Watu Wasio na Hila Sio Lazima Wawe Waaminifu
Cheng Mingjie Jiji la Xi'an, Mkoa wa Shaanxi
Mimi hujiona kuwa mtu wa aina ya kuwa wazi na mchangamfu. Mimi huzungumza na watu kwa njia ya waziwazi; chochote ninachotaka kusema, mimi husema—mimi sio aina ya mtu wa kuzungukazunguka. Katika kuingiliana kwangu na watu mimi huwa ni mwaminifu na wazi kiasi. Mara kwa mara, mimi hudanganywa na kudhihakiwa kwa sababu ya kuwaamini wengine kwa urahisi.