadhi yao hata wamepeana akiba zao zote. Ni upendo usio na ubinafsi wa aina gani huu! Uaminifu na utiifu kama huu lazima uwe unashinda ule wa watakatifu wa nyakati za zamani! Kwa kuwa Bwana anavyompa neema yeyote yule ambaye Yeye anataka, na kumrehemu yeyote ambaye Yeye anataka, kujitolea kwetu na matumizi yetu, na matumizi yetu, tunaamini, tayari yametazamika machoni pake. Kwa hivyo, pia, sala zetu za dhati zimefikia masikio Yake, na tunaamini kuwa Bwana atatuzawadia kwa ajili ya kujitolea kwetu. Aidha, Mungu aliturehemu kabla hajauumba ulimwengu, na hakuna atakayenyakua baraka na ahadi Zake kutoka kwetu. Sote tunapanga kuhusu siku za usoni, na kupuuza kwamba kujitolea kwetu na kugharamia ni mambo tunayoweza kutumia ili kuchukuliwa kwenda mbinguni kukutana na Bwana. Pia, bila kusita hata kidogo, sisi tunajiweka kwenye kiti cha enzi cha siku za baadaye, tukitawala mataifa na watu wote kwa jumla, ama tunatawala kama wafalme. Yote haya, sisi huchukulia kama jambo la lazima, kama kitu kinachotarajiwa.
Tunadharau wale wote walio kinyume na Bwana Yesu; na mwishowe, wote wataangamizwa. Nani aliwaambia wasiamini kwamba Bwana Yesu ni Mwokozi? Bila shaka, kuna wakati tunajifunza kutoka kwa Bwana Yesu na tunakuwa na huruma kwa dunia, kwa kuwa hawaelewi, na tunapaswa kuwa wavumilivu na kuwasamehe. Kila kitu tufanyacho ni kwa mujibu wa mafundisho ya Biblia, kwani kila kitu ambacho hakifuatani na Biblia ni uzushi, na madhehebu maovu. Imani kama hiyo imehifadhiwa ndani ya akili zetu. Mola wetu yumo katika Biblia, na tusipoondoka kwenye Biblia basi hatutaondoka kwa Bwana; tukitii kanuni yake, basi tutaokolewa. Sisi husaidiana na kuchochea kila mmoja wetu, na kila wakati tunapokusanyika pamoja ni matumaini yetu kwamba kila kitu tunachosema na kutenda kinaambatana na matakwa ya Bwana na kuwa kinaweza kukubaliwa na Bwana. Licha ya uhasama mkubwa ulioko kwenye mazingira yetu, mioyo yetu imejaa furaha. Tunapowaza kuhusu baraka hizi tunazoweza kupata kwa urahisi, je, kuna kitu ambacho hatuwezi kukiacha? Je, kuna kitu ambacho hatuwezi kutengana nacho? Yote haya ni thabiti, na haya yote yanatazamwa na macho ya Mungu. Sisi, walio wachache na maskini ambao tumeinuliwa kutoka jaani, ni sawa na wafuasi wa Bwana Yesu wa kawaida: Tunaota kuhusu kuchukuliwa kwenda mbinguni, na kubarikiwa, na kutawala mataifa yote. Upotovu wetu umeanikwa peupe machoni pa Mungu, na tamaa zetu na uchoyo zinahukumiwa machoni pa Mungu. Bado, yote haya hutokea bila ajabu, yenye mantiki, na hakuna hata mmoja kati yetu ambaye hushangaa kama hamu yetu ni ya haki, wala hamna kati yetu ambaye anashuku usahihi wa yote yale ambayo sisi tunashikilia. Nani anayeweza kujua mapenzi ya Mungu? Hatujui jinsi ya kutafuta, au kuchunguza, au hata kujishughulisha na njia ambayo mwanadamu hupitia. Kwa maana sisi hujali tu kuhusu kama tutaweza kuchukuliwa kwenda mbinguni, kama tunaweza kubarikiwa, kama kuna pahali tumetengewa kwa ufalme wa mbinguni, na kama sisi tutaweza kupata mgawo wa maji ya uzima wa mto wa maisha na matunda ya mti wa uzima. Je, sisi hatumwamini Bwana, na je, sisi sio wafuasi wake Bwana, kwa ajili ya kupata vitu hivi? Dhambi zetu zimesamehewa, tumetubu dhambi zetu, tumekunywa kikombe cha mvinyo ambao ni mchungu, na tumeweka msalaba migongoni mwetu. Nani anayeweza kusema kuwa gharama ambayo tumelipia haitakubalika na Bwana? Nani anayeweza kusema kuwa hatujatayarisha mafuta yanayotosha? Hatutaki kuwa kama wale bikira wapumbavu, ama kama wale ambao wameachwa. Aidha, tunaomba kila wakati, na kumwomba Bwana atuepushe kutokana na kudanganywa na Kristo wa uongo, kwa maana imeandikwa kwenye Biblia kuwa “Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko pale; msiamini hili. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi. (Matayo 24: 23-24). Sisi sote tumeweka mistari hii ya biblia kwenye kumbukumbu, tunazijua aya hizi toka mbele mpaka nyuma, na tunaziona kama hazina ya thamani, kama maisha, na kama vitambulisho vyetu vya wokovu wetu na kuchukuliwa kwenda mbinguni kwetu….
Kwa maelfu za miaka, wanaoishi wamefariki, wakichukua tamaa zao na ndoto zao, na hakuna anayejua kwa ukweli iwapo wameenda kwa ufalme wa mbinguni. Wafu wanarudi, na wamesahau hadithi zote zilizotokea wakati mmoja, na bado wanafuata mafundisho na njia za babu zetu. Kwa hivyo, miaka inavyopita na siku zinavyosonga, hakuna anayejua iwapo Bwana Yesu, Mungu wetu, kwa kweli hukubali yote tunayoyafanya. Kwa urahisi, tunangojea matokeo na kubashiri kuhusu yale yote ambayo yatatokea. Bado Mungu yu kimya siku zote, na hajawahi kutuonekania, wala kusema nasi. Na kwa hivyo, kwa hiari yetu tunahukumu mapenzi ya Mungu na tabia kwa mujibu wa Biblia na ishara. Sisi tumezoea kimya cha Mungu; tumekuwa na mazoea ya kupima haki na makosa ya tabia zetu kutumia njia zetu za mawazo: tumekuwa na mazoea ya kutumia elimu yetu, dhana, na maadili yetu na kuyafanya yachukue nafasi ya matakwa ya Mungu kwetu sisi; tumekuwa na mazoea ya kufurahia neema ya Mungu; tumekuwa na mazoea ya Mungu kutoa msaada wakati sisi tunahitaji msaada huo; tumekuwa na mazoea ya kunyosha mikono yetu kwa Mungu ili tupate mambo yote, na kumuagiza Mungu; na pia tumekuwa na mazoea ya kufuata mafundisho ya dini, bila kutilia maanani jinsi Roho Mtakatifu hutuongoza; zaidi ya hayo, tumekuwa na mazoea ya siku ambazo sisi ni bwana zetu wenyewe. Tunamwamini Mungu wa namna hii, ambaye hatujawahi kukutana naye. Maswali kama namna tabia Yake ilivyo, utu wake na mali yake, mfano wake, kama tutamjua ama hatutamjua wakati atakaporudi, na kadhalika—haya yote hayana umuhimu. Jambo muhimu ni kuwa Yeye yumo mioyoni mwetu, na kuwa tunamsubiri, na kuwa tunaweza kufikiria jinsi Alivyo. Tunathamini imani yetu, na kuthamini hali yetu ya kiroho. Tunaona kila kitu ni kama samadi, na kukanyaga mambo yote kwa nyayo zetu. Kwa sababu sisi ni wafuasi wa Bwana mwenye utukufu, bila kujali jinsi safari yetu ilivyo ndefu na ngumu, bila kujali shida na hatari inayotukumba, hakuna kitu kitakachosimamisha nyayo tunapomfuata Bwana. “Mto wa maji safi ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo. Na katika kila upande wa ule mto, ulikuwapo ule mti wa uzima, unaozaa matunda aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi: Na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. Wala hapatakuwa na laana tena: Lakini kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo kitakuwa ndani yake; na watumwa wake watamtumikia: Nao watauona uso wake; na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. Na hapatakuwa na usiku pale; wala hawahitaji mshumaa, wala nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwapa nuru: nao watatawala milele hata na milele (Ufunuo wa Yohana 22:1-5). Kila wakati sisi hukariri maneno hayo, mioyo yetu hujawa na furaha isiyo na kifani na maridhio pia, na machozi hutiririka kutoka machoni mwetu. Shukrani ni kwa Bwana kwa kutuchagua, shukrani ni kwa Bwana kwa neema Yake. Mara mia sasa, yeye ametupa uzima wa milele kwa ulimwengu ujao, na kama angetuuliza tufe sasa, tungetii amri hiyo bila kusita hata kidogo. Bwana! Tafadhali njoo hivi karibuni! Usikawie hata dakika moja tena, kwa kuwa sisi tunakutamani na tumeacha kila kitu kwa ajili yako.
Mungu amenyamaza, na kamwe hawajawahi kujionyesha kwetu, ilhali kazi Yake haijawahi kusimamishwa. Yeye huangalia nchi zote, na huamuru vitu vyote, na kuona maneno yote na matendo yote ya mwanadamu. Usimamizi wake hufanywa hatua kwa hatua na kulingana na mpango wake. Usimamizi wake huendelea kimya kimya, bila madhara ilhali nyayo zake, daima hukaribia binadamu, na kiti chake cha hukumu kimeenezwa katika ulimwengu kwa kasi ya umeme, mara moja kikifuatwa na mshuko wa kiti chake cha enzi kati yetu. Ni tukio la adhimu jinsi gani hilo, yaani, tukio hilo ni uwakilishaji wa mandhari kwa makini na wa kuonyesha Mungu ni mkuu. Kama njiwa na kama simba anayenguruma, Roho anawasili kati yetu sisi sote. Yeye ni mwenye hekima, Yeye ni mwenye haki na wa adhimu, Yeye huwasili kati yetu kwa ukimya, na huwasili na mamlaka akiwa amejazwa na upendo na huruma. Hakuna mtu anayefahamu kuja Kwake, hakuna mtu anayekaribisha kuwasili kwake, na zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ambaye anajua chote atakachokifanya Yeye. Maisha ya mwanadamu inabaki ilivyo bila kubadilika; moyo wake hauna tofauti, na siku zinapita kama kawaida. Mungu anaishi kati yetu kama mtu wa kawaida, kama mfuasi asiye na maana na pia kama muumini wa kawaida. Ana shughuli Zake Mwenyewe, malengo Yake mwenyewe, na vile vile, ana uungu usiomilikiwa na binadamu wa kawaida. Hakuna mtu ambaye ameona kuwepo kwa uungu Wake, na hakuna mtu ambaye ametambua tofauti ya kiini Chake na kile cha binadamu. Sisi huishi pamoja Naye, bila mipaka au kuogopa, kwa kuwa sisi humwona tu kama muumini wa kawaida asiye na maana. Yeye huona matukio yetu yote, na fikra na mawazo yetu yote yanaanikwa wazi mbele Yake. Hakuna mtu ambaye hutilia maanani uwepo Wake, hamna aliye na mawazo yoyote ya kazi Yake, na zaidi ya hayo, hakuna mtu ana tuhuma yoyote kuhusu Yeye ni nani. Sisi huendelea na kazi yetu tu, kana kwamba Yeye hahusiani nasi….
Kwa bahati, Roho Mtakatifu huonyesha kifungu cha maneno “kupitia” Kwake, na ingawa inaonekana ni jambo lisilotarajiwa, tunatambua kuwa huo ni usemi wa Mungu, na tunakubali kwa urahisi kutoka kwa Mungu. Hii ni kwa sababu, bila kujali ni nani anayeonyesha maneno haya, ilimradi yanatoka kwa Roho Mtakatifu tunapaswa kuyakubali, na hivyo hatuwezi kuyakana. Matamshi yajayo yanaweza kuwa kupitia kwangu, au kwako, ama yanaweza kupitia yeye. Bila kujali ni nani, yote ni neema ya Mungu. Ilhali bila kujali mtu ni nani, hatufai kumwabudu, kwa kuwa bila kuzingatia chochote kingine, hawezi kuwa Mungu; hatuwezi kwa njia yoyote kumchagua mtu wa kawaida kama huyu, kuwa ndiye Mungu wetu. Mungu wetu ni mkubwa na mwenye kuheshimika; anawezaje kuwakilishwa na binadamu wa kawaida asiye na umuhimu? Zaidi ya hayo, sisi wote tunasubiri ujaji wa Mungu kuturudisha kwa ufalme wa mbinguni, na kwa hivyo mwanadamu asiye na umuhimu mkubwa anawezaje kuhitimu kufanya kazi ngumu kama hiyo? Bwana akirudi tena, ni lazima iwe juu ya wingu jeupe, linaloonekana na wote. Huo utakuwa wa adhimu namna gani! Itakuwaje Awe amejificha kwa ukimya kati ya kundi la watu wa kawaida?
Na bado ni huyu mtu wa kawaida aliyefichika kati ya watu ndiye anayefanya kazi hii mpya ya kutuokoa. Yeye hafafanui chochote kwetu, wala hatuelezi ni sababu gani Amekuja. Yeye tu, anafanya kazi anayotarajia kufanya, na kwa mujibu wa mpango Wake. Maneno Yake na matamshi Yake yanazidi kuja kwa wingi. Kuanzia kufariji, kuonya, kukumbusha, na kupeana onyo mpaka kukaripia na kufundisha nidhamu; kuanzia kutumia sauti ya upole mpaka kutumia maneno makali na ya adhimu—yote yanatia huruma na hofu kwa mwanadamu. Kila kitu Anachosema kinatufikia kwetu na kulenga siri zilizofichwa ndani yetu, maneno Yake huchoma mioyo yetu, huchoma nafsi zetu, na hutuacha tukiwa na aibu na wanyonge. Tunaanza kutafakari iwapo Mungu Aliye katika roho ya huyu mtu kweli anatupenda, na nini hasa Anatarajia kufanya. Labda tunaweza tu kuchukuliwa kwenda mbinguni baada ya kuvumilia maumivu kama hayo? Vichwani mwetu tunafanya hesabu… kuhusu hatima inayokuja na kuhusu majaliwa yetu ya baadaye. Bado hakuna hata mmoja wetu anayeamini kwamba Mungu amechukua mwili na hutenda kazi kati yetu. Japokuwa Amekuwa pamoja nasi kwa muda mrefu, ingawa tayari Yeye amesema maneno mengi uso kwa uso nasi, bado hatuko tayari kumkubali mtu aliye wa kawaida kiasi hicho awe Mungu wa mustakabali wetu, wala hatuna nia ya kumwaminisha mtu asiye na maana udhibiti wa mustakabali na hatima yetu. Kutoka Kwake, daima tunafurahia ugavi wa maji ya uhai, na kwa sababu Yake tunaishi uso kwa uso na Mungu. Sisi tunashukuru tu kwa neema ya Bwana Yesu aliye mbinguni, na hatujawahi kamwe kupa umakini hisia za huyu mtu wa kawaida mwenye kumilikiwa na uungu. Yeye bado, kwa unyenyekevu, hufanya kazi akiwa amefichwa ndani ya mwili , akielezea sauti ya moyo wake, bila kuzingatia kukataliwa Kwake na binadamu, inavyoonekana milele kusamehe utoto na ujinga wa mwanadamu, na milele kuvumilia mwanadamu kutomheshimu.
Pasipo sisi kujua, huyu mtu asiye muhimu ametuelekeza katika hatua baada ya hatua ya kazi ya Mungu. Sisi hupitia majaribu tele, na hukabiliwa na kurudi kusikohesabika, na tunajaribiwa na kifo. Tunajifunza haki ya Mungu na adhama ya tabia Yake, na kufurahia, upendo na huruma Zake, tunakuja kufahamu nguvu za Mungu ambazo ni kubwa na hekima Yake, tunashuhudia uzuri wa Mungu, na kutazama hamu Yake ya kumwokoa mwanadamu. Kwa maneno ya huyu mtu wa kawaida, tunakuja kujua asili na kiini cha Mungu, tunakuja kufahamu mapenzi ya Mungu, tunakuja kujua asili ya mwanadamu na kiini cha mwanadamu, na tunapata kuona njia ya wokovu na ukamilifu. Maneno yake hutufanya sisi tufe, na kutufanya kuzaliwa upya; maneno yake hutufariji, na ilhali pia hutuacha tukiwa tumejawa na hatia na hisia ya kuwa wadeni; maneno yake hutuletea furaha na amani, lakini pia maumivu makubwa. Wakati mwingine sisi ni kama wanakondoo wa kuchinjwa kwenye mikononi Yake; wakati mwingine sisi ni kama kipenzi cha roho yake na kufurahia upendo wake na huba yake; wakati mwingine sisi ni kama adui wake, waliofanywa majivu na ghadhabu yake katika macho yake. Sisi ni wanadamu waliookolewa Naye, sisi ni funza machoni pake, na sisi ni wanakondoo waliopotea ambao Yeye hufikiria kuhusu kuwapata mchana na usiku. Yeye ni mwenye huruma kwetu, anatudharau, yeye hutuinua, yeye hutufariji na kutuhimiza, yeye hutuongoza, yeye hututia nuru, yeye huturudi na kutufundisha nidhamu, na Yeye hata hutulaani. Yeye hujitia wasiwasi usiku na mchana kwa ajili yetu, Yeye hutulinda na kututunza usiku na mchana, na hatuachi kamwe, na Yeye hutoa utunzaji Wake wote kwetu na hulipia gharama yoyote kwa ajili yetu. Miongoni mwa maneno ya mwili huu mdogo na wa kawaida, tumefurahia ukamilifu wa Mungu, na kuona hatima ambayo Mungu ametupa. Ila, licha ya haya, majivuno yangali mioyoni mwetu, na sisi hatuna nia ya kukubali kikamilifu mtu kama huyu kama Mungu wetu. Ingawa Yeye ametupa mana sana, mengi sana ya kufurahia, hamna kati ya haya ambayo yanaweza kunyakua nafasi ya mungu katika mioyo yetu. Tunaheshimu utambulisho maalum wa huyu mwanadamu na hadhi kwa kusita pekee. Kama Yeye haneni na kutufanya kukiri kwamba Yeye ni Mungu, basi sisi kamwe hatuwezi kukata kauli wenyewe na kukiri Yeye ni Mungu, na kuwa Yeye yumo karibu kuja ilhali amekuwa akifanya kazi kati yetu kwa muda mrefu.
Matamshi ya mungu yanaendelea, na Yeye hutumia mbinu mbalimbali na mitazamo kutuonya na kutuelekeza tutakachofanya na kueleza sauti ya moyo Wake. Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, na hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi anavyoongea, na bila hiari tunaanza kuwa na hamu ya sauti ya moyo wa huyu mwanadamu asiye wa ajabu. Yeye hufanya juhudi za mchwa kwa ajili yetu, anapoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa kwa ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na moyo Wake huvuja damu na kulia kwa ajili ya uasi na kufa ganzi kwetu. Utu kama huu na umiliki Wake haupo kwa upeo wa binadamu wa kawaida, na hauwezi kumilikiwa na yeyote aliyepotoka. Ana uvumilivu na subira isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake haumilikiwi na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu ama kiini chetu, ama kuhukumu uasi wetu na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu wa mbinguni. Hakuna mtu ila Yeye anayeweza kumiliki mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho yametoka, kwa ukamilifu wao, kutoka Kwake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana utumwa wa shetani ama upotovu wa tabia yetu potovu Yeye huwakilisha Mungu, na kuonyesha sauti ya moyo wa Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu, yote ambayo huelekezwa kwa mwanadamu. Ameanza enzi mpya, nyakati mpya, na akaleta mbingu na nchi mpya, kazi mpya, na ametuletea matumaini, na akamaliza maisha ambayo si dhahiri, na akatuwezesha kikamilifu kuona njia ya wokovu. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zinapata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na kwa muda amekuwa akikataliwa na sisi—Je, si Yeye ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye Kweli! Yeye ni Mungu wetu. Yeye ndiye kweli, njia, na uzima! Yeye ameturuhusu kuishi tena, na kuona nuru, na kusimamisha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu, tumerejea mbele ya kiti chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na Yeye, tumeshuhudia uso wake, na tumeona barabara iliyo mbele. Wakati huo, mioyo yetu imeshindwa kabisa na Yeye; hatuna shaka kuhusu Yeye ni nani tena, wala hatupingi tena kazi na neno lake, na tunasujudu, kabisa, mbele yake. Hakuna tunachotaka ila kufuata nyayo za Mungu maishani mwetu mwote, na kufanywa wakamilifu naye, na kulipa fadhila yake, na kulipa upendo wake kwetu, na kutii matayarisho na mipangilio yake, na kushirikiana na kazi yake, na kufanya kila kitu tunachoweza ili kukamilisha kile anachotuaminia.
Kushindwa na Mungu ni kama mashindano ya kareti.
Kila neno la Mungu hugonga eneo letu la ubinadamu, na hutuacha tukiwa tumejawa na huzuni na hofu. Yeye hufichua fikra zetu, hufichua mawazo yetu, na hufichua tabia zetu potovu. Kupitia kwa yale yote sisi husema na kuyatenda, na kila wazo na fikra zetu, asili na kiini zinafunuliwa kwa neno lake, na kutuacha na fedheha, tukitetemeka kwa hofu. Anatueleza kuhusu matendo yetu yote, malengo yetu na nia, na hata tabia potovu ambazo hatujawahi kugundua, na kutufanya tuhisi kwamba tumewekwa hadharani, na hata kuhisi tumeshawishika vikamilifu. Yeye hutuhukumu kwa ajili ya upinzani wetu Kwake, hutuadibu kwa ajili ya kufuru kwetu na kumshutumu kwetu, na kutufanya tuhisi kwamba hatuna thamani machoni pake, na kuwa sisi ni Shetani aishiye. Matumaini yetu yanakufa, na kamwe hatuwezi kumpa madai yasiyo na msingi au kumjaribu, na hata ndoto zetu kupotelea mara moja. Huu ni ukweli ambao hakuna kati yetu anaweza kufikiria, na kwamba hakuna yeyote kati yetu anayeweza kukubali. Kwa muda, akili zetu hukosa msimamo, na hatujui tutakavyoendelea na barabara iliyo mbele wala hatujui jinsi ambavyo tutaendelea katika imani zetu. Inaonekana kama imani yetu imerudi kama ilivyokuwa mwanzoni, na ya kuwa hatujawahi kumpata na kumtambua Yesu Kristo. Kila kitu machoni petu hutushangaza, na kutufanya tuhisi ni kama tumetupwa mbali. Tunasikitishwa, tunahuzunika, na ndani ya mioyo yetu kuna ghadhabu ambayo haiwezi kufichika na pia kuna aibu. Tunajaribu kujieleza, kupata suluhisho, na, hali kadhalika, sisi hujaribu kuendelea kumsubiri Mwokozi Yesu, na kueleza mioyo yetu mbele yake. Ingawa kuna wakati mwingine ambao hatuna kiburi wala unyenyekevu kwa kutazamwa nje, mioyoni mwetu tunateseka na kuwa na hisia ya hasara kuliko vile tumewahi kuwa nayo. Ingawa wakati mwingine tunaonekana ni kama tuna utulivu kwa kutazamwa nje, ndani yetu tunavumilia bahari ya mateso inayopanda na kushuka. Hukumu yake na kuadibu Kwake zimechukua matumaini na ndoto zetu zote, na kutuacha bila tamaa zetu kuu na kutokuwa tayari kuamini kuwa Yeye ndiye Mwokozi wetu anayeweza kutuokoa. Hukumu Yake na kuadibu zimefungua ghuba kubwa kati yetu na Yeye na hakuna aliye tayari hata kuivuka. Hukumu na kuadibu Kwake ni mara ya kwanza kwamba sisi tunateseka kwa kupata shida kubwa hivi na udhalilishaji kiasi kikubwa hivyo. Hukumu na kuadibu Kwake vimetuwezesha kwa ukweli kuthamini heshima ya Mungu na kutovumilia kwake kwa makosa ya binadamu, ikilinganishwa na ambavyo sisi ni watu wa hadhi ya chini na najisi. Hukumu Yake na kuadibu vimetufanya sisi kutambua kwa mara ya kwanza, jinsi ambavyo tuna kiburi na wenye majivuno, na jinsi ambavyo mwanadamu kamwe hawezi kulingana na Mungu, ama kuwa sawa na Mungu. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimetufanya tutumaini kutoishi katika tabia potovu kama hiyo, na zimetufanya tutamani kuacha asili kama hiyo na kiini kama hicho haraka iwezekanavyo, na kamwe tusichukiwe Naye wala tusimchafue moyo. Hukumu na kuadibu kwake vimetufanya tufurahie kutii neno Lake, na hatumo tayari kamwe kwenda kinyume na matayarisho na mipangilio yake. Hukumu na kuadibu Kwake kwa mara nyingine, zimetuwezesha sisi tuwe na tamaa ya kutafuta uzima, na zimetuwezesha kufurahia kumkubali kama Mwokozi wetu... Sisi tumetoka nje ya kazi ya ushindi, tumetoka kuzimu, tumetoka nje ya bonde la uvuli wa mauti.... Mwenyezi Mungu ametutamalaki, kundi hili la watu! Ameshinda dhidi ya Shetani, na kuwashinda adui zake!
Sisi ni kundi la watu wa kawaida waliomilikiwa na tabia potovu ya kishetani, sisi ndio watu waliochaguliwa na Mungu kabla ya enzi, na sisi ndio maskini ambao Mungu ameinua kutoka jaani. Kuna wakati tulipomkataa na kumshutumu Mungu, ila sasa kumeshindwa na Yeye. Tumepokea maisha na kupokea njia ya uzima wa milele kutoka kwa Mungu. Bila kujali mahali ambapo tupo hapa duniani, licha ya mateso na dhiki, hatuwezi kuwa mbali na wokovu wa Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa Yeye ndiye Muumba wetu, na ukombozi wetu tu!
Upendo wa Mungu unazidi kuenea kama maji ya chemichemi, na wewe unapewa, na mimi pia, na kwake, na kwa wale wote ambao wanatafuta ukweli kwa kweli na kungoja kuonekana kwa Mungu.
Kama vile daima mwezi hufuata jua, kazi ya Mungu haiishi kamwe, na inatekelezwa kwako, kwangu, kwake, na kwa wale wote ambao hufuata nyayo za Mungu na kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu.
Ilielezewa Machi 23, 2010
kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungum, Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni