Jumapili, 27 Agosti 2017

Umeme wa Mashariki | Mtu Fisadi Hawezi Kuwakilisha Mungu

       
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki | Mtu Fisadi Hawezi Kuwakilisha Mungu

Umeme wa Mashariki | Mtu Fisadi Hawezi Kuwakilisha Mungu

Mwenyezi Mungu alisema: Binadamu amekuwa akiishi katika funiko la ushawishi wa giza, huku akiwa amezingirwa na kufunikwa bila ya kuwachiliwa na ushawishi wa Shetani. Nayo hulka ya binadamu, baada ya kushughulikiwa na Shetani, inaendelea kuzoroteka kwa ufisadi. Vinginevyo, binadamu huishi akiwa katika hulka ile fisadi na ya kishetani, asiweze kumpenda Mungu kwa kweli. Kwa hiyo, kama binadamu atataka kumpenda Mungu, lazima anyang'anywe uadilifu wa kibinafsi, umuhimu wake-binafsi, kiburi, majivuno, na sifa nyingine kama hizo zinazomilikiwa na hulka ya Shetani. Vinginevyo, upendo wa binadamu ni upendo usiokuwa safi, kwa ujumla ni upendo wa Shetani, na ule ambao hauwezi kabisa kupokea idhini ya Mungu.Kama binadamu hatafanywa mtimilifu kwa njia ya moja kwa moja, kushughulikiwa, kuvunjwa, kupogolewa, kutiwa nidhamu, kuadibiwa, au kusafishwa na Roho Mtakatifu, basi hakuna yeyote yule atakayeweza kumpenda Mungu kwa kweli. Ukisema kwamba sehemu ya hulka yako inamwakilisha Mungu na hivyo basi unaweza kumpenda Mungu kwa kweli, basi wewe ndiwe unayezungumza maneno ya kiburi na kwa hakika wewe ni binadamu mpumbavu. Binadamu kama hao ni malaika mkuu! Maumbile ya ndani ya ndani ya binadamu hyawezi kumwakilisha Mungu kwa njia ya moja kwa moja. Lazima binadamu ayaondoe ndani yake kupitia kwa ukamilifu wa Mungu, kisha kutunza na kutosheleza mapenzi ya Mungu na kupitia kwa kazi ya Roho Mtakatifu, kabla ya maisha yake ya kudhihirisha kuidhinishwa na Mungu. Hakuna anayeishi katika mwili anayeweza kumwakilisha Mungu kwa njia ya moja kwa moja isipokuwa kama yeye ni binadamu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu. Hata hivyo, hata hulka ya mtu kama huyo na kuishi kwa kudhihirishwa kwake vyote haviwezi kuchukuliwa kwamba vinawakilisha Mungu kabisa; inaweza kusemekana tu kwamba kuishi kwa kudhihirishwa kwake kunatawaliwa na Roho Mtakatifu. Hulka ya mtu kama huyo haiwezi kumwakilisha Mungu.
Ingawa hulka ya binadamu inaamrishwa na Mungu — hali hii haina mjadala na inaweza kuchukuliwa kama jambo zuri — imefanyiwa mchakato na Shetani. Ndiyo maana hulka zote za binadamu kwa kweli ni hulka ya Shetani. Binadamu anaweza kusema kwamba Mungu, kwa hulka yake, hana ukora katika kazi Yake, na kwamba yeye pia anao mwenendo huu; yeye pia anayo aina hii ya tabia, na hivyo basi anasema kwamba hulka yake inamwakilisha Mungu. Huyu ni binadamu aina gani? Hulka yenye ufisadi na kishetani inaweza kumwakilisha Mungu? Yeyote yule anayetangaza kwamba hulka yake ni uwakilishi wa Mungu anamkufuru Mungu, na ni matusi kwa Roho Mtakatifu! Tukiangalia namna ambavyo Roho Mtakatifu hufanya kazi, kazi ya Mungu hapa ulimwenguni kwa kweli ni kushinda, hivyo basi, hulka nyingi yenye ufisadi na ya kishetani ya binadamu bado haijatakaswa. Kile ambacho binadamu huishi kwa kudhihirisha bado ni picha ya Shetani.Ni wema wa binadamu na unawakilisha vitendo vya mwili wa binadamu. Kwa usahihi zaidi, inawakilisha Shetani na kwa vyovyote vile haiwezi kuwakilisha Mungu. Hata kama binadamu tayari anampenda Mungu hadi kufikia kiwango ambacho anaweza kufurahia maisha ya mbinguni hapa ulimwenguni, anaweza kutamka kauli kama vile: “Mungu siwezi kukupenda zaidi ya hivi,” na kwamba amefikia kiwango cha juu zaidi, huwezi kusema kwamba anaishi kwa kudhihirisha Mungu au kuwakilisha kusudio la Mungu, kwani hali halisi ya binadmu ni tofauti na ile ya Mungu. Binadmu hawezi kutimiza ndoto ya kuishi kwa kumdhihirisha Mungu, acha kuwa Mungu. Kile ambacho binadamu anachokiishi kwa kudhihirisha, kama kinavyotawaliwa na Roho Mtakatifu, ni kulingana tu na kile ambacho Mungu anahitaji binadamu kuwa.
Vitendo vyote na matendo ya Shetani vinaonyeshwa kupitia kwa binadamu. Sasa vitendo vyote na matendo yote ya binadamu ni maonyesho ya Shetani na hivyo basi haviwezi kuwakilisha Mungu. Binadmu hawezi kutimiza ndoto ya kuwa kama Mungu, acha kuwa Mungu. Baadhi ya wanaume ni wenye tabia nzuri; Mungu anaweza kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa hulka hiyo nayo kazi yao inatawaliwa na Roho Mtakatifu, ingawa hulka yao haiwezi kumwakilisha Mungu. Kazi ambayo Mungu hufanya ndani yao ni kule tu kufanyia kazi na kupanua kile ambacho tayari kimo ndani yao. Wawe ni manabii kutoka kwenye enzi zilizopita au binadamu wanaotumiwa na Mungu, hakuna yeyote kati yao anayeweza kumwakilisha Mungu kwa njia ya moja kwa moja. Binadamu wote wanatokea kumpenda Mungu tu kutokana na shurutisho kutoka katika mazingira yao, na hakuna kati yao hulenga kuwa na kusudio la kushiriki. Mambo chanya ni yapi? Kile ambacho kinatoka kwa njia ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu ni kizuri. Hata hivyo, hulka ya binadamu imefanyiwa mchakato na Shetani na haiwezi kumwakilisha Mungu. Ni mapenzi tu, nia ya kuteseka, haki utiifu, unyenyekevu na ufiche wa Mungu mwenye mwili huonyesha waziwazi uwakilishi wa Mungu. Hii ni kwa sababu Alipokuja, Hakuwa na dosari yoyote ya dhambi na alikuja moja kwa moja kutoka kwa Mungu; Hajafanyiwa mchakato wowote na Shetani. Yesu yumo tu kwenye ufananishi wa mwili wenye dhambi na wala hawakilishi dhambi; kwa hivyo, vitendo Vyake, matendo na maneno, mpaka wakati ule kabla ya mafanikio Yake ya kazi husika kupitia kwa kusulubishwa (pamoja na kusulubishwa) vyote ni viwakilishi vya moja kwa moja vya Mungu. Tukio hili la Yesu linatosha kuthibitisha kwamba binadamu yeyote aliye na asili ya dhambi hawezi kumwakilisha Mungu, na kwamba dhambi ya binadamu inamwakilisha Shetani. Hivyo ni kusema kwamba dhambi haimwakilishi Mungu na Mungu hana dhambi. Hata kazi inayofanywa ndani ya binadamu na Roho Mtakatifu inaweza tu kuchukuliwa kuwa ilitawaliwa na Roho Mtakatifu na haiwezi kusemwa kwamba ilifanywa na binadamu kwa niaba ya Mungu. Kwa kadri ambavyo binadamu anahusika, si dhambi yake wala hulka yake inamwakilisha Mungu. Tukiangalia kazi iliyofanywa ndani ya binadamu na Roho Mtakatifu leo na kwenye siku zilizopita, wingi wa kazi hizo zilitekelezwa na Roho Mtakatifu. Hali hii ndiyo iliyomruhusu binadamu kuishi madha ya kudhihirisha. Hata hivyo, huu ni upande mmoja, na wachache sana wanaweza kuishi kwa kudhihirisha ukweli baada ya kushughulikiwa na kutiwa nidhamu na Roho Mtakatifu. Kwa hiyo tunasema kwamba kazi ya Roho Mtakatifu tu ndiyo iliyopo na ushirikiano kwa upande wa binadamu haupo. Je unaliona suala hili kwa uwazi zaidi sasa? Kwa hiyo, ni nini unachofaa kufanya ili kufanya kazi kwa bidii kwa ushirikiano na Roho Mtakatifu na, kwa kufanya hivyo, kutimiza wajibu wako?


kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili

Kujua zaidi:  Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni