Jumanne, 22 Mei 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sisitiza Zaidi Kwa Uhalisia

Mwenyezi Mungu alisema, Kila mtu ana uwezekano wa kukamilishwa na Mungu, kwa hiyo kila mtu anapaswa kuelewa ni huduma gani kwa Mungu itakayofaa zaidi makusudi ya Mungu. Watu wengi hawajui kumwamini Mungu humaanisha nini na hawajui chochote kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu. Yaani, watu wengi sana hawana ufahamu wa kazi ya Mungu au lengo la mpango wa usimamizi wa Mungu. Hadi leo, watu wengi sana bado wanadhani kumwamini Mungu kunahusu kwenda mbinguni na roho zao kuokolewa. Bado hawajui chochote kuhusu umuhimu mahususi wa kumwamini Mungu, na aidha hawana ufahamu wowote wa kazi muhimu kabisa ya Mungu katika mpango Wake wa usimamizi. Kwa aina zote za sababu zao binafsi, watu hawavutiwi na kazi ya Mungu na hawatafakari juu ya makusudi ya Mungu au mpango wa Mungu wa usimamizi.

Jumatatu, 21 Mei 2018

Wimbo wa Sifa "Upendo wa Kweli wa Mungu" | Haleluya! Msifuni Mungu! (Korean Song Swahili Subtitle)

Wimbo wa Sifa "Upendo wa Kweli wa Mungu" | Haleluya! Msifuni Mungu! (Korean Song Swahili Subtitle)


Leo naja mbele ya Mungu tena,
naona uso Wake wa kupendeza.
Leo naja mbele ya Mungu tena,
nimeacha siku zangu za zamani za kuzurura nyuma yangu.
Leo naja mbele ya Mungu tena,
kufurahia neno Lake kunanijaza na furaha.
Leo naja mbele ya Mungu tena,
moyo wangu una mengi ya kusema.
Ni maneno Yake mororo yanayoninyunyizia
na kunirutubisha ili nikue.

Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu


Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu



Mwenyezi Mungu alisema, Kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni mojawapo ya hatua muhimu sana za kuingia katika maneno ya Mungu, na ni funzo ambalo watu wote sasa wana haja ya haraka kuingia ndani. Njia za kuingia za kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni:
1. Ondoa moyo wako kwa mambo ya nje, tulia mbele ya Mungu, na uombe Mungu kwa moyo uliolenga.
2. Moyo wako ukiwa umetulia mbele ya Mungu, kula, kunywa, na kufurahia maneno ya Mungu.
3. Yafanye mazoea ya kawaida kutafakari na kuzingatia maneno ya Mungu na kufikiri kazi ya Mungu na moyo wako.

Jumapili, 20 Mei 2018

New Swahili Gospel Movie "Jina la Mungu Limebadilika?!" | Kufunua Siri ya Jina la Mungu

New Swahili Gospel Movie "Jina la Mungu Limebadilika?!" | Kufunua Siri ya Jina la Mungu

Jina lake ni Wang Hua, na ni mhubiri wa kanisa la nyumbani Kusini mwa Uchina. Baada ya kuanza kumwamini Bwana, alipata kwenye Biblia kuwa Mungu aliitwa Yehova katika Agano la Kale, na aliitwa Yesu katika Agano Jipya. Ni kwa nini Mungu ana majina tofauti? Wang Hua alishangazwa sana na hili. Alijaribu kutafuta jibu katika Biblia, lakini akakosa kuelewa fumbo hilo... Lakini alikuwa na imani thabiti kuwa hakuna jina lingine chini ya mbingu lililopewa wanadamu, hivyo Yesu pekee ndiye Mwokozi, na kuwa muradi tushikilie jina la Yesu, bila shaka tutanyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni. Hata hivyo, siku moja Wang Hua alisikia habari za kushtusha: jina la Mungu limebadilika! Baada ya hapo, moyo wake haungetulia tena …

Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Maono ya Kazi ya Mungu (3)


Mara ya kwanza Mungu alipopata mwili ilikuwa kupitia kutungwa mimba kwa Roho Mtakatifu, na ilihusiana na kazi Aliyokusudia kufanya. Jina la Yesu liliashiria mwanzo wa Enzi ya Neema. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu.

Jumamosi, 19 Mei 2018

Swahili Christian Video "Mtoto, Rudi Nyumbani" | Hakuna Wokovu Ila Kupitia Kwa Bwana


Swahili Christian Video "Mtoto, Rudi Nyumbani" | Hakuna Wokovu Ila Kupitia Kwa Bwana

Li Xinguang ni mwanafunzi wa shule ya upili ya ngazi ya juu. Alikuwa mvulana mwenye busara na mwenye tabia nzuri tangu alipokuwa mdogo. Wazazi wake na walimu wake walimpenda sana. Alipokuwa akienda katika shule ya kati, alipumbazwa na michezo ya kompyuta ya mtandaoni. Angekosa kwenda darasani mara kwa mara ili aende kwenye chumba cha mtandao. Wazazi wake walifanya kila juhudi kumsaidia kuyaondoa mazoea yake ya michezo.