Ijumaa, 18 Mei 2018

Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu

Kwa mwanadamu, haiwezekani kwa wana wa Moabu kuwa wakamilifu na hawajahitimu kufanywa hivyo. Wana wa Daudi, kwa upande mwingine, hakika wana matumaini na hakika wanaweza kufanywa kamili. Kwa sharti kwamba mtu ni mzawa wa Moabu, basi hawezi kufanywa kamili. Hata leo, bado hamjui umuhimu wa kazi inayofanyika miongoni mwenu; mpaka katika hatua hii ya sasa bado mnashikilia matumaini yenu ya baadaye katika mioyo yenu na hamtaki kuyaacha. Hakuna mtu anayejali ni kwa nini leo Mungu amewachagua tu—kikundi kisichostahili mno—kukifanyia kazi, hivyo je, kazi hii inafanywa vibaya? Je, hii ni kazi ya uangalizi wa muda mfupi? Kwa nini Mungu ameshuka chini bila upendeleo kufanya kazi kati yenu, ingawaje Amekuwa akijua kwa muda mrefu kwamba nyinyi ni wana wa Moabu?

Alhamisi, 17 Mei 2018

"Imani katika Mungu" (6) - Imani ya Kweli katika Mungu Inamaanisha Nini?

"Imani katika Mungu" (6) - Imani ya Kweli katika Mungu Inamaanisha Nini?


Watu wengi wanaamini kwamba imani katika Mungu ni imani katika Biblia, na kwamba kumfanyia Bwana kazi kwa bidii ni uhalisi wa kuamini katika Mungu. Hakuna mtu katika ulimwengu wa dini ana uwezo wa kuelewa kabisa imani ya kweli katika Mungu ina maana gani. Mwenyezi Mungu anasema, “‘Imani katika Mungu’ inamaanisha kuamini kuwa kuna Mungu; hii ndiyo dhana rahisi zaidi ya imani katika Mungu. Zaidi ya hayo, kuamini kuwa kuna Mungu sio sawa na kuamini katika Mungu kwa ukweli; bali, ni hali ya imani sahili ikiwa na vipengee vya uzito vya kidini. Imani ya kweli katika Mungu ina maana kupitia maneno na kazi ya Mungu kwa msingi wa imani kuwa Mungu ndiye mkuu juu ya vitu vyote. Kwa hivyo mtakuwa huru kutokana na tabia yenu ya upotovu, mtatimiza hamu ya Mungu, na mtapata kumjua Mungu. Ni kwa kupitia safari ya aina hii tu ndio mnaweza kusemekana kuwa mnaamini katika Mungu." ( Neno Laonekana katika Mwili).

Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Maono ya Kazi ya Mungu (2)


Mwenyezi Mungu alisema, Enzi ya Neema ilihubiri injili ya toba, na alimradi mwanadamu aliamini, basi angeokolewa. Leo, badala ya wokovu kuna majadiliano tu ya ushindi na ukamilifu. Haisemwi katu kwamba mtu mmoja akiamini, familia yake yote itabarikiwa, au kwamba wokovu ni ya mara moja na kwa wote. 

Jumatano, 16 Mei 2018

"Imani katika Mungu" (5) - Je, Kufanya Kazi kwa Bidii kwa ajili ya Bwana ni Uhalisi wa Imani katika Bwana?

"Imani katika Mungu" (5) - Je, Kufanya Kazi kwa Bidii kwa ajili ya Bwana ni Uhalisi wa Imani katika Bwana?


Waumini wengi huamini kwamba mradi tunalilinda jina la Bwana, kuomba mara kwa mara, kusoma Biblia na kuwa na mikutano, na mradi sisi huyaacha vitu, hutumia rasilmali na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya Bwana, basi hii ni imani ya kweli katika Bwana, na tutaweza kunyakuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni Bwana atakaporudi. Je, aina hii ya mtazamo ni sahihi? Wengi wataniita siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujafanya unabii kwa jina lako? na kwa jina lako kutoa pepo? na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Halafu nitasema wazi kwao, Sikuwajua nyinyi kamwe: ondokeni mbele yangu, nyinyi watenda maovu."

Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

Mwenyezi Mungu alisema, Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kutambuliwa na Mungu. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza kuwa na imani kwa Mungu, kwani mwanadamu kwa moyo wake wote hutafuta mambo yaliyo juu na hakuna aliye tayari kubaki nyuma ya wengine. Hii ndiyo njia ya mwanadamu. Kwa sababu hii, wengi kati yenu wanajaribu daima kupata neema ya Mungu mbinguni, lakini kwa kweli, uaminifu wenu na uwazi kwa Mungu ni wa kiasi kidogo sana ukilinganishwa na uaminifu na uwazi wenu kwenu wenyewe.

Jumanne, 15 Mei 2018

"Imani katika Mungu" (4) - Je, Kuamini katika Biblia ni Sawa na Kuamini katika Bwana?

"Imani katika Mungu" (4) - Je, Kuamini katika Biblia ni Sawa na Kuamini katika Bwana?

Watu wengi zaidi katika ulimwengu wa dini huamini kwamba Biblia ni kanuni ya Ukristo, kwamba mtu lazima ashikilie Biblia na kuweka msingi wa imani yake katika Bwana kwenye Biblia kabisa, na kwamba mtu hawezi kuitwa muumini akipotoka kutoka kwenye Biblia. Hivyo imani katika Bwana na imani katika Biblia ni sawa? Uhusiano kati ya Biblia na Bwana ni upi hasa? Bwana Yesu aliwakaripia Mafarisayo wakati fulani kwa maneno haya, "Tafuta katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnadhani kuwa mna uzima wa milele: na hayo ndiyo yananishuhudia. Nanyi hamtakuja Kwangu, kwamba mpate uhai." (Yohana 5:39-40). Biblia ni ushuhuda wa Mungu tu, lakini haina uzima wa milele. Mungu pekee ndiye ukweli, njia na uzima. Kwa hivyo, tuiangalie Biblia vipi kwa njia ambayo inakubaliana na mapenzi ya Bwana?