Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV |
Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV
Utakatifu wa Mungu (I)
Mwenyezi Mungu alisema,Tumekuwa na ushirika wa ziada wa mamlaka ya Mungu leo, na hatutazungumza kuhusu haki ya Mungu sasa hivi. Leo tutazungumza kuhusu mada nzima mpya—utakatifu wa Mungu. Utakatifu wa Mungu pia ni kipengele kingine cha kiini cha kipekee
cha Mungu, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki mada hii hapa. Hiki kipengele cha kiini cha Mungu ambacho Nitashiriki, pamoja na vile vipengele viwili tulivyoshiriki mbeleni, tabia ya haki ya Mungu na mamlaka ya Mungu—yote ni ya kipekee? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu pia ni wa kipekee, basi msingi wa upekee huu, mzizi wa upekee huu, ni maudhui ya ushirika wetu wa leo. Mnaelewa? Rudieni nyuma Yangu: kiini cha kipekee cha Mungu—utakatifu wa Mungu. (Kiini cha kipekee cha Mungu—utakatifu wa Mungu.) Mnahisi vipi katika mioyo yenu baada ya kurudia kirai hiki? Labda baadhi yenu wana wasiwasi kidogo, na wanauliza, “Mbona kushiriki utakatifu wa Mungu?” Msijali, Nitawazungumzia kuuhusu polepole. Punde tu mtakapousikia mtajua mbona ni muhimu Kwangu kushiriki mada hii.
cha Mungu, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki mada hii hapa. Hiki kipengele cha kiini cha Mungu ambacho Nitashiriki, pamoja na vile vipengele viwili tulivyoshiriki mbeleni, tabia ya haki ya Mungu na mamlaka ya Mungu—yote ni ya kipekee? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu pia ni wa kipekee, basi msingi wa upekee huu, mzizi wa upekee huu, ni maudhui ya ushirika wetu wa leo. Mnaelewa? Rudieni nyuma Yangu: kiini cha kipekee cha Mungu—utakatifu wa Mungu. (Kiini cha kipekee cha Mungu—utakatifu wa Mungu.) Mnahisi vipi katika mioyo yenu baada ya kurudia kirai hiki? Labda baadhi yenu wana wasiwasi kidogo, na wanauliza, “Mbona kushiriki utakatifu wa Mungu?” Msijali, Nitawazungumzia kuuhusu polepole. Punde tu mtakapousikia mtajua mbona ni muhimu Kwangu kushiriki mada hii.
Kwanza wacha tufafanue neno “takatifu.” Mkitumia utambuzi wenu na kutoka kwa maarifa yenu mmefunzwa, mnaelewa ufafanuzi wa “takatifu” kuwa nini? Nifafanulieni. (“Takatifu” inamaanisha bila doa, bila upotovu au dosari yoyote ya binadamu. Kila kitu inachonururisha—kiwe kwa mawazo, matamshi ama vitendo, kila kitu inafanya—ni chema kabisa.) Vizuri kabisa. (“Takatifu” ni ya Mungu, haijanajisiwa, haikosewi na mtu. Ni ya kipekee, ni ishara ya tabia ya Mungu.) (“Takatifu” haina doa na ni kipengele cha Mungu, tabia isiyokosewa.) Huu ni ufafanuzi wako, sio? Katika moyo wa kila mtu, neno hili “takatifu” lina wigo, ufafanuzi na fasiri. Kwa kiwango cha chini kabisa, mnapoona neno “takatifu” akili zenu si tupu. Mna wigo fulani uliofafanuliwa wa neno hili, na ufasiri wa watu wengine wa ufafanuzi huu uko karibu kutumia neno hili kufafanua kiini cha tabia ya Mungu. Hii ni vizuri sana. Watu wengi zaidi wanaamini neno “takatifu” ni neno njema, na hii inaweza kuthibitishwa. Lakini utakatifu wa Mungu Ninaotaka kushiriki leo hautafafanuliwa tu, ama kuelezwa tu. Badala yake, Nitatumia baadhi ya ukweli kudhihirisha ili kukuruhusu kuona kwa nini Nasema Mungu ni mtakatifu, na mbona Natumia neno “takatifu” kuelezea kiini cha Mungu. Kabla ya ushirika wetu kuisha, utahisi kwamba matumizi ya neno “takatifu” kuelezea kiini cha Mungu na matumizi ya neno hili kumrejelea Mungu yanastahili sana na yanafaa. Kwa kiwango cha chini zaidi, kuhusiana na lugha za sasa za binadamu, kutumia neno hili kumrejelea Mungu kunafaa hasa—ni neno pekee kwa lugha ya binadamu linalofaa kabisa kumrejelea Mungu. Si neno tupu linapotumika kumrejelea Mungu, wala si sifa bila sababu au pongezi tupu. Madhumuni ya ushirika wetu ni kumruhusu kila mtu kuutambua ukweli wa uwepo wa kipengele hiki cha kiini cha Mungu. Mungu haogopi uelewa wa watu, bali kutoelewa kwao tu. Mungu anataka kila mtu ajue kiini Chake na kile Anacho na alicho. Hivyo kila wakati tunapotaja kipengele cha kiini Cha Mungu, tunaweza kutumia ukweli mwingi kuwaruhusu watu kuona kwamba kipengele hiki cha kiini cha Mungu kweli kipo na ni cha ukweli sana na halisi sana.
Kwa sababu sasa tuna ufafanuzi wa neno “takatifu,” wacha tuangalie baadhi ya mifano. Katika fikira ambazo watu wanazo, ni rahisi kwao kufikiria vitu na watu wengi “watakatifu.” Kwa mfano, wavulana na wasichana mabikira wanaelezwa kama watakatifu katika kamusi za binadamu? Je, kweli ni watakatifu? (La.) Je, hii inayoitwa “takatifu” na “takatifu” tunayotaka kushiriki leo ni kitu sawa? (La.) Tukiangalia wale miongoni mwa watu walio na maadili ya juu, na matamshi bora na ya maarifa, wasiomwumiza yeyote, ambao, wanapozungumza, wanawafanya wengine kustareheka na kufurahia—ni watakatifu? Wasomi wa Confucius au waungwana walio na maadili ya juu, na wenye ubora wa maneno na vikitendo—ni watakatifu? Wale wanaofanya mazuri mara nyingi, wanaopenda kutoa na kuwasaidia wengine, wanaoleta raha nyingi kwa maisha ya watu—ni watakatifu? (La.) Wale wasio na fikira za kujihudumia kwa wengine, wasioweka madai makali juu ya wengine, wanaomvumilia yeyote—ni watakatifu? Wale ambao hawajawahi kuwa na mzozo na yeyote wala kujinufaisha na yeyote—ni watakatifu? Basi wale wanaofanya kazi kwa minajili ya uzuri wa wengine, wanaofaidi wengine na kuleta uboreshaji kwa wengine kwa namna zote—ni watakatifu? Wanaowapa wengine akiba zao zote za maisha na kuishi maisha rahisi, walio wakali kwa wao wenyewe lakini wanawashughulikia wengine kwa ukarimu—ni watakatifu? (La.) Mnakumbuka kwamba mama zenu waliwatunza na kuwalinda kwa njia zote zinazoweza kufikiriwa—ni watakatifu? Vijimungu mnaopenda sana, wawe watu maarufu, mashuhuri ama watu wakubwa—ni watakatifu? (La.) Haya yote ni ya uhakika. Hebu sasa tuangalie wale manabii katika Biblia walioweza kuelezea siku za baadaye ambazo hazikujulikana na wengine wengi—mtu wa aina hii alikuwa mtakatifu? Watu walioweza kurekodi maneno ya Mungu na ukweli wa kazi Yake katika Biblia—walikuwa watakatifu? (La.) Musa alikuwa mtakatifu? Ibrahimu alikuwa mtakatifu? Ayubu alikuwa mtakatifu? (La.) Mbona mnasema hivi? (Neno “takatifu” linaweza kutumika tu kumrejelea Mungu.) Ayubu aliitwa mtu mwenye haki na Mungu, basi mbona hata yeye anasemekana kutokuwa mtakatifu? Mnahisi wasiwasi kiasi hapa, sivyo? Watu wanaomcha Mungu na kuepukana na maovu kweli si watakatifu? Ni watakatifu ama si watakatifu? (La.) Jibu lenu ni hapana, sio? Basi jibu lenu la hapana limetokana na nini? (Mungu ni wa kipekee.) Huu ni msingi uliopatikana vizuri, msingi mzuri kabisa! Ninagundua kwamba mna uwezo mkubwa wa kuelewa vitu haraka na kutumia mlichojifunza, na kwamba nyinyi nyote mna ujuzi huu maalum. Mna wasiwasi kidogo, hamna uhakika sana, na hamthubutu kusema “La,” lakini pia hamthubutu kusema “Ndiyo,” kwa hivyo mmelazimika kusema “La.” Wacha Niulize swali lingine. Wajumbe wa Mungu—wajumbe ambao Mungu huwatuma chini duniani—ni watakatifu? (La.) Lifikirie kwa makini. Peana jibu lenu baada ya kulifikiria. Malaika ni watakatifu? (La.) Wanadamu ambao hawajapotoshwa na Shetani—ni watakatifu? (La.) Nyinyi nyote mnasema “La” kwa kila swali. Kwa msingi upi? Je, kirai Nilichosema sasa hivi ndicho sababu mnasema “La?” Mmechanganyikiwa, sivyo? Basi mbona hata malaika wanasemekana sio watakatifu? Mna wasiwasi hapa, sio? Basi mnaweza kugundua ni kwa msingi upi watu, vitu ama viumbe wasioumbwa tuliotaja mbeleni si watakatifu? Nina uhakika hamwezi, sio? Hivyo kusema kwenu “La” basi ni kukosekana kwa uwajibikaji kidogo? Hamjibu bila kujali? Watu wengine wanafikiria: “Unauliza kwa namna hii, kwa hivyo si lazima iwe hivyo hakika.” Msijibu tu bila kujali. Fikirieni kwa makini iwapo jibu ni ndiyo au la. Mtajua tutakaposhiriki mada ifuatayo mbona ni “La.” Nitawapa jibu hivi punde. Hebu kwanza tusome baadhi ya maandiko.
1. Amri ya Yehova Mungu kwa Mwanadamu
(Mwa 2:15-17) BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
2. Nyoka Anamshawishi Mwanamke
(Mwa 3:1-5) Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Hivi vifungu viwili ni dondoo kutoka kwa kitabu kipi cha Biblia? (Mwanzo.) Je, nyinyi nyote mnavijua vifungu hivi viwili? Hiki ni kitu kilichofanyika mwanzoni wakati binadamu kwanza aliumbwa; lilikuwa ni tukio halisi. Kwanza hebu tuangalie ni amri ya aina gani ambayo Yehova Mungu aliwapa Adamu na Hawa, kwani yaliyomo katika amri hii ni muhimu sana kwa mada yetu ya leo. “BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema….” Endelea kusoma kifungu kifuatacho. (“Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”) Amri ya Mungu kwa mwanadamu katika kifungu hiki ina nini? Kwanza, Mungu anamwambia mwanadamu kile anachoweza kula, yakiwa ni matunda ya miti ya aina nyingi. Hakuna hatari na hakuna sumu, yote yanaweza kulika na kulika atakavyo mtu, bila wasiwasi wowote. Hii ni sehemu moja. Sehemu nyingine ni onyo. Onyo hili linamwambia mwanadamu kwamba hawezi kula tunda kutoka kwa mti upi? (Mti wa ujuzi wa mema na mabaya.) Lazima asile tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Nini itafanyika akifanya hivyo? (Hakika atakufa.) Mungu alimwambia mwanadamu: Ukilila hakika utakufa. Maneno haya yanaeleweka kwa urahisi? (Ndiyo.) Iwapo Mungu angekwambia jambo hili lakini hukuelewa kwa nini, ungelichukulia kama kanuni ama amri ya kufuatwa? Linapaswa kufuatwa, sivyo? Lakini iwapo mwanadamu anaweza ama hawezi kulifuata, maneno ya Mungu hayaachi shaka. Mungu alimwambia mwanadamu kwa uwazi kabisa kile anachoweza kula na kile asichoweza, na kile kitakachofanyika akila kile hapaswi kula. Umeona tabia yoyote ya Mungu katika haya maneno machache ambayo Alisema? Haya maneno ya Mungu ni ya ukweli? (Ndiyo.) Kuna udanganyifu wowote? (La.) Kuna uongo wowote? (La.) Kuna chochote kinachotisha? (La.) Mungu kwa uaminifu, kwa kweli, kwa dhati Alimwambia mwanadamu kile anachoweza kula na kile asichoweza kula, wazi na dhahiri. Kuna maana iliyofichwa katika maneno haya? Maneno haya yanaeleweka kwa urahisi? Maana yake ni wazi kwa mtazamo mmoja, unaelewa punde tu unapoyaona. Kuna haja yoyote ya dhana? (La.) Kukisia si muhimu, sivyo? Tayari ni wazi kabisa. Katika akili ya Mungu, Anachotaka kusema, Anachotaka kuonyesha, kinatoka katika moyo Wake. Mambo ambayo Mungu anaonyesha ni safi, yanaeleweka kwa urahisi na ni wazi. Hakuna nia za siri ama maana zilizofichwa. Alizungumza moja kwa moja na mwanadamu, Akimwambia kile anachoweza kula na kile asichoweza kula. Hivyo ni kusema, kupitia maneno haya ya Mungu mwanadamu anaweza kuona kwamba moyo wa Mungu ni angavu, kwamba moyo wa Mungu ni wa kweli. Hakuna uwongo kabisa hapa, kukwambia kwamba huwezi kula kile kinacholika ama kukwambia “Ifanye na uone kitakachofanyika” na vitu ambavyo huwezi kula. Anamaanisha jambo hili? (La.) La. Chochote afikiriacho Mungu katika moyo Wake ndicho Anachosema. Nikisema Mungu ni mtakatifu kwa sababu Anaonyesha na kujifichua Mwenyewe ndani ya maneno haya kwa njia hii, unaweza kuhisi kana kwamba Nimefanya jambo lisilokuwa kubwa ama Nimenyoosha ufasiri Wangu mbali kiasi. Kama ni hivyo, usijali, hatujamaliza bado.
Hebu tuzungumze kuhusu “Nyoka Anamshawishi Mwanamke.” Nyoka ni nani? (Shetani.) Shetani anashikilia jukumu la foili[a] katika mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na ni jukumu ambalo hatuwezi kosa kutaja wakati tunaposhiriki utakatifu wa Mungu. Mbona Nasema hivi? (Kwa sababu Shetani ni mwakilishi na muasisi wa yote yaliyo machafu na potovu.) Iwapo hujui uovu na upotovu wa Shetani ama asili ya Shetani, basi huna njia ya kumtambua, wala huwezi kujua utakatifu kweli ni nini. Katika mkanganyiko, watu wanaamini kwamba kile anachofanya shetani ni chema, kwa sababu wanaishi ndani ya aina hii ya tabia potovu. Bila foili[a] , bila chochote cha kulinganisha nacho, huwezi basi kujua utakatifu ni nini, hivyo basi ni lazima mada hii itajwe hapa. Hatujatoa mada hii ghafla kutoka mahali popote, ila badala yake kupitia maneno na matendo yake tutaona jinsi Shetani anavyotenda, jinsi anavyopotosha binadamu, aina ya asili yake na jinsi uso wake ulivyo. Basi mwanamke huyu alimwambia nini nyoka? Mwanamke alimweleza nyoka kile Yehova Mungu alikuwa amemwambia. Tukitathmini alichosema, alikuwa amethibitisha uhalali wa yote ambayo Mungu alikuwa amemwambia? Hangeweza kuthibitisha haya, angeweza? Kama mtu ambaye alikuwa ameumbwa karibuni, hakuwa na uwezo wa kutambua mema kutoka kwa maovu, wala hakuwa na uwezo wa kufahamu chochote karibu naye. Maneno aliyomwambia nyoka yanatwambia kwamba hakuwa amethibitisha maneno ya Mungu kuwa kweli katika moyo wake; alikuwa na mtazamo wa shaka. Hivyo wakati nyoka aliona kwamba mwanamke huyo hakuwa na mtazamo wa uhakika kwa maneno ya Mungu, alisema: “Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” Kuna chochote kibaya na maneno haya? (Ndiyo.) Ni nini kibaya? Someni sentensi hii. (“Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”) Baada ya kusoma hii, mnahisi chochote? Mlipomaliza kusoma sentensi hii, mlipata hisia ya nia za nyoka? (Ndiyo.) Nyoka ana nia gani? (Kumjaribu mwanadamu kufanya dhambi.) Anataka kumjaribu mwanamke huyu kumfanya aache kusikiza maneno ya Mungu, lakini Je, aliongea moja kwa moja? (La.) Hakuongea moja kwa moja, kwa hivyo tunaweza kusema kwamba ana ujanja sana. Anaonyesha maana yake kwa njia ya udanganyifu na ya kukwepa ili kufikia malengo anayonuia ambayo anaficha kutoka kwa mwanadamu ndani yake—huu ndio ujanja wa nyoka. Shetani amewahi kuzungumza na kutenda hivi. Anasema “sio kwa uhakika,” bila kuthibitisha kwa njia moja au nyingine. Lakini baada ya kusikia haya, moyo wa huyu mwanamke mjinga uliguswa? (Ndiyo.) Nyoka alifurahia kwa sababu maneno yake yalikuwa na matokeo yaliyotarajiwa—hii ilikuwa nia ya ujanja ya Nyoka. Zaidi ya hayo, kwa kuahidi matokeo ambayo mwanadamu aliamini kuwa mema, alimshawishi, akisema “siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho.” Hivyo mwanamke anafikiria: “Kufumbuliwa macho yangu ni jambo zuri!” Nyoka kisha anazungumza maneno mazuri zaidi, maneno yasiyojulikana na mwanadamu, maneno yaliyo na nguvu kubwa ya majaribu juu ya wale wanaoyasikia: “nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” Maneno haya yanamvutia mwanamke sana? (Ndiyo.) Ni kama mtu kukwambia: “Uso wako una umbo nzuri. Ni mfupi kidogo katika daraja la pua, lakini ukiirekebisha, utakuwa mrembo wa kupindukia!” Kwa mtu ambaye hajawahi kutaka kufanya upasuaji wa mapambo, moyo wake utaguswa kusikia maneno haya? (Ndiyo.) Kwa hivyo maneno haya ni ya kushawishi? Ushawishi huu huu unakuvutia? Ni wa kujaribu? (Ndiyo.) Je, Mungu husema mambo kama haya? (La.) Kulikuwa na dokezo lolote la haya katika maneno ya Mungu tuliyoyaangalia sasa hivi? (La.) Mbona? Je, Mungu husema Anachofikiria katika moyo Wake? Mwanadamu anaweza kuona moyo wa Mungu kupitia maneno Yake? (Ndiyo,) Lakini wakati nyoka alikuwa amesema maneno haya kwa mwanamke, uliweza kuona moyo wake? (La.) Na kwa sababu ya ujinga wa mwanadamu, walishawishiwa kwa urahisi na maneno ya nyoka, walishikwa kwa urahisi, waliongozwa kwa urahisi. Hivyo uliweza kuona nia za Shetani? Uliweza kuona madhumuni nyuma ya kile alichosema? Uliweza kuona njama na mpango wake wa ujanja? (La.) Ni aina gani ya tabia inayowakilishwa na njia ya mazungumzo ya Shetani? Ni aina gani ya kiini ulichoona ndani ya Shetani kupitia maneno haya? (Uovu.) Uovu. Je, ni mwenye kudhuru kwa siri? Pengine juujuu anakupa tabasamu ama kutofichua maonyesho yoyote. Lakini katika moyo wake anahesabu jinsi ya kufikia lengo lake, na ni lengo hili ambalo huwezi kuliona. Kisha unashawishiwa na ahadi zote anazokupa, manufaa yote anayozungumzia. Unayaona kuwa mazuri, na unahisi kwamba kile anachosema ni cha kufaa zaidi, kikubwa zaidi kuliko asemacho Mungu. Wakati haya yanafanyika, je, mwanadamu basi hawi mfungwa mtiifu? (Ndiyo.) Basi mbinu hizi zinazotumiwa na Shetani si za kikatili? Unafanywa kuzama chini. Bila kusongeza kidole, kwa sentensi hizi mbili unafanywa kumfuata, kufanywa kumtii. Lengo lake limefikiwa. Sivyo? (Ndiyo.) Nia hii si ya husuda? Huu sio uso wa kimsingi kabisa wa Shetani? (Ndiyo.) Kutoka kwa maneno ya Shetani, mwanadamu ameona nia zake za husuda, ameona uso wake wenye sura mbaya na kiini chake. Sivyo? (Ndiyo.) Kwa kulinganisha sentensi hizi, bila uchambuzi pengine unaweza kuhisi kana kwamba maneno ya Yehovah ni ya kuchusha, ya kawaida na ya wote, kwamba hayastahili kuhangaikiwa kuusifu uaminifu wa Mungu. Tunapochukuwa maneno ya Shetani na uso wake wenye sura mbaya na kuvitumia kama foili[a] , hata hivyo, je, haya maneno ya Mungu yanabeba uzito mwingi kwa watu wa leo? (Ndiyo.) Kupitia foili[a] hii, mwanadamu anaweza kuhisi kutokuwa na dosari kwa Mungu. Niko sahihi Nikisema hivi? (Ndiyo.) Kila neno analosema Shetani pamoja na nia zake, malengo yake na jinsi anavyoongea—yote yamepotoshwa. Ni nini sifa muhimu ya njia yake ya kuzungumza? Anatumia maneno yasiyo dhahiri kukushawishi bila kukuruhusu kumwona, wala hakuruhusu kutambua lengo lake ni nini; anakuacha uchukue chambo, akikufanya umsifu na kuimba uzuri wake. Sivyo ilivyo? (Ndiyo.) Hii siyo hila ya daima ya Shetani? (Ndiyo.) Hebu sasa tuangalie maneno na maonyesho mengine ya Shetani yanayomruhusu mwanadamu kuona uso wake wenye sura mbaya. Hebu tuendelee kusoma baadhi ya maandiko.
3. Mazungumzo kati ya Shetani na Yehova Mungu
(Ayu 1:6-11) Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao. BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha BWANA bure? Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.
(Job 2:1-5) Tena kulikuwa na siku hao wana wa Mungu walipokwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao, ili kujihudhurisha mbele za BWANA. BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi? Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea juu yake, ili nimwangamize pasipokuwa na sababu. Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele za uso wako.
Vifungu hivi viwili ni mazungumzo kati ya Mungu na Shetani, na vinarekodi kile alichosema Mungu na kile alichosema Shetani. Je, Mungu alisema mengi sana? (La.) Hakuzungumza sana, na Aliongea kwa urahisi sana. Tunaweza kuona utakatifu wa Mungu katika maneno rahisi ya Mungu? Wengine watasema “Hii si rahisi.” Hivyo tunaweza kuona ubaya wa shetani katika majibu yake? (Ndiyo.) Basi kwanza wacha tuangalie ni aina gani ya swali ambalo Yehova Mungu alimwuliza Shetani. “Umetoka wapi wewe?” Hili ni swali linaloeleweka kwa urahisi? (Ndiyo.) Kuna maana iliyofichwa? (La.) Ni swali tu, safi, bila madhumuni mengine. Kama Ningekuuliza: “Unatoka wapi wewe?” mngejibu vipi? Ni swali gumu kujibu? Mngesema: “Natoka katika kuzunguka-zunguka, na katika kutembea huku na huku?” (La.) Hamngejibu namna hii, kwa hivyo mnahisi aje mnapomwona Shetani akijibu kwa njia hii? (Tunahisi kwamba Shetani ni mpumbavu na mjanja.) Mnahisi hivi? Unaweza kusema ni nini Ninachohisi? Kila wakati Ninapoona maneno haya Nahisi kuchukizwa. Mnahisi kuchukizwa? (Ndiyo.) Mbona kuchukizwa? Kwa sababu anazungumza bila kusema lolote! Alijibu swali la Mungu? (La.) Mbona? Maneno yake hayakuwa jibu, hayakuwa na matokeo yoyote, siyo? Hayakuwa jibu lililoelekezwa kwa swali la Mungu. “Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.” Niambie, unayaelewa maneno haya? Unayaelewa? Kwa hivyo Shetani ametoka wapi duniani? Mmepata jibu kuhusu wapi ametoka? (La.) Hii ndiyo “akili” ya ujanja wa Shetani, kutomwacha yeyote kujua anachosema. Baada ya kuyasikia maneno haya, bado huwezi kutambua ni nini amesema, ilhali amemaliza kujibu. Pengine anaamini kwamba amejibu vizuri sana. Basi unahisi vipi? Kuchukizwa? (Ndiyo.) Kuchukizwa, siyo? Sasa unaanza kuhisi chukizo na maneno haya, Shetani haongei moja kwa moja, kukufanya kutoweza kutambua akili yake ama chanzo cha maneno yake. Anazungumza kimakusudi, kwa ujanja, na anatawaliwa na kiini chake mwenyewe, asili yake. Shetani hakuzingatia maneno haya kwa muda mrefu; aliyaeleza kiasili. Punde tu unapomwuliza mahali ametoka, anatumia maneno haya kukujibu. “Ametoka wapi duniani? Unahisi kuchanganyikiwa, bila kujua ametoka wapi. Kuna wowote kati yenu wanaozungumza hivi? (Ndiyo.) Hii ni njia ya aina gani ya kuzungumza? (Si dhahiri na haina jibu la uhakika.) Tunapaswa kutumia aina gani ya maneno kuelezea namna hii ya kuzungumza? Ni ya kupotosha na kudanganya, siyo? Watu wengine huzungumza namna hii. Unauliza mtu: “Nilikuona jana. Ulikuwa unaelekea wapi? Hawakujibu moja kwa moja kusema mahali walienda jana. Wanasema “Jana ilikuwa siku kweli. Nimechoka sana!” Je, walijibu swali lako? Hilo si jibu ulilokuwa unataka, ni kweli? Hii ni “akili” ya ujanja wa mwanadamu. Huwezi kugundua wanachomaanisha ama kutambua chanzo ama nia nyuma ya maneno yao. Hujui mioyo yao kwa sababu ndani ya mioyo yao wanayo hadithi yao wenyewe—hii ni yenye kudhuru kwa siri. Je, ninyi pia huongea hivi mara nyingi? (Ndiyo.) Basi madhumuni yenu ni yapi? Je, huwa ni kulinda maslahi yenu wakati mwingine, kudumisha nafasi yenu wakati mwingine, taswira yenu, kuweka siri za maisha yenu ya kibinafsi, kuokoa sifa zenu binafsi? Licha ya madhumuni, hayatenganishwi na maslahi yenu, yanahusiana na maslahi yenu, sivyo? Hii ni asili ya mwanadamu? (Ndiyo.) Hivyo si kila mtu aliye na asili ya aina hii ni kama Shetani? Tunaweza kusema hivi, sivyo? Kuzungumza kwa ujumla, huu udhihirisho ni wenye makuruhu na wa kusinya. Mnahisi pia sasa kuchukizwa, sivyo? (Ndiyo.) Hii inawakilisha ujanja na uovu wa Shetani.
Tukiangalia tena kifungu cha kwanza, Shetani anamjibu tena Yehova, akisema: “Je! Huyo Ayubu yuamcha BWANA bure?” Anaanza kushambulia tathmini ya Yehova ya Ayubu, na shambulio hili linapakwa rangi na uhasama. “Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo?” Huu ndio utambulisho na tathmini ya Shetani ya kazi ya Yehova kwa Ayubu. Shetani anaitathmini hivi, akisema: “Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.” Shetani huongea kwa utata kila mara, lakini hapa anaongea kwa uhakika. Maneno haya yaliyozungumzwa kwa uhakika ni shambulio, ni kufuru na ni upinzani kwa Yehova Mungu, kwa Mungu Mwenyewe. Mnahisi vipi mnapomsikia? Mnahisi chuki? (Ndiyo.) Mnaweza kuona nia zake? Kwanza kabisa, anakataa kabisa tathmini ya Yehova ya Ayubu—yule anayemwogopa Mungu na kuepuka maovu. Kisha anakataa kabisa kila kitu anachosema na kufanya Ayubu kwa kumcha Yehova. Je, yeye anashitaki? Shetani anashitaki, anakataa na anashuku kila anachofanya na kusema Yehova. Haamini, akisema “Ukisema mambo yako namna hii, mbona sijaiona? Umempa baraka nyingi, anawezaje kukosa kukucha?” Je, huku si kukataa kabisa kila anachofanya Mungu? Kushitaki, kukataa, kufuru—maneno yake si ya ugomvi? Ni maonyesho ya ukweli ya kile anachofikiria Shetani ndani ya moyo wake? (Ndiyo.) Haya maneno hakika si sawa na maneno tuliyoyasoma hivi sasa: “katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. Ni tofauti sana na hayo. Kupitia maneno haya, Shetani anaweka wazi mtazamo wake kwa Mungu na kuchukizwa na kumcha Mungu kwa Ayubu ambako kuko katika moyo wake. Haya yakifanyika, ubaya wake na asili yake mbovu inafichuliwa kabisa. Anawachukia wale wanaomcha Mungu, anawachukia wale wanaoepukana na maovu, na hata zaidi anamchukia Yehova kwa sababu ya kumpa mwanadamu baraka. Anataka kutumia fursa hii kumwangamiza Ayubu ambaye Mungu
alimwinua na mkono Wake mwenyewe, kumtilifisha, akisema: “Unasema Ayubu anakuogopa na kuepukana na maovu. Naiona vingine.” Anatumia mbinu mbalimbali kumchochea na kumjaribu Yehova, na kutumia mbinu mbalimbali ili Yehova Mungu amkabidhi Ayubu kwa Shetani ili atawaliwe, adhuriwe na ashughulikiwe kwa ukatili. Anataka kutumia fursa hii ili kumwangamiza mtu huyu ambaye ni mwenye haki na mtimilifu katika macho ya Mungu. Yeye kuwa na moyo wa aina hii ni msukumo wa muda mfupi? La, siyo. Imekuwa ikiundwa kwa muda mrefu. Mungu anafanya kazi, Mungu anamtunza mtu, anamwangalia mtu, na Shetani anafuata hatua Yake yote. Yeyote anayefadhiliwa na Mungu, Shetani pia anatazama, akifuata nyuma. Iwapo Mungu anamtaka mtu huyu, Shetani atafanya kila kitu kwa uwezo wake kumzuia Mungu, akitumia mbinu mbalimbali mbovu kujaribu, kusumbua na kuharibu kazi anayofanya Mungu ili kufikia lengo lake lililofichwa. Lengo lake ni nini? Hataki Mungu awe na mtu yeyote; anataka wale wote ambao Mungu anataka, kuwamiliki, kuwatawala, kuwaelekeza ili wamwabudu, ili watende maovu pamoja naye. Je, hii siyo nia ya husuda ya Shetani? Kwa kawaida, ninyi husema mara nyingi kwamba Shetani ni mwovu sana, mbaya sana, lakini umemwona? Mnaweza kuona tu jinsi ambavyo mwanadamu ni mbaya na hamjaona kwa uhakika jinsi ambavyo Shetani ni mbaya sana. Lakini mmemwona kwa hili swala linalohusiana na Ayubu? (Ndiyo.) Swala hili limeufanya uso wenye sura mbaya wa Shetani na kiini chake kuwa wazi kabisa. Shetani ako vitani na Mungu, akifuata nyuma Yake. Lengo lake ni kubomoa kazi yote ambayo Mungu anataka Kufanya, kuwamiliki na kudhibiti wale wote ambao Mungu anawataka, kuwafisha kabisa wale ambao Mungu anataka. Kama hawajafishwa, basi wanakuja kwa milki ya Shetani kutumiwa naye—hili ndilo lengo lake. Na Mungu anafanya nini? Mungu anasema tu sentensi rahisi katika kifungu hiki; hakuna rekodi ya chochote zaidi ambacho Mungu anafanya, lakini tunaona kwamba kuna rekodi nyingi zaidi za kile ambacho Shetani anafanya na kusema. Katika kifungu cha maandishi hapa chini, Yehova alimwuliza Shetani, “Umetoka wapi wewe?” Jibu la Shetani ni nini? (Bado ni “Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.”) Bado ni sentensi hiyo. Niambieni, imekuwaje wito wa Shetani, kazi ya Shetani ya ujuzi wa juu? Si Shetani ni wa kuchukia? Kusema sentensi hii inayochafua moyo mara moja inatosha. Kwa nini Shetani daima anarejelea Sentensi hii? Hii inadhihirisha kitu kimoja: asili ya Shetani haibadiliki. Uso wake wenye sura mbaya si kitu anachoweza kuficha kwa muda mrefu. Mungu anamwuliza swali na anajibu kwa njia kama hiyo, sembuse anavyotendea watu! Hamwogopi Mungu, hamchi Mungu, na hamtii Mungu. Hivyo anathubutu kuwa na kiburi isiyo na maadili mbele ya Mungu, kutumia haya maneno ili kujaribu kuficha kwa maswali ya Mungu, kutumia jibu hili moja kujibu swali la Mungu, kujaribu kutumia jibu hili kumshangaza Mungu—huu ndio uso usiopendeza wa Shetani. Haamini uweza wa Mungu, haamini mamlaka ya Mungu, na hakika hayuko tayari kutii kutawaliwa na Mungu. Daima anampinga Mungu, daima anashambulia yote anayofanya Mungu, akijaribu kuharibu yote anayofanya Mungu—hili ndilo lengo lake ovu.
Katika mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka elfu sita, hasa katika kitabu cha Ayubu, vifungu hivi viwili ambavyo Shetani anasema na mambo ambayo Shetani anafanya yanawakilisha upinzani wake kwa Mungu. Tunaweza kusema hivi? (Ndiyo.) Huyu ni Shetani akidhihirisha alivyo kwa kweli. Umeyaona matendo ya Shetani katika maisha tunayoishi sasa? Utakapoyaona, unaweza kutoyafikiria kuwa vitu vilivyoongelewa na Shetani, lakini badala yake kuyafikiria kuwa vitu vilivyoongelewa na mwanadamu, siyo? Kipi kilichowakilishwa, wakati mambo kama hayo yanazungumzwa na mwanadamu? Shetani anawakilishwa? Hata kama utamtambua, bado huwezi kuona kwamba ukweli yanazungumzwa na Shetani. Lakini hapa na sasa umeona bila shaka kile ambacho Shetani mwenyewe amesema. Sasa una uelewa usio na shaka na ulio wazi kabisa wa uso wenye sura mbaya na uovu wa Shetani. Hivyo hivi vifungu viwili vilivyozungumzwa na Shetani ni vya thamani kwa watu wa leo kuweza kutambua asili ya Shetani? Hivi vifungu viwili vinastahili kukusanywa ili binadamu leo aweze kutambua uso wenye sura mbaya wa Shetani, kutambua uso wa asili na wa kweli wa Shetani? Ingawa kusema jambo hili hakuonekani kufaa sana, kulieleza kwa njia hii bado kunaweza kuchukuliwa kuwa sahihi. Naweza tu kuliweka kwa njia hii na iwapo mnalielewa, basi imetosha. Tena na tena, Shetani anayashambulia mambo ambayo Yehova anafanya, akitoa mashtaka kuhusu kumcha Yehova Mungu kwa Ayubu. Anajaribu kumchochea Yehova kwa kutumia mbinu mbalimbali, kumfanya Yehova kumkubali kumjaribu Ayubu. Maneno yake basi yanachochea sana. Basi Niambieni, baada ya Shetani kuzungumza maneno haya, Mungu anaweza kuona wazi kile ambacho Shetani anataka kufanya? (Ndiyo.) Je, Mungu anaelewa kile anataka kufanya? (Ndiyo.) Katika moyo wa Mungu, huyu mtu Ayubu ambaye Mungu anamwangalia—huyu mtumishi wa Mungu, ambaye Mungu anamchukulia kuwa mwenye haki, mtu mtimilifu—Ayubu anaweza kuyahimili majaribio ya aina hii? (Ndiyo.) Kwa nini Mungu anasema “ndiyo” kwa uhakika kama huo? Mungu huchunguza mioyo ya binadamu daima? (Ndiyo.) Kwa hivyo Shetani anaweza kuchunguza mioyo ya binadamu? (La.) Shetani hawezi. Hata kama Shetani anaweza kuona kwamba mwanadamu ana moyo unaomcha Mungu, asili yake mbovu haiwezi kuamini kwamba utakatifu ni utakatifu, ama kwamba uchafu ni uchafu. Shetani mwovu hawezi kuthamini chochote kilicho takatifu, chenye haki ama chenye kung’aa. Shetani hawezi kuepuka kuumiza kwa kutenda kupitia asili yake, uovu wake, na kupitia mbinu hizi anazotumia. Hata kwa hatari ya yeye kuadhibiwa na kuangamizwa na Mungu, hasiti kumpinga Mungu kwa ukaidi—huu ni uovu, hii ni asili ya Shetani. Kwa hivyo katika kifungu hiki, Shetani anasema: “Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele za uso wako.” Anafikiria nini? Kumcha Mungu kwa mwanadamu ni kwa sababu mwanadamu amepata manufaa mengi kutoka kwa Mungu. Mwanadamu hupata manufaa mengi kutoka kwa Mungu, kwa hivyo wanasema Mungu ni mwema. Lakini si kwa sababu Mungu ni mwema, ni kwa sababu tu mwanadamu amepata manufaa mengi na hivyo anaweza kumcha Mungu kwa njia hii: Punde unapomnyima manufaa haya, basi anaachana na wewe. Katika asili yake mbovu, Shetani haamini kwamba moyo wa mwanadamu kwa kweli unaweza kumcha Mungu. Mbona? Kwa sababu ya asili yake mbovu hajui utakatifu ni nini, na hata chini zaidi hajui heshima ya kuogopa ni nini. Hajui ni nini kumtii Mungu, ni nini kumcha Mungu. Kwa sababu yeye mwenyewe hamchi Mungu, anafikiri, “Mwanadamu pia hawezi kumcha Mungu. Haiwezekani.” Sivyo? (Ndiyo.) Niambieni, si Shetani ni mwovu? (Ndiyo!) Shetani ni mwovu. Hivyo, isipokuwa kanisa letu, yawe ni makundi na madhehebu mbalimbali, ama makundi ya kidini na ya kijamii, hawaamini uwepo wa Mungu, hawaamini kwamba Mungu anaweza kufanya kazi na hawaamini kwamba kuna Mungu, hivyo wanafikiri, “Kile unachoamini si Mungu pia.” Chukua mfano wa mwanamume mzinzi. Anaangalia na kuona kila mtu mwengine akiwa mzinzi, kama alivyo yeye. Mwanadamu anayedanganya kila wakati anaangalia na kuona hakuna mtu mwanimifu, anawaona wote wakidanganya. Mtu mwovu anawaona watu wote wakiwa waovu na anataka kupigana na kila mtu anayemwona. Wale watu walio na uaminifu kidogo wanawaona wote kuwa waaminifu, na hivyo daima wanalaghaiwa, wanadanganywa, na hakuna wanachoweza kufanya kuhusu hilo. Si hii ni sahihi? Nasema mifano hii michache ili kuwafanya kuwa na uhakika zaidi: asili mbovu ya Shetani si msukumo wa muda mfupi ama kitu kinachosababishwa na mazingira yake, wala si udhihirisho wa muda ulioletwa na sababu yoyote ama usuli wowote. Sivyo kabisa! Hana namna ila kuwa hivyo! Hawezi kufanya chochote chema! Hata anaposema kitu kinachofurahisha kusikia, anakushawishi tu. Kadiri maneno yake yanavyofurahisha, yenye busara zaidi, uungwana zaidi, ndivyo nia zake za husuda zinakuwa za kijicho zaidi nyuma ya maneno haya. Umeona Shetani akiwa na uso na asili ya aina gani katika vifungu hivi viwili? (Ya kudhuru kwa siri, yenye kijicho, na mbovu.) Tabia yake ya msingi ni mbovu, hasa mbovu na yenye kijicho; yenye kijicho na mbovu.
Kwa sababu sasa tumemaliza kuzungumza kuhusu Shetani, hebu turudie kuzungumza kuhusu Mungu wetu. Wakati wa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita wa Mungu, matamshi machache sana ya moja kwa moja ya Mungu yamerekodiwa katika Biblia, na yale yaliyorekodiwa ni rahisi sana. Hivyo wacha tuanzie mwanzoni. Mungu alimuumba mwanadamu na tangu hapo kamwe Ameongoza maisha ya binadamu. Iwe kwa kuwapa wanadamu baraka, kuwapa sheria na amri Zake, ama kuweka masharti kanuni mbalimbali za maisha, mnajua lengo analonuia Mungu kwa kufanya mambo haya ni nini? Kwanza, mnaweza kusema kwa uhakika kwamba yote anayofanya Mungu ni kwa wema wa binadamu? (Ndiyo, tunaweza.) Mnaweza kufikiria kwamba sentensi hii kwa kulinganishwa ni pana na tupu, lakini kuzungumza hasa, kila kitu anachofanya Mungu ni cha kumwongoza na kumwelekeza mwanadamu kuishi maisha ya kawaida. Iwe ili mwanadamu ahifadhi kanuni Zake ama ahifadhi sheria Zake, lengo la Mungu ni kwa mwanadamu kutomwabudu Shetani, kutodhuriwa na Shetani; hii ndiyo ya msingi sana, na hii ndiyo ilifanywa mwanzoni. Mwanzoni kabisa, wakati mwanadamu hakuelewa mapenzi ya Mungu, Alichukuwa baadhi ya sheria na kanuni rahisi na kuweka kauli zilizoshughulikia masuala yote yanayoweza kufikiriwa. Kauli hizi ni rahisi sana, lakini ndani yake kuna mapenzi ya Mungu. Mungu anamthamini, Anamtunza na kwa hakika Anampenda mwanadamu. Sivyo? (Ndiyo.) Kwa hivyo tunaweza kusema kwamba moyo Wake ni mtakatifu? Tunaweza kusema kwamba moyo wake ni safi? (Ndiyo.) Je, Mungu anazo nia zilizofichwa? (La.) Kwa hivyo hili lengo Lake ni sahihi na halisi? (Ndiyo.) Ni halisi. Licha ya kauli alizoweka Mungu, athari zake katika kazi Yake yote ni halisi kwa mwanadamu, na zinaongoza njia. Kwa hivyo kuna fikira zozote za kibinafsi kwa akili ya Mungu? Je, Mungu anayo malengo zaidi kuhusiana na mwanadamu, ama Anataka kumtumia mwanadamu kwa jinsi fulani? Sivyo hata kidogo. Mungu anafanya Asemavyo, na pia Anafikiria namna hii kwa moyo Wake. Hakuna mchanganyiko wa madhumuni, hakuna fikira za kibinafsi. Hajifanyii chochote, lakini Anamfanyia mwanadamu kila kitu kabisa, bila malengo ya kibinafsi. Ingawa Ana mipango na nia kwa mwanadamu, Hajifanyii chochote. Kila kitu Anachofanya kinafanyiwa mwanadamu tu, kumlinda mwanadamu, kumhifadhi mwanadamu dhidi ya kupotezwa. Hivyo si moyo huu ni wenye thamani? (Ndiyo.) Unaweza kuona dokezo hata kidogo zaidi la huu moyo wenye thamani kwa Shetani? (La.) Mnaweza kuliona? Mnaweza? Hatuwezi kuliona dokezo moja la moyo huu kwa Shetani. Kila kitu anachofanya Mungu kinafichuliwa kiasili. Kwa kuangalia njia Mungu anafanya kazi, Anafanyaje kazi? Je, Mungu anazichukua sheria hizi na maneno Yake na kuyafunga pamoja kwa kukaza katika kichwa cha kila mtu kama fingo la pete ya dhahabu,[b]Akizilazimisha kwa kila mtu? Je, Anafanya kazi namna hii? (La.) Kwa hivyo Mungu anafanya kazi Yake namna gani? (Anatuongoza.) Haya, hiki ni kipengele kimoja. Kuna vingine? Mungu anawafanyia kazi kwa njia nyingi, inaweza kuwaje mmekosa vitu vya kusema baada ya moja tu? (Anashauri na kutia moyo.) Kuna kipengele cha pili. Vingine zaidi? Je, Anatishia? Je, Anawazungumzia kwa njia inayochanganya? (La.) Wakati huelewi ukweli, Mungu hukuongoza vipi? (Yeye huangaza mwangaza.) Haya, Anaangaza mwangaza kwako, akikwambia wazi kwamba haya hayaambatani na ukweli, na kile unachofaa kufanya. Kwa hivyo kutoka kwa njia hizi ambazo Mungu anafanya kazi, unahisi kwamba una uhusiano wa aina gani na Mungu? Zinakufanya uhisi kwamba Mungu yuko mbali na ufahamu wako? (La.) Hivyo zinakufanya uhisi vipi? Mungu ako hasa karibu na wewe, hakuna umbali kati yenu. Wakati Mungu anakuongoza, Anapokukimu, Anapokusaidia na kukutunza, unahisi urafiki wa Mungu, kuheshimika Kwake, unahisi jinsi Anavyopendeza, jinsi Alivyo mwema. Lakini wakati Mungu anaposhutumu upotovu wako, ama Anapokuhukumu na kukufundisha nidhamu kwa sababu ya kuasi dhidi Yake, Mungu anatumia njia gani? Anakushutumu kwa kutumia maneno? (Ndiyo.) Anakufundisha nidhamu kupitia mazingira yako na kupitia watu, masuala na mambo? (Ndiyo.) Kwa hivyo nidhamu hii imefika kiwango kipi? (Kwa kiwango ambacho mwanadamu anaweza kuvumilia.) Kiwango Chake cha nidhamu kinafikia mahali sawa ambapo Shetani anamdhuru mwanadamu? (La.) Mungu anafanya kazi kwa njia ya upole, upendo, laini na ya kujali, kwa njia hasa iliyopimwa na ni sahihi. Njia Yake haikufanyi kuhisi hisia kali, ukisema, “Mungu hawezi kuniacha nifanye hivi” ama “Lazima Mungu aniache nifanye vile.” Mungu kamwe hakupi mawazo ya aina hiyo ama hisia kali zinazofanya mambo kutovumilika. Sivyo ilivyo? (Ndiyo.) Hata unapoyakubali maneno ya Mungu ya hukumu na kuadibu, unahisi vipi basi? Unapohisi mamlaka ya Mungu na nguvu ya Mungu, unahisi vipi basi? Unahisi uungu wa Mungu usiokosewa? (Ndiyo.) Unahisi ukiwa mbali na Mungu nyakati hizi? Unahisi kutishiwa na Mungu? (La.) Badala yake, unahisi heshima inayomcha Mungu. Je, watu wanahisi haya mambo yote kwa sababu tu ya kazi ya Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo wangekuwa na hisia hizi iwapo Shetani angefanya kazi kwa mwanadamu? (La.) Mungu anatumia maneno Yake, ukweli Wake na uhai Wake kuendelea bila kusita kumtolea mwanadamu, kumtunza mwanadamu. Wakati mwanadamu ni mnyonge, wakati mwanadamu anahisi huzuni, Mungu kwa hakika hazungumzi kwa ukali, akisema, “Usihisi huzuni. Mbona unahisi huzuni? Kwa nini uwe mnyonge? Kuna nini ya kuwa mnyonge kuihusu? Wewe ni mnyonge sana, unaweza hata kufa. Daima una huzuni, kuna haja gani ya kuishi? Kufa tu!” Je, Mungu anafanya kazi hivi? (La.) Je, Mungu ana mamlaka ya kutenda namna hii? (Ndiyo.) Lakini Mungu anatenda namna hii? (La.) Mungu hatendi hivi kwa sababu ya kiini Chake, kiini cha utakatifu wa Mungu. Upendo Wake kwa mwanadamu, kuthamini na utunzaji Wake wa mwanadamu haviwezi kuelezwa wazi kwa sentensi moja au mbili. Si kitu kinacholetwa na kujisifu kwa binadamu lakini ni kitu kinacholetwa kwa vitendo halisi; ni ufunuo wa kiini cha Mungu. Je, hizi njia zote ambazo Mungu anafanya kazi zinaweza kumruhusu mwanadamu kuona utakatifu wa Mungu? Kwa hizi njia zote ambazo Mungu anafanya kazi, zikiwemo nia nzuri za Mungu, zikiwemo athari ambazo Mungu anataka kutimiza kwa mwanadamu, zikiwemo njia mbalimbali Mungu anatumia kufanya kazi kwa mwanadamu, aina ya kazi Anayofanya, kile Anachotaka mwanadamu kuelewa—umeona uovu ama ujanja wowote katika nia nzuri za Mungu? (La.) Huwezi kuona uovu wowote, unaweza? (La.) Hivyo, kwa kila kitu Mungu anafanya, kila kitu Mungu anasema, kila kitu anachofikiria katika moyo Wake, na pia kiini chote cha Mungu anachofichua—tunaweza kumwita Mungu mtakatifu? (Ndiyo.) Mwanadamu yeyote amewahi kuona utakatifu huu duniani, ama kwake mwenyewe? Mbali na Mungu, umewahi kuuona kwa mtu yeyote ama kwa Shetani? (La.) Kutoka kwa yale tuliyoyazungumzia hadi sasa, tunaweza kumwita Mungu wa kipekee, Mungu mtakatifu Mwenyewe? (Ndiyo.) Yote ambayo Mungu anampa mwanadamu, yakiwemo maneno ya Mungu, njia tofauti ambazo Mungu anafanya kazi kwa mwanadamu, kile ambacho Mungu anamwambia mwanadamu, kile ambacho Mungu anamkumbusha mwanadamu kuhusu, kile ambacho Anashauri na kutia moyo, vyote vimetoka kwa kiini kimoja: Vyote vimetoka kwa utakatifu wa Mungu. Iwapo hakungekuwa na Mungu mtakatifu kama huyu, hakuna mwanadamu ambaye angechukua nafasi Yake kufanya kazi Anayofanya. Iwapo Mungu angewachukua watu hawa na kuwakabidhi kabisa kwa Shetani, mmewahi kufikiria nyinyi mlio hapa leo mngekuwa katika hali gani? Nyinyi nyote mngekuwa mmeketi hapa? Kamili na wasioharibika? (La.) Kwa hivyo mgekuwa vipi? Pia mngesema: “Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.”? Mngejitamba hivyo, kutokuwa na haya kabisa na kujigamba bila haya mbele ya Mungu, na kuzungumza kwa njia isiyo ya moja kwa moja? (Ndiyo.) Ndiyo, mngeweza. Mngeweza kwa asilimia mia moja! Mngeweza kabisa! Mtazamo wa Shetani kwa mwanadamu unawaruhusu kuona kwamba asili ya Shetani ni tofauti kabisa na ya Mungu. Kiini chake ni tofauti kabisa na cha Mungu. Kiini kipi cha Shetani ni kinyume cha utakatifu wa Mungu? (Uovu wake.) Asili ya uovu ya Shetani ni kinyume na utakatifu wa Mungu. Watu wengi zaidi hawatambui kwamba maonyesho haya ya Mungu yanawakilisha kiini cha utakatifu wa Mungu ni kabisa kwa sababu wanamilikiwa na Shetani, ndani ya upotovu wa Shetani, ndani ya boma anamoishi Shetani. Hawajui utakatifu ni nini ama jinsi ya kufafanua utakatifu. Hata unapoona utakatifu wa Mungu, bado huwezi kuufafanua kuwa utakatifu wa Mungu kwa uhakika wowote. Hii ni tofauti katika utambulisho wa mwanadamu wa utakatifu wa Mungu.
Ni sifa ya uwakilishi gani inaonyeshwa na kazi ya Shetani kwa mwanadamu? Mnapaswa kujua kuhusu hii kutokana na uzoefu wenu wenyewe—sifa ya uwakilishi zaidi ya Shetani, kitu ambacho anafanya zaidi, kitu ambacho anajaribu kufanya na kila mtu. Ana sifa ambayo pengine hamwezi kuona, ili msiweze kufikiria jinsi Shetani anatisha na wa kuchukia. Kuna mtu anayejua sifa hii ni nini? Niambieni. (Kila kitu anachofanya kinafanywa kumdhuru mwanadamu.) Anafanya vitu kumdhuru mwanadamu. Anamdhuru mwanadamu vipi? Mnaweza kunionyesha hasa zaidi na kwa kina? (Anamshawishi, anamlaghai na kumjaribu mwanadamu.) Hii ni sahihi, hii inaonyesha vipengele vingi. Kuna vingine? (Anamdanganya mwanadamu.) Anadanganya, anashambulia na anatuhumu. Ndiyo, haya yote. Kuna mengine zaidi? (Anasema uwongo.) Udanganyifu na uongo hujitokeza kiasili kabisa kwa Shetani, Anafanya hivi mara nyingi hadi uongo unabubujika kutoka kwa mdomo wake bila yeye hata kuhitaji kufikiria. Mengine zaidi? (Anapanda mfarakano.) Hii si muhimu sana. Nitawaelezea kitu ambacho kitawatisha, lakini Sifanyi hivyo ili kuwaogopesha. Mungu anafanya kazi kwa mwanadamu na mwanadamu anathaminiwa katika mtazamo na moyo wa Mungu. Kinyume na hayo, Shetani anamthamini mwanadamu? Hamthamini mwanadamu. Anataka nini na mwanadamu? Anataka kumdhuru mwanadamu, anachofikiria tu ni kumdhuru mwanadamu. Hii si sahihi? Kwa hivyo wakati anafikiria kumdhuru mwanadamu, anafanya hivyo katika hali ya dharura ya akili? (Ndiyo.) Kwa hivyo inapokuja kwa kazi ya Shetani kwa mwanadamu, hapa Nina maneno mawili yanayoweza kuelezea vizuri asili yenye nia mbaya na ovu ya Shetani, yanayoweza kuwaruhusu kujua chuki ya Shetani: Katika mtazamo wa Shetani kwa mwanadamu, daima anataka “kumiliki” na “kujishikiza” kwa nguvu kwa kila mmoja wao ili aweze kufika mahali ambapo anaweza kumdhibiti mwanadamu kabisa, kumdhuru mwanadamu, ili aweze kutimiza lengo hili na tamaa isiyowezekana. “Umiliki wa nguvu” unamaanisha nini? Unafanyika na kibali chako, ama bila kibali chako? Unafanyika na kujua kwako, ama bila kujua kwako? Ni bila kujua kwako kabisa! Katika hali ambazo huna ufahamu, pengine wakati hajasema chochote ama pengine wakati hajafanya chochote, wakati hakuna kauli kigezo, hakuna muktadha, yuko hapo karibu nawe, akikuzunguka. Anatafuta fursa ya kukunyonya, kisha anakumiliki kwa nguvu, anajishikiza kwako, kutimiza lengo lake la kukudhibiti kikamilifu na kukudhuru. Hii ni nia na tabia ya kawaida zaidi katika mapambano ya Shetani dhidi ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Mnahisi vipi mnaposikia haya? (Tuna hofu na woga katika mioyo yetu.) Mnahisi kuchukizwa? (Ndiyo, tunahisi kuchukizwa.) Basi mnapohisi kuchukizwa, mnafikiria Shetani hana haya? (Ndiyo.) Mnapofikiria Shetani hana haya, mnahisi kuchukizwa na wale watu walio karibu nanyi ambao daima wanataka kuwatawala, wale walio na matarajio yasiyowezekana ya hadhi na maslahi yao? (Ndiyo.) Hivyo ni mbinu gani anazotumia Shetani kujishikiza kwa nguvu kwa na kummiliki mwanadamu? Mnaelewa hii vizuri? Mnapoyasikia maneno haya mawili ya “umiliki” na “kushikiza” kwa nguvu, mnapata hii hisia ya ugeni na unyarafu, sivyo? Je, mnapata kionjo cha ladha yao mbovu? Bila kibali ama maarifa yako anajishikiza kwako, anakumiliki na kukupotosha. Unaweza kuonja nini kwa moyo wako? Chuki (Ndiyo!) Unyarafu? (Ndiyo!) Kwa hivyo wakati unahisi hii chuki na unyarafu kwa njia hii ya Shetani, una hisia gani kwa Mungu? (Kushukuru.) Kushukuru Mungu kwa kukuokoa. Kwa hivyo sasa, wakati huu, unayo hamu ama matakwa ya kumwacha Mungu kuongoza yako yote, kutawala yako yote? (Ndiyo.) Kwa muktadha upi? Unasema ndiyo kwa sababu unaogopa kumilikiwa kwa nguvu na kushikizwa na Shetani? Huwezi kuwa na mawazo kama haya, siyo sahihi. Usiwe na hofu, Mungu yuko hapa. Hakuna chochote cha kuhofia, siyo? Ukishaelewa asili mbovu ya Shetani, unapaswa kuwa na uelewa sahihi zaidi ama upendo wa kina wa mapenzi ya Mungu, nia nzuri za Mungu, huruma ya Mungu na msamaha kwa mwanadamu na tabia Yake ya haki. Shetani ni wa kuchukia sana, lakini ikiwa hii bado haitii moyo upendo wako kwa Mungu na utegemezi na uaminifu wako kwa Mungu, basi ungekuwa mtu wa aina gani? Uko tayari kumwacha Shetani akudhuru hivyo? Baada ya kuona uovu na ubaya wa Shetani, tunamgeuza na kisha kumwangalia Mungu. Utambulisho wako wa Mungu sasa umepitia mabadiliko yoyote? (Ndiyo.) Mabadiliko ya aina gani? Tunaweza kusema Mungu ni mtakatifu? Tunaweza kusema Mungu hana dosari? (Ndiyo.) “Mungu ni utakatifu wa kipekee”—Mungu anaweza kuvumilia jina hili? (Ndiyo.) Hivyo kwa dunia na miongoni mwa mambo yote, ni Mungu Mwenyewe pekee anayeweza kuvumilia huu uelewa wa mwanadamu? Kuna wengine? (La.) Hivyo, ni nini hasa Mungu anampatia mwanadamu? Je, Anakupa tu utunzaji, wasiwasi na kukutia maanani kidogo wakati huko makini? Mungu amempa nini mwanadamu? Mungu amempa mwanadamu uhai, Amempa mwanadamu kila kitu, na amempa mwanadamu bila masharti bila kudai chochote, bila nia zozote za siri. Anatumia ukweli, Anatumia maneno Yake, Anatumia uhai Wake kumwongoza na kumwelekeza mwanadamu, kumtoa mwanadamu mbali na madhara ya Shetani, mbali na majaribio ya Shetani, mbali na ushawishi wa Shetani na kumruhusu mwanadamu kuona wazi asili mbovu ya Shetani na uso wake unaotisha. Hivyo, upendo na wasiwasi wa Mungu kwa binadamu ni wa kweli? Ni kitu ambacho kila mmoja wenu anaweza kupitia? (Ndiyo.)
Kumbuka maisha yenu hadi sasa kwa yote ambayo Mungu amekufanyia katika miaka yote ya imani yako. Iwapo unaihisi kwa kina au la, haikuwa ya umuhimu sana? Haikuwa kile ulichohitaji zaidi kupata? (Ndiyo.) Huu si ukweli? Huu si uhai? (Ndiyo.) Kwa hivyo Mungu amewahi kukupa nuru kurudisha chochote ama kulipia kitu baada ya Yeye kukupa vitu hivi? (La.) Kwa hivyo madhumuni ya Mungu ni yapi? Mbona Mungu anafanya hivi? Mungu pia ana lengo la kukumiliki? (La.) Je, Mungu anataka kuwa mfalme katika mioyo ya mwanadamu? (Ndiyo.) Kwa hivyo ni nini tofauti kati ya Mungu kuwa mfalme na umiliki wa nguvu wa Shetani? Mungu anataka kupata mioyo ya wanadamu, Anataka kumiliki mioyo ya wanadamu—hii inamaanisha nini? Je, inamaanisha kwamba Mungu anataka mwanadamu kuwa vikaragosi Vyake? Mashine Yake? (La.) Kwa hivyo madhumuni ya Mungu ni nini? Kuna tofauti kati ya Mungu kutaka kumiliki mioyo ya mwanadamu na umiliki wa nguvu wa Shetani, yeye kujishikiza kwa mwanadamu? (Ndiyo.) Tofauti ni nini? Unaweza kuniambia wazi? (Shetani anaifanya kupitia kwa nguvu ilhali Mungu anaacha mwanadamu ajitolee.) Shetani anaifanya kupitia kwa nguvu ilhali Mungu anaacha mwanadamu ajitolee. Hii ndiyo tofauti? Kwa hivyo usipojitolea, nini kitafanyika basi? Usipojitolea, Mungu anafanya chochote? (Anapeana mwongozo na nuru, lakini kama mwishowe mwanadamu hayuko radhi, Hamlazimishi.) Mungu anataka moyo wako kufanyia nini? Na zaidi ya hayo, kwa nini Mungu anataka kukumiliki? Mnaelewa vipi ndani ya mioyo yenu “Mungu anamiliki mioyo ya mwanadamu”? Ni lazima tuwe na haki kwa Mungu hapa, vinginevyo watu daima hawaelewi, wakisema “Mungu daima anataka kunimiliki. Anataka kunimiliki kwa nini? Sitaki kumilikiwa, nataka tu kuwa mimi mwenyewe. Mnasema Shetani anawamiliki watu, lakini Mungu pia anawamiliki watu: Haya si sawa? Sitaki kumwacha yeyote kunimiliki. Mimi ni mimi mwenyewe.” Tofauti hapa ni nini? Chukua dakika kuifikiria. (Nafikiri Mungu anataka kupata mioyo ya mwanadamu na kumiliki mioyo ya mwanadamu ili kumwokoa mwanadamu, kumkamilisha mwanadamu.) Kile unachosema ni lengo la usimamizi wa Mungu wa mwanadamu—kumfanya kuwa kamili. Kwa hivyo unaelewa “miliki” inamaanisha nini hapa? (Inamaanisha kutomwacha Shetani kumiliki mwanadamu. Iwapo Mungu ako katika umiliki, basi Shetani hana njia ya kummiliki mwanadamu.) Unamaanisha Mungu ndiye mmiliki wa kwanza; kama nyumba tupu, yeyote anayeingia wa kwanza anakuwa bwana wa nyumba hiyo. Anayekuja baadaye hawezi kuwa bwana wa nyumba, lakini badala yake anakuwa mtumishi, ama sivyo hawezi kuingia kamwe. Unamaanisha hivi? (Ndiyo, namaanisha kitu kama hiki.) Kuna yeyote aliye na mtazamo tofauti? (Uelewa wangu wa “Mungu kumiliki mioyo ya wanadamu” ni kwamba Mungu anatuchukulia kama familia Yake, kututunza na kutupenda, Shetani anamiliki mioyo ya wanadamu ili kutuvunja, kutudhuru.) Huu ndio uelewa wako wa “Mungu hummiliki wanadamu,” siyo? Kuna uelewa ama maoni tofauti? (Mungu hummiliki wanadamu kwa kutumia neno Lake, kwa matumaini kwamba mwanadamu anaweza kukubali neno la Mungu kwa maisha yake, ili mwanadamu aweze kuishi kulingana na neno la Mungu.) Hii ndiyo maana ya kweli nyuma ya “Mungu hummiliki mwanadamu,” sivyo? Kuna maoni tofauti? (Mtazamo wangu ni kwamba Mungu ni mfano halisi wa ukweli kwa hivyo Mungu anataka kutupa ukweli mzima, na kwa sababu tunapata ukweli huu na tunaletwa chini ya utunzaji na ulinzi Wake, tunaweza basi kuepuka kukutana na mipango ya ujanja ya Shetani na kudhuriwa na yeye. Kuzungumza kwa vitendo, Mungu anataka kupata mioyo ya wanadamu ili mwanadamu aweze kuishi maisha ya kawaida duniani na kupata baraka za Mungu.) Lakini bado hujagusia maana ya ukweli ya “Mungu humiliki mioyo ya wanadamu.” (Kwa asili, mwanadamu aliumbwa na Mungu, kwa hivyo mwanadamu anapaswa kumwabudu na kumrudia. Mwanadamu ni wa Mungu.) Nawauliza, je “Mungu hummiliki mwanadamu” ni kirai tupu? Umiliki wa Mungu wa mwanadamu unamaanisha kwamba Anaishi katika moyo wako? Je, Mungu anatawala kila neno na kusonga kwako? Akikwambia uinue mkono wako wa kushoto, huthubutu kuinua wa kulia? Akikwambia uketi, huthubutu kusimama? Akikwambia uende Mashariki, huthubutu kwenda Magharibi? Je, ni umiliki unaomaanisha kiti kama hiki? (La.) Kwa hivyo ni nini? (Inaamisha kwa mwanadamu kuishi kwa kudhihirisha kile Mungu anacho na alicho.) Mungu amemsimamia mwanadamu katika miaka yote, kwa hivyo kwa kazi ya Mungu kwa mwanadamu hadi sasa kwa hatua hii ya mwisho, maneno yote ambayo Mungu amesema yatakuwa na athari gani kwa mwanadamu? Je, ni kwamba mwanadamu anaishi kulingana na kile anacho Mungu na alicho? Kwa kuangalia maana halisi ya “Mungu humiliki mioyo ya wanadamu,” inaonekana kama Mungu anachukua mioyo ya wanadamu na kuimiliki, Anaishi ndani yake na Hatoki nje tena; Anaishi ndani yake na kuwa bwana wa mioyo ya wanadamu, kutawala na kupanga mioyo ya wanadamu atakavyo, ili mwanadamu lazima aende asemapo Mungu aende. Katika kiwango hiki cha maana, inaonekana ni kama kila mtu alikuwa amekuwa Mungu, amemiliki kiini cha Mungu, amemiliki tabia ya Mungu. Kwa hivyo hapa, mwanadamu pia angeweza kufanya vitendo na matendo ya Mungu? Je, “umiliki” unaweza kuelezewa kwa njia hii? (La.) Kwa hivyo ni nini? (Watu ambao Mungu anataka si vikaragosi, wana fikira na mioyo yao ni hai. Kwa hivyo, umiliki wa Mungu wa wanadamu ni kwa matumaini kwamba mwanadamu anaweza kuwa na fikira na anaweza kuhisi furaha na huzuni ya Mungu; mwanadamu na Mungu wanaathiriana.) Nawauliza hii: Je, maneno na ukweli wote Mungu anampa mwanadamu ni ufunuo wa kiini cha Mungu na kile Anacho na alicho? (Ndiyo.) Hii ni ya uhakika, siyo? Lakini je, maneno yote Mungu anampa mwanadamu ni ya Mungu Mwenyewe kuweka katika vitendo, ya Mungu Mwenyewe kumiliki? Chukua dakika moja kuifikiria? Wakati Mungu anamhukumu mwanadamu, Anafanya hivi kwa sababu ya nini? Maneno haya yalitoka wapi? Ni nini yaliyomo katika maneno haya ambayo Mungu anazungumza Anapomhukumu mwanadamu? Ni nini msingi wake? Msingi wake ni tabia potovu ya mwanadamu? (Ndiyo.) Kwa hivyo athari iliyofikiwa na hukumu ya Mungu ya mwanadamu imetokana na kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo umiliki wa Mungu wa mwanadamu ni kirai tupu? Kwa hakika sicho. Kwa hivyo mbona Mungu anasema maneno haya kwa mwanadamu? Ni nini madhumuni Yake ya kusema maneno haya? Anataka kutumia maneno haya kwa maisha ya mwanadamu? (Ndiyo.) Mungu anataka kutumia ukweli huu wote ambao amezungumza kwa maisha ya mwanadamu. Kwa hivyo wakati mwanadamu anachukua ukweli huu wote na neno la Mungu na kuyabadilisha katika maisha yake, mwanadamu basi anaweza kumtii Mungu? Mwanadamu basi anaweza kumcha Mungu? Mwanadamu basi anaweza kuepuka maovu? Wakati mwanadamu amefika hapa, anaweza basi kutii ukuu na mipango ya Mungu? Mwanadamu sasa ako katika nafasi ya kutii mamlaka ya Mungu? Wakati watu kama Ayubu, ama kama Petro wanafika mwisho wa barabara yao, wakati maisha yao yanaweza kufikiriwa kuwa yamekomaa, wakati wako na uelewa halisi wa Mungu—Shetani bado anaweza kuwapoteza? Shetani bado anaweza kuwamiliki? Shetani bado anaweza kujishikiza kwao kwa nguvu? (La.) Kwa hivyo huyu ni mtu wa aina gani? Huyu ni mtu ambaye amepatwa kabisa na Mungu? (Ndiyo.) Katika kiwango hiki cha maana, unamwonaje mtu huyu ambaye amepatwa kabisa na Mungu? Kwa Mungu, katika hali hii tayari Amemiliki moyo wa mtu huyu. Lakini mtu huyu anahisi nini? Je, ni kwamba neno la Mungu, mamlaka ya Mungu, na njia ya Mungu yamekuwa uhai ndani ya mwanadamu, basi uhai huu unaomiliki utu wote wa mwanadamu unafanya yote anayozidi kutosha, unafanya kiini chake kutosha kumridhisha Mungu? Kwa hivyo kwa Mungu, moyo wa binadamu wakati huu umemilikiwa na Yeye? (Ndiyo.) Mnaelewaje kiwango hiki cha maana sasa? Je, ni Roho wa Mungu anayekumiliki? (La.) Kwa hivyo ni nini hasa kinachokumiliki? (Neno la Mungu.) Haya, neno la Mungu, njia ya Mungu. Ni ukweli na neno la Mungu yanayokuwa maisha yako. Wakati huu, mwanadamu basi ana maisha yanayotoka kwa Mungu, lakini hatuwezi kusema kwamba haya maisha ni maisha ya Mungu. Ni maisha ambayo mwanadamu anapaswa kupata kutoka kwa neno la Mungu. Tunaweza kusema kwamba maisha haya ni maisha ya Mungu? (La.) Hivyo, licha ya muda ambao mwanadamu anamfuata Mungu, licha ya idadi ya maneno ambayo mwanadamu anapata kutoka kwa Mungu, mwanadamu hawezi kuwa Mungu. Hii ni sahihi? (Ndiyo.) Hata kama siku moja Mungu aseme, “Nimemiliki moyo wako, sasa unamiliki maisha Yangu,” utahisi basi kwamba wewe ni Mungu? (La.) Utakuwa nini basi? Hutakuwa na utii kabisa wa Mungu? Mwili na moyo wako hautajawa na maisha Mungu amekupa? Huu ni udhihirisho wa kawaida wakati Mungu anamiliki mioyo ya mwanadamu. Huu ni ukweli. Kwa hivyo kuuangalia kutoka kipengele hiki, mwanadamu anaweza kuwa Mungu? (La.) Wakati mwanadamu amepata maneno yote ya Mungu, wakati mwanadamu anaweza kumcha Mungu na kuepukana na maovu, mwanadamu basi anaweza kumiliki utambulisho wa Mungu? (La.) Mwanadamu anaweza basi kumiliki kiini cha Mungu? (La.) Licha ya kile kitakachofanyika, mwanadamu bado ni mwanadamu wakati yote yamesemwa na kufanywa. Wewe ni kiumbe; wakati umepokea neno la Mungu kutoka kwa Mungu na kupokea njia ya Mungu, unamiliki tu maisha ambayo yanatoka kwa neno la Mungu, na kamwe huwezi kuwa Mungu.
Tukirudia mada yetu hivi sasa, Niliwauliza iwapo Ibrahimu alikuwa mtakatifu ama la. Yeye si mtakatifu, na mnaelewa hii sasa, sivyo? Ayubu ni mtakatifu? (La.) Ndani ya utakatifu huu kuna kiini cha Mungu. Mwanadamu hana kiini cha Mungu ama tabia ya Mungu. Hata wakati mwanadamu amepitia maneno yote ya Mungu na kumiliki kiini cha neno la Mungu, mwanadamu bado hawezi kuitwa mtakatifu; mwanadamu ni mwanadamu. Mnaelewa, sivyo? (Ndiyo.) Kwa hivyo mnakielewaje kirai hiki “Mungu anakaa katika mioyo ya mwanadamu” sasa? (Ni maneno ya Mungu, njia ya Mungu na ukweli Wake yanayokuwa maisha ya mwanadamu.) Umekariri hili, siyo? Natumai sasa mna uelewa wa kina. Watu wengine wanaweza kuuliza, “Kwa hivyo mbona useme kwamba wajumbe na malaika wa Mungu si watakatifu?” Mnafikiria nini kuhusu swali hili? Labda hamjalifikiria mbeleni. Nitatumia mfano rahisi: Unapowasha roboti, inaweza kucheza ngoma na kuongea, na unaweza kuelewa inachosema, lakini unaweza kuiita nzuri? Unaweza kuiita yenye uhai? Unaweza kusema haya, lakini roboti hii haitaelewa kwa sababu haina uhai. Unapozima uletaji wake wa umeme, bado inaweza kusongasonga? (La.) Wakati roboti hii inaamshwa, unaweza kuona ina uhai na ni nzuri. Unaitathmini, iwe tathmini ya kina au ya juujuu, lakini iwe vipi macho yako yanaweza kuiona ikisonga. Lakini unapozima uletaji wake wa umeme, unaona tabia ya aina yoyote kwake? Unaona ikiwa na kiini cha aina yoyote? Unaelewa maana ya kile ninachosema? (Ndiyo.) Unaweza kuelewa, sivyo? Hivyo ni kusema, ingawaje roboti hii inaweza kusonga na inaweza kuacha, kamwe hungeweza kuielezea kama kuwa “na aina yoyote ya kiini.” Huu si ukweli? Hatutazungumzia haya zaidi. Yametosha kwenu kuwa na uelewa wa jumla wa maana. Hebu tutamatishe ushirika wetu hapa. Kwaheri!
Desemba 17, 2013
Tanbihi:
a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kivilinganisha.
b. “Fingo la pete ya dhahabu” inarejelea riwaya maarufu ya Kichina “Safari ya Magharibi,” ambamo mtawa Xuanzang anatumia fingo kumleta tumbili mfalme chini ya udhibiti kwa kutumia pete ya dhahabu iliyowekwa juu ya kichwa cha tumbili mfalme inayoweza kukazwa kwa uchawi, hivyo kumpa maumivi yasiyovumilika ya kichwa. Baadaye ikawa sitiari ya kuwafunga watu.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu
Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu
Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni