Liu Zhen, mwenye umri wa miaka 78, ni mke wa nyumbani wa kawaida wa mashambani. Baada ya kumwamini Mungu, alihisi furaha isiyo na kisawe na kusoma maneno Yake na kuimba nyimbo za kumsifu siku zote, na mara nyingi kukusanyika pamoja na ndugu zake kushirikiana juu ya ukweli. ... Hata hivyo, mambo mazuri hayadumu. Anakamatwa na kuteswa na serikali ya Kikomunisti ya China, ikimtia katika shida mbaya sana. Polisi wanampeleka kwenye kituo cha polisi kwa ajili ya kuhojiwa mara tatu, na kumwonya asimwamini Mungu tena.
Kuelewa Mapenzi ya Mungu Katikati ya Matatizo
Xiao Rui Mji wa Panzhihua, Mkoa wa Sichuan
Nilipokuwa nikihubiri injili nilikutana na viongozi wa madhehebu ambao walisema uongo ili kupinga na kuvuruga, na kuwaita polisi. Hili lilisababisha wale niliokuwa nikihubiria kutothubutu kuwasiliana nasi, na wale ambao walikuwa tu wameikubali injili kutoweza kuwa na imani katika kazi ya Mungu. Nilipofanya kazi kwa bidii sana lakini matokeo yalikuwa duni, nilifikiri: kazi ya Kiinjili ni ngumu sana kutekeleza.