Jumapili, 27 Mei 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | 72. Nilijifunza Kufanya Kazi na Wengine

Liu Heng    Mkoa wa Jiangxi
Kupitia neema na kuinuliwa kwa Mungu, nilichukua jukumu la kuwa kiongozi wa kanisa. Wakati huo, nilikuwa na shauku mno na niliweka azimio mbele ya Mungu: Bila kujali kinachonikabili, sitayatelekeza majukumu yangu. Nitafanya kazi vizuri na yule dada mwingine na nitakuwa mtu anayetafuta ukweli. Lakini nilikuwa nimeamua tu, na sikujua jinsi ya kuingia katika uhalisi wa uhusiano wa kufanya kazi kwa mpangilio wa kuridhisha. Nilipoanza mwanzo kushirikiana na dada ambaye nilikuwa nikifanya kazi naye, na tulipokuwa na maoni tofauti au migogoro, ningemwomba Mungu kwa uwazi nikimuuliza Yeye kuulinda moyo wangu na roho yangu ili nisimlaumu mshirika wangu. Hata hivyo, niilizingatia tu kudhibiti vitendo vyangu ili nisiwe na migogoro na mshirika wangu, kwa hivyo sikuwa nimeingia katika ukweli. Kwa hiyo, baada ya muda, nilikuwa na kutoafikiana zaidi na zaidi na dada huyu. Wakati mmoja nilitaka kumpandisha cheo dada mmoja kwa kazi ya kunyunyizia na dada niliyekuwa nikifanya kazi naye alisema kuwa dada huyo hakuwa wa kufaa.

Jumamosi, 26 Mei 2018

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (5) - Kukubali Mwenyezi Mungu Pekee Ndiko Kuambatana na Nyayo za Mwanakondoo

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (5) - Kukubali Mwenyezi Mungu Pekee Ndiko Kuambatana na Nyayo za Mwanakondoo

Wachungaji na wazee wa ulimwengu wa dinimara nyingi huhubiri kwa waumini kuwa Bwana Yesu alisulubishwa msalabani kwa ajili ya dhambi za kila mmoja na kuwa mwanadamu amekombolewa kutoka kwa dhambi. Wanahubiri kuwa, mtu anapomwacha Bwana Yesu na kuamini Mwenyezi Mungu, ni sawa na kumsaliti Bwana Yesu na kuasi imani. Je, hakika ukweli uko hivi? Bwana Yesu alipokuja kufanya kazi Yake wakati huo, je, wale walioiacha hekalu na kumfuata Bwana Yesu hawakushutumiwa pia na Mafarisayo Wayahudi kwa njia hii kuwa wanasaliti Yehova Mungu? Hivyo, je, kukubali kazi mpya ya Mungu ni kuasi imani na kumsaliti Mungu? Au ni kuambatana na nyayo za Mwanakondoo na kupata wokovu wa Mungu? Tutaangazia masuala haya pamoja katika video hii fupi.

Ijumaa, 25 Mei 2018

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (4) - Ni Kwa Nini Bwana Aliyerejelea Amechukua Jina la "Mwenyezi Mungu"?

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (4) - Ni Kwa Nini Bwana Aliyerejelea Amechukua Jina la "Mwenyezi Mungu"?

Biblia inatabiri, "Nitaliandika jina la Mungu wangu juu yake, na jina la mji wa Mungu wangu, ambao ni Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu: na nitaliandika juu yake jina langu jipya" (Ufunuo 3:12). "you shall be called by a new name, which the mouth of the LORD shall name" (Isaiah 62:2). Katika siku za mwisho, Mungu anaonekana kwa mwanadamu kwa jina la "Mwenyezi Mungu," anafanya kazi Yake ya hukumu akianzia nafamilia ya Mungu na kufichua tabia Yake ya haki, ya uadhama na ghadhabu. Umuhimu wa jina la "Mwenyezi Mungu" ni mkubwa sana; je, unajua umuhimu wa jina hili ni upi? Video hii itakupa jibu.

39. Kutumia Neno la Mungu Kama Kioo

Wu Xia    Mji wa Linyi , Mkoa wa Shandong
Baada ya kuikubali kazi hii na kula na kunywa neno la Mungu, ilikuwa dhahiri kwangu kwamba ni muhimu sana kwamba mimi nijifahamu. Kwa hiyo, nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, nilihakikisha nimejithibitisha tena dhidi ya neno ambalo Mungu humfichua mwanadamu. Katika hali nyingi, niliweza kutambua kasoro zangu na upungufu. Nilihisi kwamba ningekuja kujifahamu kweli. Hata hivyo, ilikuwa ni kwa njia ya ufunuo kutoka kwa Mungu tu nilipoweza kuona kwamba kwa hakika sikujifahamu kulingana na neno la Mungu.

Alhamisi, 24 Mei 2018

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (3) - Umuhimu wa Jina la Mungu

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (3) - Umuhimu wa Jina la Mungu

"Yehova" na "Yesu" yalikuwa ni majina ya Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, na imetabiriwa katika Ufunuo kuwa Mungu atakuwa na jina jipya katika siku za mwisho. Ni kwa nini Mungu anaitwa kwa majina tofauti katika enzi mbalimbali? Majina haya mawili ya "Yehova" na "Yesu" yana umuhimu gani? Video hii fupi itakusaidia kukutatulia fumbo hili.

46. Maana halisi ya "Uasi dhidi ya Mungu"

Kanisa la Mwenyezi Mungu, ushuhuda, Umeme wa Mashariki

46. Maana halisi ya "Uasi dhidi ya Mungu"


Zhang Jun    Mji wa Shenyang, Mkoa wa Liaoning
Katika siku za nyuma, niliamini kuwa "uasi dhidi ya Mungu" ilimaanisha kumsaliti Mungu, kuacha kanisa, au kuutelekeza wajibu wa mtu. Nilidhani tabia hizi hufanyiza uasi. Kwa hiyo, wakati wowote niliposikia kuhusu watu wakihusika katika tabia hizo, ningejikumbusha kwamba sipaswi kuasi dhidi ya Mungu kama walivyofanya. Aidha, nilikuwa mwangalifu katika jitihada zangu zote na nilishikilia kazi zote nilizopewa na kanisa. Sikurudi nyuma kutoka kwa wajibu wangu wakati niliposhughulikiwa na kupogolewa wala kuondoka kutoka kanisani nilipojaribiwa, bila kujali shida. Kwa hiyo, niliamini kwamba sikuwahi kuasi dhidi ya Mungu kamwe. Nilihisi kuwa nilikuwa nimepata hadhi fulani tayari na nilikuwa na hakika kwamba ningemfuata Mungu mpaka mwisho na hatimaye kufanikisha wokovu.